Tafuta

2023.02.13 Papa amekutana na ujumbe kutoka Chuo Kikuu cha Sulkhan-Saba Orbeliani(Tbilisi, Georgia). 2023.02.13 Papa amekutana na ujumbe kutoka Chuo Kikuu cha Sulkhan-Saba Orbeliani(Tbilisi, Georgia).  (Vatican Media)

Papa:Mwanga hufungua peo za maarifa ili kuangaza giza la chuki

Kuondoka kwenye giza la ujinga kwenda kwenye mwangaza wa maarifa.Ndiyo kazi ya elimu iliyoelezwa na Papa kwa ujumbe waChuo Kikuu cha Sulkhan-Saba Orbeliani,Tbilisi,Georgia.Katika Chuo Kikuu kuna umuhimu wa utamaduni na imani katika ulimwengu ambao giza huzidi kufanya kusahau na kutojali.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko  Jumatatu tarehe 13 Februari 2023 amekutana na wajumbe wa Chuo Kikuu cha Sulkhan-Saba Orbeliani cha Tibilisi huko Georgia ambacho hivi karibuni kimetimiza miaka 20, na amewapongeza na kuwashukuru kwa ziara yao na kwa kile ambacho wanafanya na kwamba wanatoa mfano mzuri wa utafiti wa utamaduni wa shauku na kutunza ule wema wa ajabu ambao ni wa kukuza vijana katika mafunzo. Elimu inafanya hivyo: inasaidia, kizazi cha vijana kukua, kugundua na kukuza mizizi ya kina ya kuzaa matunda. Baba Mtakatifu Francisko amebainisha juu ya utambulisho wa Geogria, kwamba ni nchi changa, lakini yenye historia ya zamani, ardhi iliyobarikiwa kutoka mbinguni ambayo inahifadhi kumbu kumbu. Papa amefikiria Patriaki Ilia, mtu wa Mungu ambaye anamkumbuka katika maombi yake na ambaye alipenda kusikiliza sala zake zilizomo kwenye muziki.

Mkutano wa Papa na ujumbe kutoka Chuo Kikuu cha Sulkhan-Saba Orbeliani (Tbilisi,Georgia).
Mkutano wa Papa na ujumbe kutoka Chuo Kikuu cha Sulkhan-Saba Orbeliani (Tbilisi,Georgia).

Baba Mtakatifu aidha anazo kumbu kumbu moyoni mwake ile mikutano aliyofanya hasa ile ya Kanisa Kuu la Kipatriaki, ambayo walikuwa karibu mmoja na wingine kama ishara ya joho la Kristo; joho lile ambalo Injili inaeleza “ilikuwa kipande chote kuanzia juu hadi chini (Yh 19,23) na kwa mujibu wa tamaduni , inawakilisha umoja wa Kanisa, na Mwili wa Kristo. Kwa hiyo Chuo kikuu chao kinawakilisha mfano hata kwa maana hiyo ya umoja wa kushirikishana kati ya wakatoliki na Waorthodox katika muktadha wa utamaduni na elimu. Papa amebainisha kwamba katika lugha ya kigeorgia neno Elimu, ganatleba linavutia sana, kwani linatokana na neno mwanga ambao unaelekezea hatua kutoka kwenye giza na ujinga kwenda kwenye mwanga wa maarifa. Kuelimisha kwao ni kuja kwa mara nyingine katika mwanga ambao una maana ya kuangazwa.

Hii ina maana yake, ambayo inafanya kufikia wakati wanawasha taa katika chumba cha giza: hawabadilishi chochote, lakini kuna mabadiliko ya mantiki ya kila kitu. Na ndivyo yalivyo maarifa ambayo yamepokelewa katika chuo kikuu chao, ambao wanapendekeza kuweka kitovu cha hadhi ya mtu binadamu. Kwa njia ya mafunzo na jitihada inawezekana kufikia kama alivyotaja historia za kizamani za Delfi: “kujijua mwenyewe”.  Ni muhimu hata iwa imani ambayo mmonaki mmoja wa kizamani aliandika kuwa “ ikiwa Unataka kujua Mungu”. Anza kujijua mwenyewe. Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kwamba kuna umuhimu wa wema huu wa kuangazwa, wakati katika ulimwengu inakuwa ngumu giza la chuki, ambalo mara nyingi linakuja kutokana na kusahau na sintofahau. Ndiyo mara nyingi kusahau na kutokujali kunaonesha kila kitu ni giza, na kutoeleweka, wakati utamaduni na elimu hurejesha kumbukumbu za zamani na kutoa mwanga juu ya wakati wa  sasa.

Wajumbe wa chuo Kikuu kutoka Georgia
Wajumbe wa chuo Kikuu kutoka Georgia

Kwa hiyo hii ni muhimu kwa ajili ya makuzi ya vijana, lakini hata jamii kwa sababu kama alivyokuwa amesema Baba wa nchi yao: “Kuanguka kwa watu, kunaanzia pale mahali panapoishi kumbu kumbu. Kinyume chake, kwa msaada wa Mungu! “kila kitu kinawezekana kwa mtu aliyeelimishwa”. Kwa hiyo utamaduni wa Gerogia, unaalika kukaa na taa imewaka daima  ya elimu na kuzingatia kufungua dirisha la imani, kwa sababu vyote viwili vinawasha vyumba vya maisha. Sio kwa bahati mbaya, huko Georgia, mzizi ya mwanga, unaonesha iwe katika neno elimu na iwe katika neno la ubatizo ikiwa na maana ya tamaduni na imani.

Baba Mtakatifu amesema historia ya Georgia, inasimulia hatua nyingi za giza katika mwanga, kwa sababu nchi yao daima iliweza kusimama na kuangaza, hata kama wakati mwingi ambapo, mara nyingi ilivamiwa na kutawaliwa na wageni. Watu wao, vijana na ujasiri, wakalimu, na wanaopenda maisha, walijua kukuza, hata katika hatari za giza zaidi, hali chanya, shukrani kwa imani yake na utamaduni wake. Kwa hiyo Kanisa katoliki ni tunu. Imeruhusu fursa za kiutamaduni zenye matunda ambazo historia ya nchi imefaidika nayo. Unawakilisha mwendelezo wa mchango huu na ni jambo zuri kwamba, kwa njia ya furaha na kujenga, unastawisha huduma ya Jumuiya ya Kikatoliki katika ardhi ya Georgia, ili iwe ni mbegu inayozaa matunda kwa ajili ya wote. Amewaalika kuendelea na huduma hiyo ya unyenyekevu na ya kindugu.

Na Papa  anaelewa kwamba, kwa vitivo mbalimbali vilivyopo tayari, wanaongeza ile ya madawa, ambayo itaweza kufanya mengi mazuri. Jukumu hilo la kuunda nafasi na madaraja kwa manufaa ya nchi na watu wake limeandikwa kwa jina la Taasisi yao, iliyowekwa  Sulkhan-Saba Orbeliani, mwanadiplomasia bora wa Georgia, mtu wa utamaduni wa ajabu na uwazi. Watu wa Georgia, kuanzia na ujana wao, wanastahili kuwa na fursa pana zaidi. Na wakati huo huo ubinadamu wa kawaida watu wa Georgia, katika upekee na uzuri wake, unastahili kuthaminiwa mahali pengine, na sanaa yake, fasihi, muziki na maneno mengine mengi muhimu, ambayo yanaweza kuimarishwa kwa kulinganisha kwa heshima na tamaduni nyingine. Mwanga  ni mfano kwao katika hilo pia: kwa sababu haipo ili kuonekana, lakini kwa kuoneesha karibu na zaidi na  hiyo ni utamaduni, ambayo hufungua upeo na kupanua mipaka.

Papa kwa Ujumbe kutoka Chuo kikuu huko Georgia
13 February 2023, 16:13