Tafuta

2023.01.04 kifuniko cha kitabu (Lev) "Mungu daima ni mpya"kinakusanya mawazo ya kiroho ya Papa Benedikito XVI. 2023.01.04 kifuniko cha kitabu (Lev) "Mungu daima ni mpya"kinakusanya mawazo ya kiroho ya Papa Benedikito XVI. 

Papa:Taalimungu ya Benedikto XVI,shauku na utajiri unaounganishwa na Injili

Papa Francisko ametia saini katika utangulizi wa kitabu chenye kichwa:“Mungu daima ni mpya”, ambacho kinakusanya mawazo ya kiroho ya Papa Mstaafu Benedikto XVI:"Papa anaandika kuwa:Hoja yake ya imani ilikamilishwa kwa kujitolea kwa mtu ambaye amejitolea mwenyewe kwa Mungu na chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu,alitafuta ufahamu zaidi wa fumbo la Yesu."

PAPA FRANCESCO

Ninafurahi kwamba msomaji katika mikononi mwake anaweza kuwa na maandishi haya ya mawazo ya kiroho ya hayati Baba Mtakatifu Benedikto XVI. Kichwa tayari kinaeleza mojawapo ya vipengele vya sifa zaidi vya mafundisho na maono ya imani ya mtangulizi wangu: ndiyo, Mungu daima ni mpya kwa sababu Yeye ndiye chanzo na sababu ya uzuri, neema na ukweli. Mungu hajirudii kamwe, Mungu hutushangaa, Mungu huleta mambo mapya. Upya wa kiroho unaojitokeza kutoka katika kurasa hizi ambazo zinathibitisha hilo kwa kina. Benedikto XVI alifanya taalimungu kwa magoti yake. Hoja yake ya imani ilikamilishwa kwa kujitolea kwa mtu ambaye amejitolea mwenyewe kwa Mungu na ambaye, chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, alitafuta ufahamu mkubwa zaidi wa fumbo la Yesu ambaye alikuwa amemvutia tangu alipokuwa mdogo.

Mkusanyo wa mawazo ya kiroho ambao umewasilishwa katika kurasa hizi unaonesha uwezo wa kiubunifu wa Benedikto XVI katika kujua jinsi ya kuchunguza nyanja mbalimbali za Ukristo kwa kuzaa matunda ya taswira, lugha na mitazamo ambayo inakuwa kichocheo endelevu cha kukuza karama ya thamani ya kumkaribisha Mungu katika maisha binafsi. Njia ambayo Benedikto wa kumi na sita aliweza kuunda moyo na hoja, mawazo na mapenzi, busara na hisia kuingiliana ni kielelezo cha matunda cha jinsi ya kuweza kumwambia kila mtu kuhusu nguvu kubwa  ya kulipuka ya Injili.

Msomaji ataona imethibitishwa katika kurasa hizi, ambazo zinawakilisha pia shukrani zetu kwa utaalamu,  Mhariri, ambaye shukran za dhati kwa ajili ya aina ya asili ya kiroho ya maandishi ya Benedikto XVI: hapa yanaangaza uwezo wake wa kuonesha daima upya wa kina cha imani ya Kikristo. Inatosha tu kidogo Florilegium. “Mungu ni tukio la upendo, usemi ambao peke yake hufanya haki kamili kwa taalimungu ambayo daima inapatana kati ya sababu na upendo. “Ni nini kinachoweza kutuokoa ikiwa sio upendo? aliwauliza vijana katika mkesha wa maombi huko Cologne mnamo mwaka 2005, tafakari kama hiyo ilikumbukwa, wakati akiuliza swali linalofanana na Fyodor Dostoevsky. Na anapozungumza juu ya Kanisa, shauku ya kikanisa humfanya aseme maneno ambayo yamejazwa sana na mapenzi: “Sisi sio kituo cha uzalishaji, sisi sio kampuni ya kutengeneza faida, sisi ni Kanisa”.

Undani wa mawazo ya Joseph Ratzinger, ambayo yanasimikwa juu ya Maandiko Matakatifu na Mababa wa Kanisa, yangali bado ni  msaada kwetu leo hii. Kurasa hizi zinashughulikia mada mbalimbali za kiroho na ni kichocheo cha kubaki wazi kwa upeo wa umilele ambao Ukristo unao katika Vinasaba vyake (DNA). Hilo ndilo litabaki daima la Papa Benedikto XVI , wazo lake kuwa lenye kuzaa matunda na uadilifu baada ya muda, kwa sababu aliweza kuzingatia marejeo msingi ya maisha yetu ya Kikristo: kwanza kabisa, nafsi na neno la Yesu Kristo, zaidi ya hayo fadhila za kitaalimungu, au upendo, tumaini na imani. Na kwa hili Kanisa lote litamshukuru, daima.

Kwake  Benedikto XVI, ibada isiyo na kikomo na mafundisho yenye nuru vimeunganuishwa kwa dhati katika muungano wenye usawa. Ni mara ngapi alizungumza uzuri kwa  maneno ya kugusa. Benedikto daima amezingatia uzuri kama njia ya upendeleo ya kuwafungua wanaume na wanawake kwa wapitao maumbile na hivyo kuweza kukutana na Mungu, ambayo kwake ilikuwa kazi kuu na utume wa haraka sana wa Kanisa. Hasa, muziki ulikuwa kwake sanaa ya karibu ambayo angeweza kuinua roho na mambo ya ndani. Lakini hii haikumfanya aende , mbali akiwa mtu wa kweli wa imani, kwa maswali makuu na miiba ya wakati wetu, yaliyochunguzwa na kuchambuliwa kwa uamuzi wa kufahamu na roho ya ushujaa ya kuchambua. Kutokana na kusikiliza Maandiko Matakatifu, yaliyosomwa katika mapokeo ya Kanisa yaliyo hai daima, aliweza kutoka katika umri mdogo kutumia hekima hiyo muhimu na ya lazima kuanzisha mazungumzo na utamaduni wa wakati wake, kama kurasa hizi zinavyothibitisha.

Tunamshukuru Mungu kwa kutupatia Baba Mtakatifu Benedikto XVI: kwa neno lake na ushuhuda wake ametufundisha kwamba kwa tafakari, fikra, utafiti, kusikiliza, mazungumzo na zaidi ya yote sala inawezekana kulitumikia Kanisa na kutenda mema kwa wanadamu wote; alitupatia zana changamfu za kiakili ili kuruhusu kila mwamini kutoa sababu ya tumaini lake kwa kutumia njia ya kufikiri na kuwasiliana ambayo inaweza kueleweka na watu wa wakati wake. Nia yake ilikuwa ya kudumu: kuingia katika mazungumzo na kila mtu katika kutafuta pamoja njia za kukutana na Mungu. Utaftaji huu wa mazungumzo na tamaduni za wakati wake umekuwa shauku  ya moto ya Joseph Ratzinger: yeye, kwanza kama mtaalimungu na kisha kama mchungaji, hajawahi kujifungia mwenyewe katika utamaduni wa kiakili tu,uliotengwa na historia ya wanadamu na ulimwengu.

Kwa mfano wake wa kiakili uliojaa upendo na shauku (ambayo maana yake ni kuwa ndani ya Mungu) alituonesha uwezekano kwamba kuutafuta ukweli kunawezekana, na kwamba kujiachilia kutawaliwa nao ndiko juu zaidi roho ya mwanadamu inaweza kufikia. Katika safari hii vipimo vyote vya mwanadamu, sababu na imani, akili na hali ya kiroho, vina jukumu lake na umaalumu wao wenyewe. Utimilifu wa uwepo wetu, alikumbusha kwa maneno na mfano wa Benedikto XVI kwa neno na mfano, kuwa  unapatikana tu katika kukutana kibinafsi na Yesu Kristo, Aliye Hai, Logos aliyefanyika mwili, akajifunua kamili na wa uhakika wa Mungu, anayedhihirishwa ndani yake. Hadi mwisho. Haya ndiyo matashi yangu kwa msomaji: na ili apate katika kurasa hizi zilizopitiwa na sauti ya shauku na upole ya mwalimu wa imani na matumaini neema ya kukutana kwa upya na Yesu na uzima.

Papa Francisko na utangulizi wa kitabu kuhusu Papa Benedikto XVI
04 January 2023, 16:49