Tafuta

2023.02.13 Ispania, TOLEDO Madhahabu ya Bikira Maria wa Guadalupe: madhabau mawili kuungana. 2023.02.13 Ispania, TOLEDO Madhahabu ya Bikira Maria wa Guadalupe: madhabau mawili kuungana. 

Papa,Guadalupe:madhabahu mawili ya Mexico na Hispania kuungana!

Jumatano 13 Februari imetiwa saini ya makubaliana ya Kanisa Kuu la Monasteri ya Kifalme ya Mtakatifu Maria wa Guadalupe huko Hispania.Papa Francisko katika barua yake ametoa salamu kwa Askofu Mkuu Cerro Chaves wa Toledo na Kadinali Aguiar Retes.Ni migogoro mingapi tungepuka kama tungemwamini Maria?

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Mexico na Hispania zimengana katika ishara ya Bikira Maria, ambaye ubinadamu wote umesimama chini miguuni yake. Maeneo mawili muhimu zaidi yaliyotengwa kwa ajili ya Mama Yetu wa Guadalupe,  na yake ya Morenita de las Villuercas na ile ya Morenita del Tepeyac, na sasa zimeunganishwa. Saini ya makubaliano hayo iliwekwa mnamo tarehe 13 Februari katika Kanisa Kuu la  Monasteri ya Kifalme ya Mtakatifu María wa Guadalupe nchini Hispania. Papa, katika barua kwa Askofu mkuu Francisco Cerro Chaves wa Toledo, ametuma salamu zake kwa “furaha kuu” kwa Kardinali Carlos Aguiar Retes, Askofu mkuu wa  mji wa Mexico na kwa maaskofu wote, mapadre, waliowekwa wakfu na waamini mbao walitaka kujiweka siku hii chini ya miguu ya Bikira Mtakatifu zaidi, kama watu watakatifu wa Mungu peke yake.

Roho Mtakatifu hufanya ishara ya kusikia ujumbe wake katika lugha yake ya kila kabila

Katika barua hiyo Papa anaadika kuwa “Maria, Mama yetu, daima ni kifungo cha ushirika kwa Watu wake. Mama wa Yesu, kwa njia rahisi, anaendelea kutuita. Haya yameelezwa katika sehemu nyingi za dunia kwa mwaliko wa kujenga hekalu ambalo lingekuwa nyumba yenye milango yake wazi kila wakati kwa kila mtu, nyumba ya sala na ushirika". Katika barua iliyoandikwa kwa lugha ya kihispania, Papa Francisko anaendelea kuwa: “ leo hii Jina tamu la Maria linawaleta pamoja, kwa usahihi zaidi jina la milenia ambalo tayari katika mizizi yake ya neno inazungumza nasi juu ya upotovu, wa kukutana na Mungu na wanadamu. Kupotoka kwa sababu wasomi ambao hawawezi kukubaliana kama tunapaswa kusoma jina 'Guadalupe' katika Kiarabu, Kilatino au Nahuatl. Lakini inashangaza kwamba kile kinachoweza kuonekana kama mzozo kinaweza kusomeka kama 'makonyezo' ya Roho Mtakatifu ambaye humfanya kila mtu asikie ujumbe wake wa upendo katika lugha yao wenyewe.

Mto uliofichwa ni chanzo cha maji ya uzima

Kwa hiyo katika lugha ya Kiarabu neno hili lingeweza kusikika kama 'mto uliofichwa', kama vile chanzo cha maji ya uzima ambacho Yesu aliahidi kwa mwanamke Msamaria, nguvu ile ya neema ambayo hata wakati wa kukataliwa na kutokuelewana hulifanya Kanisa kuwa hai. Kama wachungaji, dokezo hili lazima liwe kichocheo cha sisi kutafuta daima katika ule mto mwingine wa neema uliofichwa, ule Upendo wa Mungu unaomfanya kuwa hazina isiyokadirika. Kila kitu kingebadilika ikiwa, kama kwa Bikira, tungeona siri hiyo iliyofichwa juu ya  nyingine, na je ni makosa ngapi na migogoro ambayo tungeepuka.

Ushirika na upatanisho kati ya Mungu

Hata hivyo, akichanganya  na Kilatino  Papa aliendelea kusema kuwa  “neno hilo lingezungumza nasi juu ya ‘mto wa mbwa-mwitu’ na, kwa maana hiyo, juu ya chemchemi ya amani kwa wale wanaoteswa na dhambi zao wenyewe, kwa jeuri, na vita vingi sana ndani na nje ambayo humfanya mtu kuwa mbwa mwitu kwa mtu. Ni mto ule ule uliofichwa wa neema ambao katika mazungumzo na Yesu hutuonesha uhalisia wetu, na kutufungulia kuwa na tumaini”. Bikira tena anahimiza “kuwa chachu ya ushirika na upatanisho kati ya Mungu na wanadamu, akiwatia moyo waamini wengi wanaokaribia patakatifu kwa ajili hiyo”.

Mama wa Guadalupe anajitangaza

Hatimaye, kwa kuchanganya na mzizi wa Mexico, “Mama  Yetu wa Guadalupe anajitangaza kuwa yeye ndiye anayemshinda nyoka, kwa msukumo unaogusa moyo wa Iinjili ya Mwanzo. Kwa hiyo, Asiye na hatia ndiye mama wa kweli wa wale wote wanaoishi; ya wale waliokusanyika leo katika  mahali patakatifu hapo, pamoja na wachungaji wao, ili kutangaza imani yao katika Mwana wa Mungu, ambaye, kwa kufanya vitu vyote kuwa mpya, ameupatanisha ulimwengu naye.” Kwa hiyo  Baba Mtakatifu amewatia kutia moyo ili “kufanya ule mto wa maji ya uzima urukao mbinguni utiririke kutoka katika mioyo ya wanaume na wanawake wa wakati wetu, kumwabudu Mungu katika Roho na Kweli”.

Barua ya Papa kwa maakofu wakuu wa Hispania na Mexico
13 Februari 2023, 17:54