Papa,Malaika wa Bwana:tambua hatima ya maisha na vishawishi vya safari!

Kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana,Papa ametoa tafakari yake katika siku kuu ya Tokeo la Bwana 6 Januari:Wataalamu na wenye hekima walishangazwa zaidi na kile ambacho walikuwa hawajuhi na kile wanajua. Walihisi kuitwa kwenda zaidi.Ni muhimu hasa sisi kutotosheka,kutafuta Bwana,kuondokana na starehe zetu,kutembea kuelekea Yeye na wengine na kujikita ndani ya uhalisia.

Na Angella Rwezaula; -Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko kabla ya sala ya Malaika wa Bwana ametoa tafakari yake akiwageukia waamini na wanahija kutoka sehemu mbali mbali  za dunia waliounganika kwa wingi sana katika Kiwanja cha Mtakatifu Petro mjini Vatican  Ijumaa tarehe 6 Januari 2023, ambapo Mama Kanisa anaadhimisha Siku Kuu ya Epifania yaani Tokeo la Bwan. Papa amesema  Leo ni siku kuu ya Epifania, Injili inazungumza juu ya Mamajusi ambao walifika Bethlehemu , wakafunga zawadi zao na kumpatia Yesu dhahabu, uvumba na manemane ( Mt 2,11) Wataalamu hawa wa mashariki ni maarufu kwa ajili ya zawadi walizompatia: kwa kufikiria lakini historia yao, tunaweza kusema kuwa, hao  awali ya yote walipokea zawadi tatu: zawadi tatu za thamani ambazo zinatutazama hasa sisi pia. Baba Mtakatifu amesema zawadi ya kwanza ni wito. Mamajusi hawakuhisi huo kwa sababu ya kusoma Maandiko au kupata maono ya Malaika, lakini ni  wakati wanajifunza  nyota.  Hii inatueleza kitu muhimu sana: Mungu anatuita kwa njia ya matamanio na shauku zetu kubwa zaidi. Mamajusi waliacha washangazwe na kusumbuliwa na upya wa nyota na walianza mchakato wa safari kuelekea yale ambayo walikuwa hawajuhi.

Siku kuu ya Epifania
Siku kuu ya Epifania

"Wataalamu na wenye hekima walishangazwa zaidi na kile ambacho walikuwa hawajuhi na kile ambacho walikuwa wanajua", Papa amesisitiza. Walihisi kuitwa kwenda zaidi ya. Hiyo ni muhimu kwamba hasa sisi, tunaitwa kutotosheka, kutafuta Bwana, kwa kuondokana na starehe zetu, kutembea kuelekea Yeye na wengine, kwa kujikita ndani ya uhalisia. Kwa sababu Mungu anatuita kila siku, hapa, leo hii, katika ulimwengu wetu. Mamajusi wanazungumza nasi baadaye zawadi ya pili ambayo ni utambuzi. Kutokana na kumtafuta Mfalme, walikwenda Yerusalemu na wakazungumza na Mfalme Herode, lakini ambaye alikuwa na kiu cha madaraka na alitaka kuutumia ili kumuua Masiha mtoto. Lakini mamajusi, hawakuacha wadanganywe na Herode. Walitambua kufanya mang’amzi kati ya hatima ya mchakato na vishawishi ambavyo wanakutana navyo njiani. Waliacha Jumba la Heroda na kwa kuwa na umakini wa ishara za Mungu hawakupita tena, badala yake walirudi kwao kupitia njia nyingine.

Sala ya Malaika wa Bwana katika siku kuu ya Epifania
Sala ya Malaika wa Bwana katika siku kuu ya Epifania

Ni jambo gani muhimu sana kujua namna ya kutofautisha hatima ya maisha kutokana na vishawishi vya safari!, Papa ameongeza.  Kujua namna ya kukataa kile kinacholaghai,  ambacho kinakupeleka katika njia mbaya, ili kujua na kuchagua njia za Mungu! Ni zawadi kubwa ya utambuzi na haipaswi kamwe kuchoka kuiomba katika sala. Kumwambi Bwana tunaomba utujalie uwezo wa kung'amua wema na ubaya”, amesisitiza. Mwisho Mamajusi wanazungumza zawadi ya tatu, ambayo ni mshangao. Baada ya safari ndefu ya watu hawa wa ngazi ya juu kijamii, walipata nini? Mtoto na mama yake. Ni tamasha kwa hakika la huruma, lakini linaloshangaza! Hawakuona malaika kama wale  wachungaji, lakini walikutana na Mungu katika umaskini. Labda walikuwa wanasubiri kuona Masiha wa nguvu, na wa ajabu, na wanamkuta na mtoto. Na pia hawakuwa wanafikiria kuwa wamekosea, kwani walijua kumtambua. Walimpokea kwa mshangao wa Mungu na kuishi kwa mshangao wa kukutana naye, wakimuabubu; katika udogo wa kumjua uso wa Mungu. Kiukweli Sisi sote tuna mwelekeo wa kibinadamu wa kutafuta ukuu katika udogo ambao Mungu anaupenda sana. Kwa sababu Mungu anapatikana kwa  namna hiyo katika unyenyekevu, katika ukimya, katika kuabudu, na katika walio wadogo na maskini.

Papa katika sala ya Malaika wa Bwana 6 Januari 2023
Papa katika sala ya Malaika wa Bwana 6 Januari 2023

Baba Mtakatifu Francisko kwa kuhitimisha amesema "wote tunaitwa na Yesu, wote tunaweza kufanya mang’amuzi ya uwepo wake, wote tunaweza kufanya uzoefu wa mshangao wake. Leo hii ingekuwa vizuri kufanya kumbu kumbu za zawadi hizi, ambazo tulipokea tayari, kwa kufikiria tulivyohisi wakati wa mwito wa Mungu wa maisha;  au wakati labda baada ya ugumu sana tuliweza kutambua sauti yake; au mshangaousiosahuliwa, ambao Yeye alitufanyia na  kwa kutushangaza sana. Mama Maria atusaidie  kukumbuka na kuhifadhi zawadi tulizopokea.

Tafakari kabla ya sala ya Malaika wa Bwana 6 Januari 2023
06 January 2023, 14:01