Tafuta

2023.01.20 Papa na watawa wa shirika la huruma za Kijamii 2023.01.20 Papa na watawa wa shirika la huruma za Kijamii  (Vatican Media)

Papa:kabiliana na changamoto za kijamii kwa silaha ya upendo

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Watawa wa Huduma ya Jamii na hotuba iliyowakabidhi,anamkumbuka mwanzilishi Margit Slachta,mfasiri wa shirika hilo la upanedo kijamii lililotajwa katika waraka wa Fratelli tutti:“Karama yake imebadilika kulingana na hali mbalimbali za kisiasa na kijamii, hadi leo hii.Hata kama mwanamke mtawa alidumisha dhamira ya kisiasa kama hiyo.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana Ijumaa tarehe 20 Januari 2023 na Shirika la watawa wa Huduma ya kijamii ambao amewakaribisha. Baba Mtakatifu Francisjko, amependa kuwakabidhi Hotuba yake na kuzungumza moja kwa moja. Katika hotuba yake aliyo wakabidhi anawaleza kwamba wamefika katika kusherekea miaka 100 tangu kuanzishwa shirika lao. Kwa hakika ni tukio maalum sana kwa ajili yao na hivyo wamependelea kufanya kumbu kumbu wakiwa katika kaburi la Mtume Petro. Amewakikishia  kuwa pia ni furaha kwa Kanisa zima, kwa sababu kila karama ni zawadi ya Mungu ambaye anaitoa, kwa njia ya Roho Mtakatifu, neema ambayo kuna haja ya kila wakati wa kihistoria. “Katika hilo kuna fumbo: zawadi ambazo tunazipokea kutoka kwa watu na zile ambazo tunaweza kuzitengeneza kwa nguvu zetu, zinaweza kuharibika. Kinyume chake zawadi za Roho zina maisha mapya daima na kila wakati katika muda na katika mahali zinazaa na zikujifumbua, kwa kubaki wakati huo huo aminifu katika mizizi yake.

Papa akizungumza na watawa wa shirika la huduma za kijamii
Papa akizungumza na watawa wa shirika la huduma za kijamii

Kutokana na hiyo Papa amesema inawezakana kutazama karama ambayo kwa miaka 100 iliyopitia zilipokelewa na mwanzilishi Margit Slachta, na katika mchakato wa kipindi na katika mafundisho jamii ya Kanisa, zilikubaliwa katika hali tofauti za kisiasa na kijamii, hadi kufikia katika siku zetu. Papa Francisko ameshangazwa kwamba hata mtawa, mwanzilishi wao, aliweka juhudi katika siasa sana. Ni wa kuvutia uthibitisho wake, wakati wa mauaji ya kimbari, kwamba kanuni za imani ziliwalazimisha watawa kuwalinda Wayahudi, kwa kuhatarisha maisha yao wenyewe. Ni ukweli ambao una gharama sana kukubali kwamba mashahidi wengi walikufa kwa imani, si kwa sababu ya kunyimwa uhuru tu wa kumwabudu Mungu wao, lakini kwa usahihi wa maisha ambayo imani ilikuwa inawatuma na matokeo yake, kwa ajili ya kulinda uhuru, haki na ukweli. Inawezakana kushangazwa, lakini ni ukweli wa jaribu la kwanza ni shahidi Yohane Mbatizaji. Nabii aliyekufa baada ya kumkaripia aliyekuwa anaishi, si kwa mujibu wa sheria ya Mungu, na kwa sababu ya kuwaalika watu wakatae mfumo tofauti ambao unapeleka mbali na mapenzi ya Mungu, na kwa hiyo akawa shuhuda wa ukweli mkubwa.

Mkutano wa Papa na watawa wa shirika la huduma za kijamii
Mkutano wa Papa na watawa wa shirika la huduma za kijamii

Katika muktadha huo, mwanzoni kwa karne iliyopita, katika mabadiliko ya kijamii ambayo yaliona njia za vita vya dunia, ndiyo ulikuwa wakati mkali sana, ambao Mungu alimtia moyo wa kuzaliwa Shirika lao. Baba Mtakatifu katika hotuba yake aliyowakabidhi amebainisha kwamba wakati ule sio tofauti na wakati wa sasa, kama hapo awali, wito wa kuwa shuhuda unaendelea sasa. Na ingekuwa vizuri  ikiwa katika mioyo yao ingesikika tena maneno ya Margit, kwa mkazo ule ule ambao kwa hakika ulikuwa wa watawa wa kwanza. Hiyo ni chachu kwao, ambayo inawafundisha kukabiliana na changamoto za kijamii kama walivyofanya wao dhidi ya Wanazi, kwa kuwa na silaha moja ya upendo. Baba Mtakatifu Francisko amsisitiza kuwa mwanzilishi wao, Kanisa na Roho Mtakatifu bado vinawaalika daima ukweli huo huo kwani hakuna upendo ulio mkubwa zaidi wa kutoa maisha kwa ajili ya wengine. Upendo kijamii kama  Papa alivyokumbusha katika Waraka wa Fratelli Tutti, ambao hata katika maandishi ya Margit Slachta, ni jaribu ambalo linaonesha mapya hayo. Mungu wapatie nguvu kwa ajili ya kushuhudia upendo huo, ukweli na haki katika wito ambao amewaita. Ni kumuomba kwa njia ya maombezi ya mwenyeheri Sara Salkaházi. Na Yesu awabariki na Bikira awalinde.

Hotuba ya Papa kwa watawa kijamii

 

20 January 2023, 15:57