Papa,washiriki wa mafunzo,'Siblingis':dada na kaka katika ulemavu na ugonjwa wa akili
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Baba Mtakatifu aliwatumia salamu washiriki wa Siku ya Mafunzo “Siblings:kaka na dada katika ulemavu na magonjwa ya kiakili”, ambayo ilifanyika asubuhi Jumamosi tarehe 18 Februrari 2023 katika Ukumbi wa Trois huko Trastevere, jijini Roma, Siku hiyo ya Mkutano wa mafunzo iliandaliwa na Chama Jumuiya ya Arck “Il Chicco”, kinachojikita na shughuli za walemavu wenye usumbufu wa mfuno wa neva ya kiakili. Baba mtakatifu kwa maana hiyo katika salamu hizo amekuwa na furaha kubwa kuwapongeza kwa kuanzisha mpango huo mzuri. Na katika siku ya mafunzo kuhusu mada ya Sblings, alikiri jinsi ambavyo hakulijua neno hilo, lakini anafahamu vyema jambo linamaanisha nini.
Msaada na faraja ya wengine
Papa amesema:“Ni ukweli ambao unatukumbusha kwamba, kuwa bora au mbaya, hakuna mtu aliye peke yake, lakini daima anaishi ndani ya mtandao wa mahusiano. Kwa manufaa, kufaidika na ukaribu, msaada na faraja ya wengine; ni mbaya kwa sababu tatizo la mtu mmoja hurejea kwa wengine kuwa sababu ya kuwa na wasiwasi na mateso. Ulemavu huendeleza athari zake zaidi ya yote katika mazingira ya nyumbani, na katika familia kwa ujumla.”
Kubeba msalaba kama mkirene
Baba Mtakatifu Francisko alibainisha kuwa kaka au dada mwenye afya wa kaka au dada mwenye ulemavu anafanana na yule Simoni aliyetoka Kirene na kulazimishwa na maaskari kubeba msalaba wa Yesu kwa mwendo mrefu wa Njia ya Uchungu. Ndugu mwenye afya ni mtu ambaye maisha yamemlazimisha kuwa Mkirene. Anaweza kuwa katika sehemu ya barabara iliyofunikwa na huyu ndugu wa Kirene, na ambayo inaweza kuwa ndefu zaidi au kidogo, lakini mwanzoni mpango huo tayari umeandaliwa; na yeye itamlazimu kushiriki na kubeba msalaba wa mwingine, wa kaka/dada yake mwenyewe ambamo Yesu amefichwa.
Yesu haoni aibu kuwa na sisi
Baba Mtakatifu alibainisha jinsi alivyoona ilivyokuwa programu yao na ripoti ambayo, katika kichwa, inanukuu kifungu kutoka kwa Waraka kwa Waebrania 2, 11 huku ikirejeea kwa usahihi Yesu ambaye haoni haya kutuita ndugu. Papa Francisko kwa hiyo, alifurahishwa na kumbukumbu kuwa hiyo ni kwa sababu iko hivyo kwamba Yesu haoni haya, hafanyi matatizo, matatizo yetu yanakuwa yake; Yesu anatupenda jinsi tulivyo, kwa talanta zetu na kwa udhaifu na ulemavu wetu.
Sisi ni njia nyingine mbadala ya mwingine
Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza kuwa Yesu anafurahi kwa sababu sisi ni, na si kwa sababu sisi ni njia moja badala ya nyingine, katika umbo kamili au mbaya. Sisi pia, tunapopenda hatufanyi kwa kile ambacho mwingine anacho au anajua jinsi ya kufanya, lakini kwa kile ambacho mwingine hana na kwa ajili ya Upendo. Upendo ni huo ni kutaka mwingine awe nacho; kwa namna nyingine kuwa kama yeye, si kama tunavyofikiri anapaswa kuwa, bali kulingana na viwango vilivyoainishwa. Na hapo ndipo upendo hauzalishi ubadhirifu au ubaguzi.
Mfumo wa ushuhuda halisi
Ni hali iliyoenea na ngumu, ya kushangaza ambayo ipo chini ya neno hilo, msaidizi wa ndugu, wa ulemavu wa nyumbani na familia, na ni sawa na ya haraka kwamba iwekwe katikati ya umakini wa siku za mafunzo kama hiyo waliyofanya, ambayo iliwaona watu mbalimbali wa tamaduni na mbinu mbalimbali ambazo zilikabiliwa, pamoja na ushiriki hai wa baadhi ya ndugu ambao wataleta uzoefu wao wa moja kwa moja, hali halisi katika mfumo wa ushuhuda. Papa Francisko akiwapongeza wabunifu na waandaaji, aliwatakia kazi njema na yenye matunda, akitumaini kuwa tukio hilo lingekuwa mbegu yenye uwezo wa kuzaa matunda mengi.