Papa kwa Vyuo Vikuu vya Kipapa:fanyeni kazi pamoja kwa ari na maono!
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Taasisi za kitaaluma za Kipapa zilizoko Roma ni urithi tajiri sana, ambao unaweza kuhamasisha maisha mapya, lakini ambayo yanaweza pia kuzuia ikiwa zitakuwa za kujitegemea sana au kuwa kama kipande kidogo cha makumbusho. Ni katika maneno ya hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko, wakati wa kukutana na watu wapatao 3,000 katika Ukumbi wa Paulo VI, mjini Vatican wakiwemo wakuu, maprofesa, wanafunzi na wafanyakazi wa vyuo vikuu vya Kipapa jijini Roma, tarehe 25 Februari 2023. Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba hiyo amewashauri kutengeneza kama kwaya ili waweze kukabiliana na changamoto zisizo na kifani za sasa, hasa kwa kuwaalika watazame picha iliyo kwenye Jukwaa hilo ikimuonesha Yesu Mfufuka!
Hasa baada ya janga la Uviko-19, ni uharaka sana wa kuanza mchakato unaopelekea makakati wa maelewano madhubuti, thabiti na ya kiunganisho kati ya taasisi za kitaaluma, ili kuheshimu vyema madhumuni maalum ya kila mmoja na kusaidia utume wa Kanisa katika ulimwengu wote. Baba Mtakatifu kwa hiyo ameonya kwamba wasiende wakibishana kati yao ya kuchukua mwanafunzi kwa saa ya ziada. Kwa hiyo amewaalika wasitake kutafuta suluhishi za muda mfupi, na wasifikirie mchakato huo wa ukuaji kama hatua ya kujihami, inayolenga kukabiliana na kushuka kwa rasilimali za kiuchumi na watu. Badala yake, inapaswa kuonekana kama msukumo zaidi kuelekea siku zijazo na kama mwaliko wa kukubali changamoto za enzi mpya katika historia.
Kutengeneza kwaya kati ya viunga mbalimbali vya jumuiya, ndio Papa amesisitiza zaidi kati ya taasisi mbalimbali za kitaaluma ambazo zilizaliwa jijini Roma kwa karne nyingi kutokana na ukarimu na mtazamo wa mbali wa mashirika mengi ya kidini. kwa hiyo alisema Papa, Francisko kuwa hiyo hujiweka kama inavyohitajika. Kwa kuzingatia idadi ndogo ya wanafunzi na walimu, wingi huu wa vituo vya kusomea unahatarisha kupoteza nguvu za thamani. Kwa hivyo, badala ya kupendelea uenezaji wa furaha ya kiinjili ya kusoma, ya kufundisha na kutafiti, wakati mwingine unatishia kuupunguza kasi na kuwa ngumu, kwa hiyo ni lazima suala hilo lizingatiwe.
Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kuwa “urithi wa karne nyingi wa vitivo vya kipapa na vyuo vikuu lazima uendelezwe, kwa kuanzisha mchakato wa kujiamini haraka iwezekanavyo katika mwelekeo wa kwaya, kwa akili, busara na ujasiri, kwa kuzingatia daima kwamba ukweli ni muhimu zaidi kuliko wazo. Kwa sababu ikiwa unataka kuwa na wakati ujao wenye matunda, ulinzi wake hauwezi kuwa mdogo kwa kudumisha kile kilichopokelewa badala yake ni kwamba iwe wazi kwa ujasiri na ikiwa ni lazima, hata maendeleo ambayo hayajawahi kutokea. Katika suala hilo, Baba Mtakatifu ameelekeza Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu kuwa ndilo rejeo la mawasiliano kwa ajili ya kusindikiza taasisi za kitaaluma katika mchakato wa safari hiyo.
Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba hiyo vile vile ameeleza kwamba “Kwaya ni ukweli wa matumaini” kutokana na kutafakari picha kubwa ya Kristo Mfufuka, ambayo ni kazi ya msanii Pericle Fazzini, inayotawala jukwaa zima la Ukumbi wa Paulo VI, kwamba picha hiyo anaakisi jinsi mikono ya sanamu hiyo inavyofanana na ya mwalimu wa kwaya. Hapo inaonekana kuwaelekeza wanakwaya wote; kwa upande wa kushoto, badala yake utafikiri anapendekeza wazo kwamba anamwita mwimbaji mmoja, akimwambia sasa: “Ni zamu yako”. Hivyo ndivyo mikono ya Kristo inavyoeleza. Kwa hiyo mikono ya Kristo inahusisha kwaya na mwimbaji mmoja kwa wakati mmoja, ili katika tamasha hilo jukumu la maelewano na jingine, liwe katika kukamilishana pamoja. Kwa hiyo Papa ameongeza kuwasihi kwamba: “Tafadhali: kamwe waimbaji wasiwe pekee yao bila kwaya nzima. “Ni zamu yenu” na wakati huo huo: “Ni zamu yako!” Hivyo ndivyo mikono ya Aliyefufuka inavyofafanua. Tunapotafakari ishara zake, basi na tujipyaishe kujitolea kwetu kama kwaya kwa uaminifu na mapatano ya sauti, utulivu na kwa utendaji hai wa Roho."
Kwa upande mwingine, Baba Mtakatifu amesema "Chuo kikuu ni shule ya makubaliano na maelewano kati ya sauti na vyombo tofauti, ameongeza huku akimnukuu Mtakatifu John Henry Newman, mahali ambapo maarifa na mitazamo tofauti hujidhihirisha katika maelewano na kukamilishana, kusahihisha kila mmoja na wengine na wanasawazisha wao kwa wao”. Kwa hiyo maelewano ambayo ni lazima kwanza yakuzwe kuanzia na mtu binafsi kwa kuelewana na akili nyingine tatu ambazo hutetemeka katika nafsi ambazo ni akili, moyo na mikono. Hizo za mwisho, kwa kulinganishwa na wafalsafa Aristotle na Kant kuhusu roho na ubongo wa nje wa mwanadamu, Papa Francisko ameleza kuwa ni Ekaristi kama zile za Kristo, zenye uwezo wa kutoa shukrani, wa huruma, wa ukarimu na kuunga mikono ya wengine. Papa Francisko ametoa mfano binafsi kwamba:“ kwa mara ya kwanza alipotoka nje kweny Uwanja akiwa kama Papa, alikaribia kundi la vijana vipofu. Na mmoja wao alimwambia kama angeweza kumuona: Je, ninaweza kukutazama?”
Papa alisema kwamba hakuelewa, lakini alimjibu kuwaa “Ndiyo”. Kwa hiyo kipofu huyo alimtafuta kwa kumpapasa mikono yake…. Na baadaye alimshukuru Papa kwa sababu alisema alivyoona mikono yake. Kwa hiyo Papa amethibitisha alivyogusa sana na hilo. Kwa njia hiyo akiwaelekea wanachuo amesema kuwa "ikiwa neno linachukua na linaonesha kitendo cha kawaida, pia ni mzizi wa maneno kama vile kuelewa, kujifunza na kushangaa na wakati huo huo mikono inapochukua, akili inaelewa, na inajifunza na ikiwa haijiruhusu kushangaa, ni kutokana na kwamba ili hilo lipate kutendeka mikono iliyo nyeti inahitajika". "Kwa sababu akili haitaweza kuelewa chochote ikiwa mikono imefungwa na tamaa, au ikiwa ni mikono yenye shimo, ya kupoteza muda, afya na vipaji, au bado ikiwa inakataa kutoa amani, salamu na kuunga mikono mingine. Haitawezekana kujifunza chochote ikiwa mikono ina vidole vinavyo nyoshea bila huruma kaka na dada wanaokosea. Na hakutakuwa na kitakachoshangaza ikiwa mikono hiyo hiyo haitaweza kuungana ili kuomba juu mbinguni.