Papa Francisko ahimizia wajasiliamali wa Mexico kusaidia wenye kuhitaji!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 17 Februari 2023 amekutana na Kikundi cha wajasiliamali wa Mexico, ambapo ameshukuru Askofu Mkuu Eduardo Piza wa Jimbo Kuu la Mji wa Mexico na Msimamizi wa mali za Kikanisa, kwa hotuba yake aliyomwelekeza. Papa kwa hotuba kwa lugha ya kihispania amefurahishwa kukutana nao na amerudia sentesi ya kimexico isemayo: “Nyumba yangu ni nyumba yenu”. Kiukweli kwa wakatoliki wote, hata Vatican ni kama nyumba yao; ni mahali ambapo wana wa Kanisa wanaweza kukutana na kusifu Mungu katika familia. Hata hivyo Baba Mtakatifu amebainisha jinsi ambavyo kwa bahati mbaya, tupo tunafanya uzoefu wa vita ambavyo vinapelekea uharibifu katika familia yote ya kibinadamu, kwa kusababisha mateso na umaskini. Tupo tunapoteza maana ya kuwa familia, ya kuheshimiana na kuvumiliana, hata katika tofauti zetu na shida. Tupo tunasahau kuwa katika famili mambo yanaweza kuwa sawa kwa uvumilivu, kwa upendo, kwa majadiliano. Kwa kushirikishana mitazamo yetu na mahitaji ya kila mmoja, ili kusaidiana mmoja na mwingine.
Utamaduni wa wakati wetu kwa kipindi sasa umeambukizwa na ubinafsi na kujifunga binafsi. Pole pole tuko tunaona matokeo ya dhamiri zetu zilizo lala katika raha, ambazo hupelekea kupoteza mtazamo kwa wale wanaoteseka au wamebaguliwa. Mwezi mmoja uliopita, Papa amekumbuka alivyo wambia kikundi kingine cha wajasiriamali kutoka Hispania, kuwa “Ili mjasiliamali katoliki aweze kuwa ishara ya uwepo wa Mungu katika ulimwengu wa uchumi na wa kazi lazima aweze kutunza mahusiano na Bwana”. Mtaji muhimu tunaoweza kuwa nao ni mtaji wa kiroho. Wakati Bwana anapogusa mioyo yetu, tunapanua mitazamo yetu na tunaweza kuona ni wangapi walio na mahitaji na kutunza uumbaji: tunaweza kutanguliza faida ya wote, na sisi inayofaa kwa familia, na kuweka kando na mantiki ya kidunia za umimi wa mafanikio, utawala na pesa.
Kila mmoja wetu anaitwa kuchangia ili jamii iwe na mafundi zaidi na zaidi wa amani na utamaduni wa kukutana; na ili wajenzi wa jumuiya ambamo wote, bila ubaguzi, wanahisi kuwa wamekaribishwa na kupendwa na Bwana na waweze kuongezeka katika Kanisa. Kuhusu kutunza uhusiano na Mungu, tunajua kwamba ili kufanya hivyo ni lazima kuwe na makuhani wazuri, kwa kuwa wao ni wachungaji wa watu wa Mungu. Papa amefurahi kuona kwamba wanalipenda Kanisa na wanajali kuhusu makuhani. Ni haki ya waamini kuwa na mapadre wenye umbo zuri, wanaolisha jumuiya ya waamini kwa furaha ya mkate wa Neno na Ekaristi; na ambayo pia hushuhudia maisha ya kujitolea kwa wengine.
Kwa hiyo Papa amewatia moyo na kuwaombea, ili wakimshukuru Mungu kwa ajili ya karama ambazo kwazo wanatajirisha familia nzima ya kikanisa, na kuwaombea katika mapambano na juhudi zao za kila siku. Vile vile amewaalika wakae nao karibu na kuwasaidia ili waweze kuelekeza nguvu na ubunifu wao katika zoezi la kichungaji. Papa Francisko amependa kuhitimisha kwa kuwakabidhi katika ulinzi wa Mama Yetu wa Guadalupe. Amesema kwamba yeye aliomba ajengewe nyumba ambapo watoto wake wote wangeweza kumtembelea ili kuweka huzuni na matumaini yao. Kwa hiyo Kanisa Kuu la Guadalupe ni taswira ya Kanisa, linalowakaribisha watoto wake wote. Morenita del Tepeyac awatunze wao, familia zao na awatie moyo na kuwasindikiza katika miradi yao mizuri. Papa amemaliza akiwabariki huku akiwaomba wasali kwa ajili yake.