Papa atoa msaada kwa watu wa Uturuki na Siria
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Mbele ya kukabiliwa na janga lililosababishwa na tetemeko la ardhi lililoikumba Siria na Uturuki mnamo tarehe 6 Februari 2023, na kwa bahati mbaya idadi ya vifo vinazidi kuoengezeka na kufikia zaidi ya 41,000, Baba Mtakatifu aliomba wakati wa sala ya Malaika wa Malaika Dominika tarehe 12 Februari ukaribu wao lakini pia hata kwa msaada wa dhati ili kupunguza uzito na maumivu ya watu hao wanaendelea kuteseka kutokana na tetemeko la ardhi. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko kupitia Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo, ametoa msaada.
Msaada ambao uliotoka kwa Papa mwenyewe kupitia Sadaka ya Kitume, Jumatano tarehe 15 Februari 2023, katika bandari ya Napoli, kwa njia ya Meli ya MSCAurelia umetumwa na ambao utawasili huko Iskenderum nchini Uturuki baada ya siku mbili. Ndani ya meli pamoja na misaada mingine kutoka serikali ya Italia na mashirika mengine yasiyo ya kiserikali, pia kuna masweta 10,000 ya kujinga na baridi ambayo Kadinali Konrad Krajewski, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo alipeleka yeye mwenyewe katika mji mkuu wa Campania nchini Italia tarehe 14 Februari. Nguo hizo zimetumwa kwa kambi ya wakimbizi ya Kilis nchini Uturuki, kilomita 50 kutoka Gaziantep na kilomita 60 kutoka mji wa Aleppo nchini Siria.
Kutoka hapo usambazaji huo utakabidhiwa kwa waendeshaji wa Wahudumu wa Mfuko wa Rava ambao wamekuwepo kwa muda mrefu katika eneo hilo, ambayo wanaohusika na kutoa chakula na makazi kwa maelfu ya watu ambao wameachwa bila makazi. Katika miaka ya hivi karibuni, kufuatia kuzuka kwa vita nchini Sria, kambi hiyo imepanuka zaidi na kuwahifadhi takriban wakimbizi 60,000, lakini wengine wengi wanaishi katika kambi za muda. Tetemeko la ardhi, kama walivyoeleza, limezidisha hali na mamia ya watu wanajiunga na familia za wakimbizi waliokuwa tayari wapo.
Kuhusu nchini Siria, Kardinali Konrad Krajewski ameripoti, kwamba Papa ametuma, pia kupitia Baraza hilo, msaada wa kifedha kwa Balozi wa Vatican aliyepo kwenye nchi hizo ambazo zitaitumika katika eneo hilo, kusaidia watu ambao tayari wamedhoofika kwa miaka mingi ya vita na sasa kutokana na tetemeko kubwa la ardhi.