Papa,nia za maombi:Tusali kwa ajili ya anayehatarisha maisha kwa ajili ya Injili!
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko mara nyingi amekuwa akisema kwamba “Kuna mashuhuda zaidi leo kuliko siku za kwanza za Kanisa. Kaka na dada zetu wengi ambao hutoa ushuhuda wao wa Yesu na wanateswa. Kwa njia hiyo tarehe 11 Februari 2023 zimechapishwa nia za maombi ya Papa katik mtandao wake wa sala kwa mwaka ujao 2024. Kwa maana hiyo kila mwezi unajikita na nia ya maombi. Kama vile a,nayp imetolewa kwa hakika kwa ajili ya mashuhuda wa Kikristo kwamba: “Tuombe kwa sababu wale ambao katika sehemu mbali mbali za ulimwengu huhatarisha maisha yao kwa ajili ya Injili waweze kuambukiza Kanisa ujasiri wao na msukumo wa kimisionari.
Papa ametoa mwaliko mara kwa mara ili kufikiria juu ya Wakristo wengi ambao walikuwa wamefungwa kwenye magereza ya Wanazi na Wakomunisti, kwa sababu tu walikuwa Wakristo, lakini hiyo ndio hufanyika hata leo. Kuna mateso kwa sababu ulimwengu hauvumilii umungu wa Kristo, hauvumilii kutangazwa kwa Injili, anasisitiza Papa. Jibu la Kikristo kwa uovu huo ni upendo. Papa Francesco pia alikuwa alisisitiza hilo tena mnamo Februari 2020 huko Bari, katika fursa ya mkutano kuhusu “Mpaka wa Amani ya Mediterranean”.
Kwa hiyo “Wapende maadui zenu na uwaombee wale wanaowatesa. Ni mambo mapya ya Kikristo. Ni tofauti ya Kikristo. Kuomba na Kupenda: Hapa ndio tunapaswa kufanya; Na sio tu kwa wale wanaotupenda, sio tu kwa marafiki, sio tu kwa watu wetu. Kwa sababu upendo wa Yesu haujui mipaka na vizuizi. Bwana anatuomba kuwa na ujasiri wa upendo bila mahesabu. Kwa sababu kipimo cha Yesu ni upendo bila kipimo”, Papa anakabidhi nia hiyo tena kwa mwezi mwingine.
Na Tena katika nia nyingine: “Ni mara ngapi tumepuuza maombi yake, kwa kuishi kama wote! Na bado amri ya upendo sio uchochezi rahisi, ni juu ya moyo wa Injili. Kwa upendo kwa wote bila kukubali udhuru, hatuhubiri busara nzuri. Kwa sababu Bwana hakuwa mwenye busara hakushuka kuhaidi, bali alituomba kuhusu msimamo mkali wa upendo. Ni msimamo halali wa Kikristo tu na msimamo mkali wa upendo.”
Katika nia hizo pia kuna sala kwa ajili ya viongozi wa kisiasa, kwa sababu wako kwenye huduma ya watu wao, wafanye kazi kwa ajili ya maendeleo kamili ya wanadamu na kwa ajili ya faida ya kawaida, na wapendelee maskini zaidi. Nguvu sio ukandamizaji au unyonyaji, amesema Baba Mtakatifu Francisko kwa hiyo Nguvu ni huduma.