Tafuta

Waandamanaji nchini Nicaragua wakitaha haki kwa waliohukumiwa kifungo miongoni kwao Askofu Rolando Alvarez wa Matagalpa kuhukumiwa kifungo cha miaka 26. Waandamanaji nchini Nicaragua wakitaha haki kwa waliohukumiwa kifungo miongoni kwao Askofu Rolando Alvarez wa Matagalpa kuhukumiwa kifungo cha miaka 26. 

Papa:Sala kwa waathirika wa tetemeko pia kwa Askofu Alvarez wa Nicaragua

Papa katika salamu zake mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana,ameelezea uchungu wake kuhusu taarifa za nchi ya Amerika ya Kati mahali ambapo Askofu Rolando Alvarez wa Matagalpa,amehukumiwa kifungo cha miaka 26.Papa ameomba kusali kwa waliokufa kwa sababu ya tetemeko la Ardhi huko Siria na Uturuki.

Na Angella Rwezaula; -Vatican

Mara baada ya sala ya malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu Francisko Dominika, tarehe 12 Februari 2023, kwa waamini na mahujaji waliunganika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, amesema “Tunaendelea kuwa karibu, kwa maombi na usaidizi madhubuti, kwa watu walioathiriwa na tetemeko la ardhi nchini Siria na Uturuki. Nilikuwa nikitazama katika kipindi cha Asua Immagine”  picha za janga hilo, maumivu haya ya watu hawa wanaoteseka na tetemeko la ardhi. Tuwaombee, na tusisahau, tuwaombee na tufikirie nini tunaweza kuwafanyia. Na tusisahau Ukraine inayoteswa: Bwana afungue njia za amani na awape wale wanaohusika ujasiri wa kuzifuata.

Papa pia aliwaomba waamini wote Jumatano wakti wa Katesi kusali kwa ajili ya Siria na Uturuki
Papa pia aliwaomba waamini wote Jumatano wakti wa Katesi kusali kwa ajili ya Siria na Uturuki

Akiendelea Baba Mtakatifu Francisko ameonesha wasiwasi mkubwa kuhusu habari kutoka Nicaragua  na kwamba amehuzunisha si kidogo na hawezi kukosa kukumbuka kwa wasiwasi Askofu wa Matagalpa, Rolando Alvarez, “ambaye ninampenda sana, alihukumiwa kifungo cha miaka 26 gerezani na pia watu waliofukuzwa  na kuelekea nchini Marekani. Ninawaombea na wote wanaoteseka katika nchi hiyo pendwa”.


Kwa maana hiyo baba Mtakatifu amewageukia waamini akiwaomba sala zao. Na Zaidi tumwombe Mungu  kwa maombezi ya Bikira Maria afungue mioyo ya viongozi wa kisiasa na wananchi wote katika utafutaji wa dhati wa amani inayozaliwa na ukweli, haki, uhuru na upendo na kupatikana kwa zoezi la subira la mazungumzo. Tusali pamoja kwa Mama Yetu. (Ave Maria, Salamu Maria).

Papa hakusahau nchi ya Ukraine,ameomba kuendelea kuiombea
Papa hakusahau nchi ya Ukraine,ameomba kuendelea kuiombea

Ametoa  salamu zake kwa wote, kuanzia kwa waroma na mahujaji kutoka Italia na kutoka nchi nyingine.Hivi vikiwemo  vikundi kutoka Poland, Jamhuri ya Czech na Peru, aidha salamu kwa raia wa congo waliokuwapo unwanja na ambao ameeleza kuwa “, nchi yenu ni nzuri, ni nzuri, iombeeni nchi yenu! Salamu kwa  wanafunzi wa Badajoz (Hispania) na wale wa Taasisi ya Gregoriana ya Lisbon.Vijana wa  Amendolara. Cosenza na kikundi cha  AVIS cha  Estense – Padova. Na hatimaye amewatakia mlo mwema na Dominika njema lakini wasisahau kusali kwa ajili yake.

Papa aliwasalimia hata wanahija kutoka DRC na kueleza jinis nchi yao ni nzuri na waendelee kuiombea
Papa aliwasalimia hata wanahija kutoka DRC na kueleza jinis nchi yao ni nzuri na waendelee kuiombea

Na Baraza la Maaskofu wa Amerika Kusini CELAM na maaskofu wa Chile na Uhispania wamelaani ukiukaji wa haki za binadamu na kufukuzwa kwa wapinzani wa kisiasa wa serikali kutoka nchi hiyo ya Amerika ya Kati, pamoja na kifungo cha miaka 26 jela kilichotolewa kwa Askofu Rolando Álvarez.

Kuhusiana na tetemeko la Siria na Uturuki

Idadi ya waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi nchini Uturuki na Siria inaongezeka kwa saa moja, hadi nyingine na kuzidi vifo vya watu 29,000.  Kwa hiyo Vifo vinaongezeka katika nchi zote mbili, zaidi ya 24,500 huko Siria na  wakati katika Uturuki kuna karibu 4,500. Kushangaza ni utabiri wa Umoja wa Mataifa ambao unaamini kwamba jumla inaweza hata kuwa mara mbili.

Msaada wa kwanza kutoka Umoja wa Ulaya unatarajiwa kuwasili Damasco Dominika tarehe 12 Februari 2023. Utawasili kutoka Italia na kupangwa katika maeneo yaliyoathirika zaidi nchini Siria ambako, kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, zaidi ya watu milioni 5 huenda wamesalia bila kuwa na makazi.

Baada ya Sala ya Malaika wa Bwana 12 .02.2023
12 February 2023, 14:56