Kilio cha Papa dhidi ya ukoloni mpya
Na Angella Rwezaula, - Vatican
Nchi kubwa na iliyojaa maisha, pafu la pili la sayari baada ya Amazon shukrani kwa upanuzi wa msitu wake wa kitropiki, ambao umeporwa kwa pupa. Nchi yenye maliasili nyingi, iliyokumbwa na vurugu kama ngumi ya tumbo, ambayo inaonekana kukosa pumzi kwa muda. Haya ni kati ya maneno mazito katika hotuba yake, mara baada ya kulakiwa na maelfu ya watu wa rika zote waliofurika barabarani kutoka uwanja wa ndege wa Ndolo hadi katikati mwa jiji kuu la Kinshasa, ambapo Baba Mtakatifu alizindua ujumbe wake wa kwanza katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kwa Afrika yote.
Katika bustani ya Ikulu ya Taifa, akiwa ameketi karibu na Rais Felix Tshisekedi Tshilombo, Mrithi wa Petro alizungumza maneno ya kuunga mkono Wakongo wote ambao wanapinga majaribio ya kugawanya nchi iliyovuka kikomo kwa ghasia na kwa mara nyingine tena akakumbuka kitu cha unyonyaji huko Congo na zaidi kwa ujumla kwa bara zima la Afrika. “Baada ya ule wa kisiasa, ukoloni wa kiuchumi umeibuka ambao ni utumwa zaidi”, alisema Papa Francisko.
Ni ukoloni wa hila zaidi na usio na kelele zaidi, unaowaondoa watu wa Kiafrika uhuru na kujitawala. Kwa hiyo, Papa aliongeza, kusema kwamba huko Congo “umefikia kama kitendawili cha matunda ya ardhi yake kufanywa nchi kuwa ya kigeni kwa wakazi wake. Kwa sababu sumu ya pupa imefanya damu yake kuwa almasi. Ni janga ambalo mbele yake ulimwengu ulioendelea zaidi kiuchumi mara nyingi hufunga macho, masikio na midomo yao”.
Papa Fransisko kwa hiyo alitaka kufika hapo ili kuwakumbatia watu hao waliojaribiwa na migogoro na umaskini ili kuhakikisha kwamba macho, masikio na midomo ya wote inafunguka na kukumbusha juu ya migogoro iliyosahaulika ambayo inaunda vipande vingi vya Vita vya tatu vya Kidunia na matokeo yake ya mfumo wa kiuchumi na kifedha ambao unaua kwa sababu hauweki mtu katikati, bali ni mungu pesa. “Nchi hii na bara hili, alisema Papa katika hotuba yake ya kwanza huko Kinshasa kwamba wanastahili kuheshimiwa na kusikilizwa, wanastahili nafasi na tahadhari: toeni mikono yenu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, iondoeni katika bara la Afrika! Acha kuisumbua Afrika: sio mgodi wa kunyonywa au udongo wa kuporwa", alisisitiza.