WYD,Papa:kwa kukaribisha vijana mtafunguliwa upeo wa ulimwengu
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 25 Januari 2023, kwa mara nyingine tena amependa kuwatumia ujumbe kwa njia ya video, kwa watu wa kujitolea na wanafamilia ambao watakaribisha vijana wakati wa Siku za Vijana duniani(WYD) mwaka huu mwezi Agosti. Baba Mtakatifu amesema: “kwa maneno mengine, familia zenu zitapanuka, zitakuwa kubwa zaidi. Mtawapokea wageni vijana kama watoto wenu, kama jamaa zenu vijana. Mtawakaribisha nyumbani kwenu na hii itabadilisha maisha yenu kidogo. Kwa maneno rahisi itawaletea usumbufu. Lakini mtafanya hivyo kwa ukarimu, sio tu kuduhumia, ambalo ni jambo kubwa, lakini pia kwa kujifungulia kwa vijana wengine, kwa tamaduni nyingine, kwa njia nyingine za kutazamaa maisha. Baba Matakatifu amesema: “Vijana hawa kwa hakika watawaletea shida, kwa maana ya usumbufu na kazi, nyumbani kwenu, lakini wao wataacha mbegu ya utamaduni mwingine, mbegu ya mtazamo mwingine na watawaunganisha kila mmoja wenu, hakika nyingi ambazo mlikuwa mnafikiri kuwa nazo na kuwafanya kuona katika maeneo mengine kuwa mambo yanaweza kuwa tofauti. Watawafanya kuwa wa ulimwengu”.
Vijana wengi wa kigeni wanathibitisha uzoefu mzuri kukaribishwa na familia
Baba Mtakatifu amesema kwamba watawakaribisha vijana kutoka duniani kote, na inaonekana kuwa si kitu, kwa sababu kila familia itakaribisha kijana mmoja au wawili, na bado itakuwa ni ulimwengu ndani yao, pamoja na uzoefu wao. Kwa maana hiyo vijana wa kigeni wanasema kwamba uzoefu wa kukaribishwa ndani ya familia ni wenye utajiri zaidi. Wanasema hivyo”. Na kwa hiyo wao wawe na uhakika kwamba mtu anaweza kuwa Mkristo kwa njia tofauti na utamaduni mwingine, na mtazamo mwingine.
Kufungulia upeo wa ulimwengu
Hii ina maana ya kuwa wa ulimwengu, kwa kufungua upeo. Papa ameshukuru kwa kile wanachofanya. Kiukweli, itakuwa ngumu kwao, kwani itahusisha juhudi, lakini itakuwa ni kama kupanda mbegu katika ulimwengu, kwa kutazama upeo ambao uko nje ya mipaka yetu ndogo na vizingiti, viwe vya kijiografia, kiutamaduni au kiroho. Papa ameshukuru kwa ukarimu wao wa kuwakaribisha vijana. Mungu awabariki na Mama yetu awalinde. Amehitimisha kwa kuomba wasali kwa ajili yake.
Ikumbukwe kwamba ni hivi karibuni Papa Francisko tayari alikuwa amewatumia ujumbe mwingine kwa kuwashukuru wale ambao wamejiandikisha 400,000 na kuwaalika wengine waendelee kujiandikisha ili kushiriki Siku ya vijana duniani itakayo fanyika huko Lisbon nchini Ureno kuanzia tarehe Mosi hadi 6 Agosti 2023. Kwa maana hiyo anatumia fursa hii kuwashukuru sana familia ambao wataweza kuwakaribisha vijana katika nyumba zao. Ndio anajua jinsi ambavyo inawezekana kuleta usumbufu lakini ni nzuri, itawaboresha wakati ambao utaratibu na mipaka ya mambo ya kawaida itaruka na upeo wa ulimwengu utafunguliwa kwa siku zijazo.