Tafuta

2023.01.29 Wakati Tafakari na sala ya malaika wa bwana, Papa amekumbusha matukio ya ghasia za kidunia na kutoa wito 2023.01.29 Wakati Tafakari na sala ya malaika wa bwana, Papa amekumbusha matukio ya ghasia za kidunia na kutoa wito  (Vatican Media)

Papa kwa:ACI,Israeli,Palestina,Caucasus&Siku ya Ukoma duniani

Kwa mara nyingine tena,Dominika 29 Januari 2023,Jimbo la Roma limeandaa tukio la “Carovana della pace” yaani “Msafara wa amani” kupitia mitaa ya katikati ya jiji la Roma,baadaye walishiriki sala ya Malaika wa Bwana na Papa.Papa ametoa wito kwa ajili ya Ukraine,Israeli na Palestina,Caucasus na kukumbuka Siku ya Kimataifa ya Ukoma.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Dominika tarehe  29 Januari 2023  vijana wa chama katoliki cha matendo katika jimbo la Roma, pamoja na waelimishaji na wazazi wao na wenzao kutoka shule na parokia za jiji kwa mara nyingine tena wamefanya tukio la Carovana dela Pace yaani “Msafara wa amani” ambao ni maandamano ya sherehe na rangi ya alama ya amani ambao wamepitia barabara za katikati ya mji mkuu, wakiwa na kauli moja isemayo:“Kufanya mazoezi kwa ajili ya amani. Siku  hiyo imewakilisha wakati muhimu sana wa safari ambayo imefanyika kila mwaka kupitia vikundi vyote vya parokia jimbo la Jiji la Roma. Watoto hawa ni kuanzia umri wa miaka 3 hadi 14 wa chama  Wakatoli ambao kila mwaka wamekuwa wakialikana ili kushuhudia kwa pamoja matumaini ya amani katika mitaa ya Roma.  Kwa maana hiyo ni zaidi ya miaka 40 kwa mujibu wa maelezo ya kutoka kwa mmoja wa waandaaji katika jimbi Bi Marilena Pintagro. Kwake yeye amesema kwamba katika Mwezi wa Amani, vijana wamejitoa wenyewe kuwa mashuhuda dhidi ya aina zote za unyanyasaji na ukandamizaji, kuaniza na  ugomvi kati ya watu binafsi hadi migogoro kati ya mataifa, na ambapo kiukweli ni kupaza sauti kuu katika  mji ile shauku yao ya amani, shauku ambayo imekuwa ya haraka na ya sasa katika mwaka uliopita. Ushiriki  kwa maana hiyo ulikuwa karibu ni watu 3,000 ambao walikusanyuka kuanzia saa 4.00 katika bustani ya Nyumba ya kifalme ya  Mtakatifu Angelo(Castel Sant’Angelo).

Chama cha matendo ya vijana Katoliki katika Uwanja wa Mtakatifu Petro
Chama cha matendo ya vijana Katoliki katika Uwanja wa Mtakatifu Petro

Baada ya dakika za kwanza, washiriki hao walihamia katika Uwanja wa Mtakatifu Pietro mjini Vatican kwa sherehe na msafara wa kupendeza sana , wakipitia katika Njia ndefu ya Conciliazione katikati yake wakiwa na michezo na seti zinazokumbuka mpangilio wa michezo ya wana timu mbali mbali. Baada ya kufikia sekta iliyotengwa katika Viwanja vya Mtakatifu Petro, waliendelea  na uhuishaji kutoka jukwaani, pia salamu za rais wa Chama hicho kijimbo Bwana Marco Di Tommasi, viongozi wa kitaifa wa chama na sala ilioongozwa na Kardinali Angelo De Donatis. Baada ya hapo walishiriki Sala ya Malaika iliyoongozwa na Papa Francisko. Papa alisema: " Na sasa kwa upendo mkuu ninawasalimu wavulana na wasichana wa Chama cha Matendo  Kikatoliki Jimbo la Roma! Mmekuja katika “Msafara wa Amani” Ninawakushukuru kwa mpango huu, wa thamani zaidi mwaka huu kwa sababu, ya kufikiria juu ya Ukraine iliyouawa, kujitolea kwetu na sala zetu za amani lazima ziwe na nguvu zaidi. Hebu tufikirie Ukraine na tuwaombee watu wa Kiukreni, ambao wanateswa vibaya sana”.

Papa akiwa na watoto wawili waliowakilisha umati wao kumkabidhi Papa majitoleo yao
Papa akiwa na watoto wawili waliowakilisha umati wao kumkabidhi Papa majitoleo yao

Hata hivyo katika maelezo kuhusu Msafara wa amani, zaidi ya hayo vijana hao kwa hakika katika maelezo yao waliyosmoa  waliwezeshwa kujitambua kama wamisionari, wakichukua kwa moyo wa dhati kushikamana na mipango  miwili ya mshikamano katika  shughuli zao za parokia. Mpango wa kwanza uliopendekezwa na Chama cha Kikatoliki cha vijana Italia ambacho kwa njia ya uuzaji wa mipira iliyotengenezwa kwa nyenzo za kiikolojia, kitakwenda kusaidia mradi wa CSI kwa ulimwengu unaohamasishwa na Kituo cha Michezo cha Italia; mpango wa pili ni katika eneo la Roma ambapo kila Parokia inaalikwa kukusanya  michango itakayotolewa kwa ajili ya shughuli za Caritas  Jimbo ili  kuunga mkono wa hali halisi inayofanya kazi na watoto na vijana walio katika matatizo. Kwa maana hiyo kila parokia pia inaalikwa  kuchangia mpira ambao utatolewa kiukweli, kama ishara madhubuti ya uzuri wa kazi ya pamoja ya kikundi. Vile vile Papa alitoa salamu kwa wote  waliotoka Italia na nchi nyingine. Aliwasalimia kikundi cha quinceañera kutoka Panama na wanafunzi kutoka Badajoz nchini Hispania. Aliwasalimu mahujaji kutoka Moiano na Monteleone ya Orvieto, wengine kutoka  Acqui Terme na vijana wa Agesci  huko Cercola Primo.

Uchungu kwa waliouawa huko Nchi Takatifu na wito kwa serikali mbili

Kwa uchungu mkubwa Papa ameelzea alivyo pokea habari zinazotoka katika Nchi Takatifu, hususan za kifo cha Wapalestina kumi, akiwemo mwanamke, aliyeuawa wakati wa harakati za kijeshi za Israeli dhidi ya ugaidi huko Palestina; na yale yaliyotokea karibu na Yerusalemu, siku ya Ijumaa jioni 27 Januari, wakati Wayahudi saba wa Kiisraeli waliuawa na Mpalestina na watatu walijeruhiwa walipokuwa wakitoka kwenye sinagogi. Papa amenainisha kwamba mzunguko wa kifo unaoongezeka siku baada ya siku ambao haufanyiwi chochote ili kuziba miale michache ya uaminifu iliyopo kati ya watu hao wawili. Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, makumi ya Wapalestina wameuawa katika mapigano ya kisilaha na jeshi la Israeli.  Kwa maana hiyo “Ninatoa wito kwa Serikali mbili na jumuiya ya kimataifa kutafuta, mara moja na bila kuchelewa, njia nyingine zinazojumuisha mazungumzo na utafutaji wa dhati wa amani. Tuombee haya ndugu”.

Wito wa Papa kwa ajili ya Ukanda wa Lachin huko Caucasus

Papa Francisko vile vile ametoa wito wake   kwa sababu ya hali mbaya ya kibinadamu katika Ukanda wa Lachin, Kusini mwa Caucasus. “Niko karibu na wale wote ambao, katikati ya majira ya baridi, wanalazimika kukabiliana na hali hizi zisizo za kibinadamu. Kila juhudi lazima zifanywe kimataifa kutafuta suluhishi za amani kwa manufaa ya watu.”

Wito wa Papa kwa Siku ya Kimataifa ya Wakoma

Papa Francisko akiendelea amekumbuka Siku ya LVXX ya Ukoma Duniani.  Kwa hiyo amesema kwamba: “Kwa bahati mbaya, unyanyapaa unaohusishwa na ugonjwa huu unaendelea kusababisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu katika sehemu mbalimbali za dunia”. Kwa hiyo amebainisha jinsi anavyoonesha ukaribu wake kwa wale majeruhi na kuhimiza  kujitolea kwa ushirikiano kamili kwa ajili ya hawa kaka na dada zetu.

Papa Francisko baada ya Sala
29 January 2023, 14:09