Papa:Benedikto XVI,mwalimu mkuu wa katekesi,‘mkali&mwenye adabu’
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, kabla ya kuanza katekesi yake Jumatano tarehe 4 Januari 2023 ikiwa ni siku ya Tatu ya maombolezo ya Papa Mstaafu, ameomba kuungna na wale wote ambao karibu wanatoa heshima zao za mwisho kwa Papa Mstaafu Benedikto XVI na kutoa wazo lake kwake kuwa alikuwa mwalimu mkuu wa katekesi. “Fikra zake kali na za upole hazikuwa za kujipendekeza bali za kikanisa, kwa sababu alipenda kutusindikiza daima kukutana na Yesu. Yesu Msulibiwa na mfufuka, Anayeishi na Bwana alikuwa ndiyo hatima ambayo Papa Benedikito alitusindikiza akitushika mikono. Atusaidie kugundua katika Kristo furaha ya kuamini na matumaini ya kuishi”.
Baba Mtakatifu kwa maana hiyo akiendelea amesema katika katekesi hii ni kuhitimisha mzunguko ambao umejikita na mada ya utambuzi, na tunaifanya kwa kuhitisha kwa hotuba ambazo zinaweza kusaidia katika mchakato wa kufanya utambuzi huo. Moja ya hiyo ni ile ya usindikizwaji wa kiroho, umuhimu wake awali ya yote kwa ajili ya kujitambua binafsi ambao tuliona kuwa ni hali muhimu kwa ajili ya utambuzi. Kwa kujitazama katika kioo peke yake daima hakusaidii kwa sababu mtu anaweza kubadilisha picha. Badala yake, kujitazama kwenye kioo kwa msaada wa mwingine, ndiyo inasaidia sana kwa sababu mwingine anakuambia ukweli, wakati ni ukweli na hivyo kukusaidia. Neema ya Mungu kwetu sisi inafanya kazi daima katika asili yetu. Kwa kufikiria moja ya msemo wa kiinjili, Neema tunaweza kuifananisha na mbegu njema na asili katika ardhi (Mt 4,3-9). Ni muhimu awali ya yote kufanya kuelewa bila kuogopa kushirikishana na mantiki za udhaifu zaidi, mahali ambapo tunagundua unyeti zaidi, udhaifu au hofu ya kuhukumiwa. Ole wale ambao hawajihisi kuwa wadhaifu, ni wagumu, na madektata.
Kinyume chake kwa unyenyekevu, kujijua udhaifu binafsi ni jambo linaloeleweka kwa wengine. Kujitambulisha, kujidhihirisha kwa mtu ambaye anatusindikiza katika safari ya maisha, sio kwamba anatuamulia, hapana: lakini anatusindikiza. Kwa sababu udhaifu ni kiukweli, na utajiri wetu wa kweli: sisi sote ni matajiri katika udhaifu; utajiri wa kweli ambao tunapaswa kujifunza kuheshimu na kuukaribisha, kwa sababu unatolewa na Mungu, na unatuwezesha kuwa na uwezo wa kuwa na huruma, na wa upendo. Udhaifu “Unatufanya kuwa binadamu zaidi. Si kwa bahati mbaya, moja ya vishawishi vitatu vya Yesu katika jangwa, ni kile ambacho kinahusiana na njaa, ambacho kinatafuta kuiba udhaifu, kwa kujiwakilisha kama ubaya ambao tunapaswa kuondokana nao, kwa kumzuia kuwa kama Mungu.
Na kinyume chake ni tunu yetu msingi zaidi, kwani kiukweli, ili sisi tuweze kuwa kama Yeye, Mungu alipenda kushirikishana nasi hadi mwisho wa udhaifu wetu. Tutazame msalabani; Mungu aliyeshuka kwa udhafu wetu. Tutazame pango ambapo anafikia udhaifu mkubwa wa kibinadamu. Yeye alishirikishana nasi udhaifu wetu. Na kusindikizwa kiroho, ikiwa ni mpole wa Roho Mtakatifu, anasaidia kutoa mabarakoa za kujidanganya hata yaliyo mabaya katika kujifikiria sisi wenyewe na katika uhusiano na Bwana. Injili inawakilisha mifano kadhaa katika mazungumzo yaliyo wazi na yanayotoa uhuru ambayo alifanya Yesu. Baba Mtakatifu ametoa mfano wa Msamaria, ambao tunasoma kila mara na daima kuna hekima na huruma ya Mungu; tufikirie ile ya Zakayo, tufikirie, ile ya mwanamke mwenye dhambi, Nikodemu na mitume wa Emau, kwa namna ya kumkaribia Bwana. Watu waliokutana na Yesu kweli hawana hofu ya kumfungulia moyo, kumwakilisha ulegevu na kutoweza kwao, yaani udhaifu binafsi. Kwa mtindo huo, ushirikishwaji wao binafsi unageuka kuwa uzoefu wa wokovu, wa msamaha wa bure uliokubaliwa.
Baba Mtakaktifu Francisko akiendelea na katekesi amesema kusimulia mwingine kile ambacho tuliona na kuishi au tunafuta kusaidia, awali ya yote kufanya uwazi ndani mwetu, inapelekea mwanga kwa mawazo mengi ambayo yamo ndani mwetu, na mara nyingi yanatuchafua kwa kujirudia. Ni mara ngapi katika wakati wa giza mawazo mengi yanatujia kwamba: nilikosea yote, sistahili lolote, hakuna anayenielewa, sitoweza kamwe, hatima yangu ni ya kushindwa; ni mara ngapi mawazo hayo yote yamejitokeza. Ni mawazo ya uongo na sumu ambayo kwa kukabiliana na mwingine inasaidia kuyaweka wazi, na hivyo kuweza kuhisi kupendwa na Bwana kwa jinsi tulivyo, wenye uwezo wa kufanya mambo mema kwa ajili yake. Tunashuhudia kwa mshangao kwa njia nyingi ya kuona mambo, alama za wema ambazo zimo daima ndani mwetu. Ni kweli, tunaweza kushirikishana udhaifu wetu sisi kwa sisi, na yule anayetusindikiza katika maisha, maisha ya kiroho, Bwana wa maisha ya kiroho, kama mlei, kuhani na kumwambia: “ Tazama kile kinachotokea kwangu: mimi ni mnyonge, mambo haya yananitokea. Na yule anayekusindikiza atajibu: “Ndiyo, sisi sote tuna mambo haya”. Hii inatusaidia kuzifafanua vizuri na kuona mizizi inatoka wapi na hivyo kuishinda”.
Kwa yeyote yule anayetusindikiza awe wa kike au kiume hachukui nafasi ya Bwana, hafanyi kazi katika nafasi ya mtu anayesindikizwa lakini anatembea karibu naye kandoni, akimtika moyo ili aweze kusoma na kujua kile ambacho kinamsibu rohoni, mahali muafaka ambamo Bwana anazungumza. Kwa maana hiyo msindikizaji wa kiroho anakusaidia kuona verma ni wapi unakosea na hata kukufanya uwe makini katika mambo ambayo hukuwa unafikiria. Anakusaidia kuelewa vizuri zaidi ishara za nyakati, sauti ya Bwana, sauti ya mjaribu, sauti ya magumu usiyoweza kuishinda. Ndiyo maana ni muhimu sana kutotembea peke yako. Papa ametoa mfano kuwa “Kuna msemo wa hekima za Kiafrika , kwa sababu wana fumbo hilo la kabila usemao: “Ukitaka kufika haraka, nenda peke yako; ikiwa unataka kufika salama nenda na wengine”,kwa hiyo nenda uongozane, nenda na watu wako. Ni muhimu. Katika maisha ya kiroho ni bora kuambatana na mtu anayejua mambo yetu na kutusaidia. Na huu ni usindikizaji wa kiroho”.
Usindizwaji huo unaweza kuzaa matunda ikiwa kwa upande mmoja na mwingine kumefanyika uzofu wa umwana na wa udugu kiroho. Tunagundua kuwa mwana wa Mungu kwa watu ambamo tunajigundua kuwa ndugu wana wa Baba Mmoja. Kwa maana hiyo ni muhimu kuingizwa ndani ya jumuiya katika mchakato wa safari. Hatuko peke yetu, sisi ni watu wa watu, wa taifa, wa mji unaotembea, wa Kanisa, wa parokia, wa kundi hilo na mengine yaani jumuiya iliyo katika mchakato wa safari. Huwezi kwenda kwa Bwana peke yako. Hiyo hapana, lazima kutambua hilo vema. Kama inavyosimulia Injili kuhusu mwenye kupooza, kwani mara nyingi tunasaidiwa na kupona shukrani kwa imani ya mwingine ( Mk 2,1-5), anayetusaidia kwenda mbele kwa sababu sisi sote, wakati mwingine tumegandamana kiundani na tunahitaji mwingine aweze kutusaidia ili kushinda shida hiyo kwa msaada. Haiwezekani kwenda kwa Bwana peke yetu na lazima kukumbuka vizuri, kwani mara nyingine ni sisi tunachukua pia jukumu la kaka na dada zetu; hivyo sisi pia ni wasindikizaji wa kusaidia mwingine. Bila uzoefu wa umwana na udugu wa kusindikizwa, inawezekana kufikiria kitu kisicho kweli kwa mtindo wa kutegemea ambacho kinaacha mtu katika hali ya kitoto. Lakini ni muhimu kusindikiza kama wana wa Mungu na ndugu kama sisi.
Bikira Maria ni mwalimu wa utambuzi: Yeye anazungumza kidogo, na anasikiliza sana na kuhifadhi katika moyo (Lk 2,19). Kwa njia hiyo kuna tabia tatu za Mama Maria ambazo ni kuzungumza kidogo, kusikiliza sana, na kuhifadhi katika moyo wake”. Na mara chache anapozungumza anaacha ishara. Papa ameongeza “Inashangaza: mara moja nilisikia bibi kizee mzuri sana, na mcha Mungu sana, hakuwa amesoma taalimungu, alikuwa rahisi sana. Na aliniambia: ‘Je! unajua ni ishara gani ambayo Mama Maria hufanya kila wakati?’. Papa alijibu “Sijui: labda ‘anakukumbatia, anakuita” ... Bibi kizee akajibu ‘Hapana’ na alitumia ishara ambayo Papa hakuilewa na akauliza nini maana yake. Kumbe Bibi kizee alikuwa anamwonesha Yesu na kwamba ndiyo ishara ya Maria anayofanya. Papa amethibitisha kuwa hiyo ni nzuri sana kwa sababu Mama yetu hachukui chochote kwa ajili yake mwenyewe, bali anatuonesha Yesu. Katika Injili ya Yohane, kuna sentesi moja fupi aliyosema kuwa: “Fanyeni atakayowambia (Lk 2,5). Kufanya kile ambacho Yesu anatueleza. Maria anajua kuwa Bwana anazungumza katika moyo wa kila mmoja, na anamwomba kutafsiri neno hilo katika matendo na chaguzi. Yeye alitambua kufanya zaidi ya kila yoyote yule na kiukweli yupo katika wakati muhimu wa maisha ya Yesu hasa katika wakati ule mgumu sana wa kifo chake msalabani.
Utambuzi kwa hiyo ni sanaa, sanaa ambayo inaweza kujifunza na ambayo ina kanuni zake. Ikiwa inachukuliwa vizuri, hiyo inawezesha kuishi uzoefu wa Mungu, ambaye anapaswa kuombwa daima, bila kweli kujifikiria kuwa wataalamu au wanaojitosheleza. Ni muhimu kuomba Bwana, kwamba nijalie neema ya kupambanua nyakati za maisha, kile ninachopaswa kufanya, na kile ninachopaswa kuelewa. Nipe neema ya kupambanua na unipe mtu wa kunisaidia kupambanua. Sauti ya Bwana inaweza daima kutambuliwa, kwani ina mtindo mmoja, ambao ni sauti ya amani, inayotia moyo na ya uhakika katika matatizo. Injili inatukumbusha kila wakati kuwa “Usiogope” ni jinsi gani lilivo zuri neno hilo, kama Malaika alivyomwambia Maria ( Lk 1,30)! Baada ya ufufuko wa Yesu; Yesu alimwambia Petro Usiogope, aliwambia wanawake asubuhi ya Pasaka Msiwe na hofu . Usiogope ! ni neno ambalo Bwana anarudia hata kwetu, ikiwa tunajikabidhi katika Neno lake, ikiwa tutatumia muda wetu wa maisha vizuri, na kuweza kuwasaidia wengine. Kama Zaburi isemavyo : “Neno lako ni Taa ya miguu yangu, na katika safari yetu (119,105).
Salamu mara baada ya Katekesi: Kongamano la Chama cha walimu katoliki
Papa Francisko, mara baada ya Katekesi yake, akiwasalimia mahujaji kwa lugha mbali mbali, pia amewakaribishwa kwa moyo mkunjufu mahujaji wanaozungumza Kiitaliano. Hasa, amewasalimu washiriki wa Kongamano la Chama cha Walimu Wakatoliki. “Wapendwa kaka na dada, ninawatia moyo kujitolea kwa upole kwa malezi ya wanafunzi, wanaohitaji kuona ndani yenu mashuhuda wa ukweli, wa matumaini, wa huruma”.
Kumtafuta Ktisot nuru ya Ulimwengu
Hatimaye mawazo yangu yamewaendea vijana, wagonjwa, wazee na wanandoa wapya, ambao ni wengi. Amekumbusha siku ya maadhimisho ya tokeo la Bwana ambalo litaadhimisha Ijumaa tarehe 6 Januari, siku ambayo Mamajusi walileta zawadi kwa Bwana. Papa Francisko amesema kama Mamajusi, watambue jinsi ya kumtafuta Kristo nuru ya ulimwengu na Mwokozi wa wanadamu kwa akili iliyo wazi.
Maombi kwa ajili ya watu wa Ukraine wanaoteseka
Papa ameongeza kusema: “Ninawasihi kila mtu kudumu katika ukaribu wa upendo na mshikamano na watu wa Ukraine waliouawa kishahidi ambao wanateseka sana na wanaendelea kuteseka, kwa kuwaombea zawadi ya amani. Tusichoke kuomba. Watu wa Ukraine wanateseka, watoto wa Ukraine wanateseka: tuwaombee. Na kwa baraka zangu zote”.