Papa Francisko:mchezo ni huduma ya mtu,sio mantiki ya nguvu
Na Angella Rwezaula: - Vatican
Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican Jumatatu tarehe 30 Januari 2023 na Wasimamizi na Wanamichezo wa Shirikisho la Italia la mchezo wa Mpira wa Wavu ambapo mara baada ya salamu kwa viongozi waliosindikiza ujumbe huo kike na kiume ambao wengi ni vijana amesema wapo pamoja na Sekretarieti ya Baraza la maaskofu Italia wakitimiza mchakato kwa ajili ya kueneza katika eneo lote na katika jamii ya michezo thamani ya elimu ya mchezo, kwa matarajio fungamani ambayo yanaunganisha ufundi wa uwezekano wa kutoka wakiwa bora, iwe katika shugughuli za michezo na katika maisha. Mchezo kiukweli lazima na daima uwe kwa huduma ya mtu na jamii na sio kwa maslahi au mantiki za nguvu.
Kwa maana hiyo Papa amewatia moyo kufuata mchakato walio uanzisha huku akiwapa maelekezo ambayo yanaendana na matendo msingi wa mchezo wao. Awali ya yote ni kufanya matani ambayo kwa kujitokeza tu yanatoa njia ya mchezo. Katika timu kama ilivyo katika maisha ya kila siku inabidi kuchukua uwajibijaji na kuwa ndani mwake. Kamwe hakuna kubaki umesimama. Mchezo unaweza kusaidia sana kushinda vishawishi vya aibu na udhaifu na kukomaa katika umbuzi binafsi wa kuwa mstari wa mbele bila kusahau kamwe kuwa hadhi ya mtu binadamu inajenga hatima na kipimo cha kila shughuli za mchezo (Papa Yohane Paulo Mt Jubileio ya mchezo 29 Oktoba 2000)
Baada ya matani inaendana na upokezi. Kama ilivyo na haja ya kuwa tayari kupokea mpira ili kuuelekeza katika eneo jingine, ndivyo ilivyo muhimu kuwa na uwezekano wa kupokea ushauri na kuusikiliza kwa unyenyekevu na uvumilivu. Huwezi kuwa bingwa bila kiongozi, msaada wa mwalimu aliye tayari kukusindikiza, kukutia moyo, kukusahihisha bila kukunyenyekeza, kukuinua wakati unaanguka na kushirikishana furaha za ushindi. Wanahitajika watu ambao wawe kitovu thabiti cha kufikia, wenye uwezo wa kufundisha kupokea wema, kubaini talanta binafsi za wachezaji ili kuzifanya zizae matunda vema.
Kisha Papa amesema kuna ya kuinuka, kwamba hatua kuelekea mwezako ambaye anakazi ya kuhitimisha tendo. Hii ina maana kwamba sisi hatuko peke yetu kamwe kwa sababu, daima kuna mtu wa kuhudumia. Wachezaji wa timu ni kama kiungo cha mwili, kama alivyoeleza Mtakatifu Paulo kwamba: “Na kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia nacho, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja nacho.” (1 Wakor 12,26).Katika ulimwengu ambamo watu wanajizatiti kuonekana na kujitokeza kwa gharama yoyote ile, ambapo ubinafsi unakuja mbele yetu, ambapo wanyonge na wasio na tija wanatupwa, michezo inaweza kuwa ishara ya kushawishi ya umoja, ushirikiano, na inaweza kuzindua ujumbe mkali wa amani na urafiki.
Hatua ya kushambulia kwa hakika ni ya uamuzi ambayo inakuwezesha kupata pointi na kujenga ushindi. Baba Mtakatifu ameeleza kuwa Mchezo lazima uendeleze ushindani wenye afya, bila kuangukia katika jaribu la kushinda kwa kukanyaga sheria. Sadaka ya mafunzo, na uzito ni mambo muhimu ya mchezo, wakati mazoezi ya madawa ya kuongeza nguvu pamoja na kuwa hatari, ni udanganyifu unaoondoa uzuri na furaha ya mchezo, kuutia doa kwa uwongo na kuufanya kuwa mchafu.
Baba Mtakatifu amebainisha kuwa ili kupinga mashambulizi, ukuta unajengwa. Neno hili linatufanya tufikirie kuta zilizopo katika sehemu mbalimbali za dunia, ishara ya mgawanyiko na kufungwa, ya kutokuwa na uwezo wa watu kufanya mazungumzo, ya dhana ya wale wanaofikiri kwamba mtu anaweza kujiokoa peke yake. Badala yake, katika mpira wa wavu, unapozuia, unaruka juu ili kukabili mpinzani: ishara hii hutusaidia kufikiria neno kwa maana chanya. Kuruka juu kunamaanisha kujitenga na ardhi, kutoka katika mali na kwa hivyo kutoka kwa mantiki zote za biashara zinazodhoofisha roho ya michezo. Pesa na mafanikio lazima kamwe kuacha sehemu ya mchezo, ya furaha. Na kwa hilo Papa amependekeza sana: wasiache kamwe mwelekeo wa mazoezi ya mchezo. Mchezo ni ukomavu au sio mchezo. Hii lazima ihifadhiwe vizuri, vizuri, kwa sababu kwa hili pia linaweka moyo wao. Amewashukuru ujio wa ona amewasahuru daima wawe mashuhuda wa dhati na ukweli. Kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu amesema Vijana wengi wanawatazama na kuwashangilia: wao ni mfano wao kwa hiyo usiwakatishe tamaa! Ni matashi mema kwamba wacheze vyema huku ukiburudika, wakieneza maadili ya urafiki, mshikamano na amani ndani na nje ya uwanja. Amehitimisha kwa kuwaomba wasali kwa ajili yake tafadhali.