Tafuta

2023.01.16 Papa ametuma salamu za rambi rambi kwa waathirika wa shambulio huko Kasindi nchini (DRC) lililotokea 15 Januari 2023. 2023.01.16 Papa ametuma salamu za rambi rambi kwa waathirika wa shambulio huko Kasindi nchini (DRC) lililotokea 15 Januari 2023. 

Ukaribu wa Papa kwa waathirika wa shambulio la Kanisa la kipentekoste DRC

Papa Francisko,katika telegramu iliyotiwa saini na Kardinali Parolin,anaonesha maskitiko na huruma yake kwa wale walioathiriwa na shambulio la Kanisa la Kipentekoste la Kasindi nchini (DRC)mnamo Dominika tarehe 15 Januari 2023.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Huruma na ukaribu wake kwa watu walioshambulio mnamo Dominika tarehe 15 Januari 2023, ambalo linadaiwa kuwa ni la IS, dhidi ya Kanisa la Kipentekoste la Kasindi, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) umeoneshwa na Baba Mtakatifu Francisko, ambapo shambulio hilo “limesasababisha vifo vya watu wasio na hatia” kama inavyoelezwa katika telegramu iliyotiwa saini na Karidnli Pietro Parolin, Katibu wa Vatican zilizo elekezwa kwa mchungaji André Bokundoa-bo-Likabe, na Mwenyekiti wa Kanisa la Kristo katika nchi hiyo ya Afrika. Katika ujumbe huo unasomeka kwamba: "Baba Mtakatifu Francisko anawakabidhi marehemu na waliojeruhiwa kwa rehema ya Mungu". Aidha "anamwomba sana Bwana wa uzima ili wanaoteseka wapate faraja na tumaini kwa Mungu, huku akiwaombea zawadi ya amani."

Tawi la ISIS katika Afrika ya Kati, ISCAP, lilidai kuhusika na mlipuko huo tarehe 15 Januari 2023 katika kanisa la Kipentekoste katika jimbo la Kivu Kaskazini na kusababisha vifo vya watu 17 na wengine zaidi ya arobaini kujeruhiwa. Wanajihadi hao walisema walitega na kulipua bomu hilo na kutishia mashambulizi zaidi. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ndiyo nchi itakayotembelewa na Papa Francisko mnamo tarehe 31  Januari katika ziara yake ya kitume ambayo pia itamfikisha  huko Sudan Kusini.

Balozi wa Vatican anachambua mazingira hayo

Kuhusiana na shambulio hilo Vatican ilifanya mahojiano na Balozi wa Vatican nchini humo kwamba wakati wanamsumbiri Papa kufika katika maeneo yaliyojaa makovu ya majeraha, ni wasi wasi wake mkubwa kuona tena ukatili  unaendelea hata katika Kanisa la kipentekoste.  Na alielezea jinsi ambavyo sababu kuu ya vita vya msituni huko mashariki ni utajiri wa ardhi ya chini ambayo malengo ya wengi yamejikita mizizi. Kanisa linafanya kazi kubwa na wao ndio chachu ya misaada. Katika muktadha huo, juhudi kubwa zaidi zinafanywa ili kuhakikisha usalama unaohitajika wakati wa  ziara ya Papa Francisko ambaye pia atakutana na waathirika wa ukatili huo.Kwa maana hiyo waamini watu wa Mungu milioni mbili wanatarajiwa kuhudhuria Misa mjini Kinshasa.

Askofu Mkuu Ettore Balestrero, Balozi wa Vatican nchini humo kwa maana hiyo alichambua mazingira ya kijamii na kisiasa ya eneo hilo na kutathmini maandalizi ya ziara ya upapa. “Ishara ya wasiwasi, hata zaidi kwa sababu inathibitisha mabadiliko ya hali ya ardhi. Kwa hakika kwa sababu hiyo mkutano wa Papa, atakapokuja, na waathirika wa Mashariki itakuwa muhimu sana. Ni lazima pia kusema kwamba kiukweli kulikuwa na mashambulizi mawili: moja kwenye mpaka na Uganda katika hekalu la Kipentekoste: picha walizonitumia zinaelezea kuzimu halisi. Miili iliyoharibiwa ya watu wazima na watoto, jengo lililoharibiwa nusu. Lakini siku hiyo hiyo kulikuwa na shambulio jingine huko Beni, katika soko kuu ambalo liko katika moja ya maeneo salama zaidi ya jiji. Tena, wengine wanaamini kuwa AdF (Allience Democratic Forces) wanawajibika kama onesho la nguvu na ugaidi. Wapo wanaoamini kuwa badala yake kumekuwa na ushirikiano na usalama wa eneo hilo, lakini dhana moja haiondoi nyingine. Kwa vyovyote vile, ningesema kwamba amani Mashariki ingali bado mbali. Tuko katika jimbo la Kivu Kaskazini, ambalo limezingirwa kwa zaidi ya mwaka mmoja, tukionesha jinsi hali si tu kwamba haijaimarika bali imekuwa mbaya Zaidi”

Akiendelea Balozi wa Vatican alisema: “Ujumbe unaotia wasiwasi sana ni kwamba AdF kwa bahati mbaya wanazidi kuimarika na inaonekana kwangu kuwa wao pia ndio wanufaika wakuu wa mzozo unaoendelea kusini zaidi, karibu na Goma, na M23. Shambulio la jana pia linaonesha kuwa wamepata ushawishi mkubwa huko Butembo, jiji kubwa karibu na Kasindi. Ukweli kwamba imekuwa ikidaiwa na Isis pia inaonesha kwamba uhusiano kati ya ADF na Isis unaunganishwa, kwa bahati mbaya mbinu za mashambulizi zinazozidi kuwa sawa na hii inaweza tu kuwa na wasiwasi kwa usalama wa kikanda na juu ya yote kwa ile ya wakazi ambao ndio wahanga wa mara kwa mara wa mauaji dhidi yao”.

Telegramu ya Papa kwa mchungaji wa Kipentekoste huko DRC
17 January 2023, 16:15