Tafuta

Papa Francisko:Usiridhike na kidogo,Yesu anakualika kupenda bila kipimo

Katika sala ya Malaika wa Bwana Papa ametafakari Injili ya siku kuwa kanuni za kidini ni za manufaa na ni nzuri,lakini “li kuzitimiza ni muhimu kwenda zaidi ya neno.Kuhisi kila huko sawa na kwamba hujaua,hujaiba au kufanya madhara yoyote ni udini wa nje na uliojitenga,ina maana kuridhika na kidogo wakati wito wa Yesu ni kufanya mengi na kupenda bila kipimo kama alivyofanya.

Angella Rwezaula; - Vatican.

Katika Injili ya liturujia ya Siku,Yesu alisema“msifikiri nilikuja kutengua sheria au Manabii; sikuja kutengua, lakini kuitimiza (Mt 5,17). Kutimiza ndiyo ufunguo wa neno ili kujua Yesu na ujumbe wake. Je  nini maana yake? Ili kuelezea Bwana anaanza kusema kile ambacho sio utimilifu. Maandiko yanasema “ usiue, lakini kwa upande wa Yesu hiyo haitoshi ikiwa  unaumiza ndugu kwa maneno; Andiko linasema “ usizini “, lakini hiyo haitoshi ikiwa ni kuishi upendo mchafu wa ndumila kuwili na uongo; Andiko linasema“usiape uongo” lakini hiyo haitoshi iwapo  ni kusheherekea kuapa baadaye unatenda kwa unafiki (Mt 5,21-37). Kwa namna hiyo hakuna utimilifu. Ndivyo Baba Mtakatifu Francisko, ameanza tafakari yake, Dominika tarehe 12 Februari, kwa waamini na mahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican.

Waamini wakisali sala ya Malaika wa Bwana na Papa Francisko
Waamini wakisali sala ya Malaika wa Bwana na Papa Francisko

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na tafakari hiyo amesema : Ili kutoa mfano wa dhati, Yesu anajikita juu ya ibada ya kutoa.  Kwa kutoa sadaka kwa Mungu ilikuwa ni kubadilishana bure zawadi zake: ilikuwa ni ibada muhimu sana, kiasi kwamba ilikuwa imekatazwa kuikatiza kama hapakuwapo na sababu kubwa. Lakini Yesu anathibitisha kuwa lazima kuikatiza ikiwa ndugu ana lolote dhidi yetu, awali ni vema  kujipatanisha na Yeye (23-24); ni kwa njia hiyo tu ibada inatimilika. Ujumbe huko wazi: Mungu anatupenda kwanza, bure, kwa kuanzisha hatua ya kwanza kuja kwetu bila kustahili; na hivyo sisi hatuwezi kusheherekea upendo wake bila kufanya kwa namna hiyo ya kupiga hatua ya kwanza ya kujipatanisha na yule aliye tujeruhi.

Uwana wa Mtakatifu Petro ulijaa waamini ili kusikiliza tafakari ya Papa na kusali sala ya Malaika wa Bwana
Uwana wa Mtakatifu Petro ulijaa waamini ili kusikiliza tafakari ya Papa na kusali sala ya Malaika wa Bwana

Kuna utimilifu gani mbele ya macho ya Mungu, labda mtazamaji wa nje, ambaye kiukweli ni bure. Kwa maneno mengine  Yesu anatufanya kuelewa kuwa sheria za kidini zinahitajika,  na ni nzuri, lakini ziko mwanzoni; kwa ajili ya kutoa utimilifu ni lazima kwenda zaidi ya neno na kuiishi maana yake. Amri ambazo Mungu ametupatia zisifungiwe katika usalama safu, uzingativu rasmi, vinginevyo tunabaki katika udini wa nje na uliojitenga, watumishi wa mungu Bwana, badala ya kuwa  watoto wa Mungu Baba. Baba Mtakatifu Francisko aidha amesema, shida hii haikuwapo wakati wa Yesu tu, ipo hata leo hii. Wakati mwingine kwa mfano inasikika wanasema: “ Padre mimi sijaua, sijaiba, sijafanya vibaya kwa mtu yeyote…” Ni kama kusema kuwa “mimi niko sawa.”

Dominika 12 Februari: waamini katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Dominika 12 Februari: waamini katika uwanja wa Mtakatifu Petro

Ndiyo maana kuna  kuridhika na kiwango cha chini kabisa, wakati Yesu anatualika kufanya mengi iwezekanavyo na kupenda bila kipimo kama alivyofanya. Tukumbuke: Mungu hafikiri kwa kuhesabu; Yeye anatupenda kama mpendwa: sio kidogo, lakini kikubwa! Yeye hasemi “ Ninakupenda mpaka sehemu fulani”. Hapana kwa sababu upendo wa kweli hauishi kamwe hadi sehemu fulani na hahisi kamwe sawa; upendo unakwenda zaidi ya, hawezi kufanya kinyume. Bwana alituonesha kwa kutoa maisha yake juu ya msalaba na kwa kusamehe wauaji wake (Lk 23,34). Na alitukabidhi amri ambayo anazingatia “ kuwa tupendane mmoja na mwingine, kama Yeye alivyo tupenda (Yh 15,12). Huo ni upendo ambao unatimiliza sheria, kwa imani na kwa maisha.

Dominika 12 Februari: Tafakari na sala ya Malaika wa Bwana katika uwanja wa Mtakatifu Petro.
Dominika 12 Februari: Tafakari na sala ya Malaika wa Bwana katika uwanja wa Mtakatifu Petro.

Kwa hiyo tunaweza kujiuliza: ninaishije imani? Je, ni suala la mahesabu, taratibu, au historia  ya upendo na Mungu? Je, ninatosheka kutofanya ubaya wowote, kuweka “uso wa mbele” mahali pake, au ninajaribu kukua katika upendo kwa Mungu na kwa wengine? Na mara kwa mara ninajihakikisha juu ya amri kuu ya Yesu ambaye ananiomba ikiwa ninampenda jirani kama Yeye anavyonipenda?  Kwa sababu wakati mwingine ni rahisi kuhukumu wengine na kusahau kuwa wenye huruma, kama Mungu alivyo kwetu sisi. Mama Maria aliyehifadhi kabisa Neno la Mungu, atusaidie kwenda kutimiza imani yetu na upendo wetu. Papa Francisko amehitimisha.

Tafakari ya Papa kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana 12 02.2023
12 February 2023, 14:42