Kard.Krajewski:msada mpya wa Papa kwa wahanga wa tetemeko Uturu
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Jitihada ya pamoja na ya haraka katika ushara ya msaada na wa mshikamano kwa watu ambao wanateseka. Kardinali Konrad Krajewski, Mwenyekiti wa Huduma ya Upendo wa Kipapa amesimulia hivyo kwa kile ambacho kwa siku moja kimetokea jijini Vatican, kufuatia na mwaliko wa Papa kuhusu uchungu na ushirikishano kwa wale ambao wameptata janga huko nchini Uturuki na Siria. Katika nchi ya mwezi mpevu (kama iitwavyo Uturuki), idadi ya watu waliokufa kutokana na tetemeko la ardhi, lililopiga eneo hilo mnamo tarehe 6 Februari, imeongezeka hadi zaidi ya watu 39,600 waliokufa, hata kama kuna miujiza midogo midogo kama vile ya kugunduliwa kwa watu ambao bado wakiwa hai chini ya vifusi.
Tarehe 16 Februari 2023, Papa Francisko alikutana mjini Vatican na Balozi mpya wa Uturuki Bwana Ufuk Ulutaş, aliyepokelewa kwa ajili ya kuwasilisha barua na hati za utambulisho mjini Vatican. Katika hafla hiyo, baada ya kuzungumzia wazo la ukaribu na upendo kwa watu wa Uturuki, Baba Mtakatifu aliuliza mahitaji ya dharura ni yapi kwa idadi ya watu na akapendekeza kwa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo kutoa mahitaji yoyote. Saa moja baada ya mkutano na Baba Mtakatifu kwa mujibu wa Kardinali Konrad Krajewski alikutana na balozi huyo ambaye alinielezea kile walichohitaji zaidi.
Zawadi ya Papa kuelekezwa Uturuki
Orodha ya mwanadiplomasia huyo ilihusu hasa vyakula vya makopo kama vile wali na tuna, lakini pia nepi na nyenzo nyinginezo zinazoweza kustahimili hali ya hewa kwa sasa ambayo ni baridi. Mara moja, alisisitiza Kardinali Krajeski kila mtu mjini Vatican alijishughulisha na kuandaa vifushi 10 za vya vyakula, ambavyo vilipakiwa kwenye Lori na kuelekea uwanja wa ndege wa Fiumicino. Zawadi ya Papa iliekezwa kwenye ghala za Kituruki, wafanyakazi wa kujitolea na wafanyakazi wa uwanja wa ndege walifanya kazi bila kuchoka ili kupanga mizigo ambayo iweze kuwasili Istanbul. Kumekuwa na uangalifu mkubwa katika kuandaa vifurushi ambavyo vilisafirishwa kwa ndege na sio ndege za mizigo, kwa hivyo umakini mkubwa ulilipwa kwa uzito na urefu wa vifurushi vyenyewe.
Upendo bila upendo haupo
Kardinali Krajewski alisema: “Katika Injili siku zote inasemwa leo, si kesho. Yesu alipofanya miujiza, aliifanya mara moja, hakusema subiri juma moja au wakati fulani na hivyo tulifanya hivyo mara moja kwa shukrani kwa maegesho ya gari ya Vatican, michango, na wengi walisaidia. Katika masaa 24 kila kitu kilifanyika, na hivyo anao uhakika kuwa “upendo bila upendo haupo”. Na wakati huohuo, Mwenyekiti wa Baraza la kipapa la Makanisa ya Mashariki, Mosninyo Claudio Gugerotti, alianza utume wake wa kutembelea miongoni mwa wahanga wa tetemeko la ardhi nchini Siria, ambapo tetemeko hilo lilisababisha vifo vya zaidi ya watu 5,800. Safari ambayo pia itampeleka Uturuki kuelezea ukaribu wa Papa kwa watu walioathiriwa na tetemeko la ardhi.