Tafuta

2023.01.16  Wajumbe wa Shirikisho la Vyama vya Ibada za Watu wa Mungu,Italia. 2023.01.16 Wajumbe wa Shirikisho la Vyama vya Ibada za Watu wa Mungu,Italia.  (Vatican Media)

Papa Francisko:Ibada za Watu wa Mungu ni urithi mkubwa!

Baba Mtakatifu Fransisko ameviomba vyama vya Ibada za Watu wa Mungu Italia vilivyoanzishwa karibu mika miaka 25 iliyopita wasijitenge na nafsi zao,bali wapyaishe ushirika na Kanisa,wakiwekeza tena katika urithi wa kiroho,kiuchumi,kisanii na kihistoria.Kwa ibada zao za kizaman,uzoefu wao uhuishwe na maisha ya kiroho na kujitolea madhubuti kwa upendo.

Na angella Rwezaula; - Vatican.

Baba Francisko Jumatatu tarehe 16 Januari 2023, amekutana na Shirikisho la vyama vya ibada za watu wa Mungu vya Majimbo nchini Italia na kuwakaribisha kwa furaha. Amemshukuru Rais wao Dk. Rino Bisignano,  Askofu Michele Pennisi, Msimamizi wa Kikanisa Kitaifa na vile vile  wajumbe wote wa Baraza Tendaji la Shirikisho hilo, Waratibu na Wasaidizi wao Kikanda waliokuwapo. Kwa kutoa  kidogo historia ya shirikisho amebainisha kuwa kwa  kuanzishwa kwake  mnamo mwaka 2000 katika muktadha wa Jubilei kubwa, linafanya kazi sasa zaidi ya miaka 20 kwa kukaribisha, kusaidia,na kuratibu utajiri na mkubwa wa uwepo wa Washirika wengine katika Majimbo ya Italia.   Kwa sasa wanajifunga vibwebwe, kuelekea kuadhimisha miaka 25,  miaka miwili ijayo katika muktadha wa Jubilei nyingine kubwa ya 2025 ambayo inaongozwa na Kauli mbiu: “ Wanahija wa Matumaini”.  Kwa maana hiyo amesema tumeanza kujiandalia wakati huo  nguvu katika maisha ya Kanisa na wao kiukweli wana maana kubwa katika maandalizi na baadaye kusheherekea.

Papa Francisko amekutana na Wajumbe wa wanachama wa Ibaza za Kimungu nchini Italia
Papa Francisko amekutana na Wajumbe wa wanachama wa Ibaza za Kimungu nchini Italia

Baba Mtakatifu Francisko amesema awali ya yote wao ni kama mkondo ambao katika uso wa eneo lote la  kitaifa na kwa wingi wa watu ambao wanawahusika  kwa karibia elfu tatu na mia mbili wanachama waliojiandikisha na zaidi walioko ambao lakini hawajajiandikisha na milioni mbili ya wajumbe; ambao wote  wanajumuisha jumuyia kubwa za familia. Na marafiki ambao kwa njia yao wanaunga mkono shughuli zao. Ni jambo la kushangaza, ambalo limemjia akilini kwa kile ambacho Mtaguso wa II wa Vatican ulisema kuhusiana na  asili na utume wa walei katika Kanisa  hasa kwamba: “Wameitwa na Mungu kuchangia, karibu kutoka ndani kama  chachu, kwa kutakatifuza ulimwengu (Lumenium gentium,31). Chachu yao, inaonekana vizuri katika kiungo cha kikanisa na kijamii nchini Italia na lazima kukitunza ili kibaki hai, kwa sababu kiweze kutoa chachu kwa unga wote. Msisitizo wa Mtakatifu Yohane Paulo II katika mahubiri yake mnamo 1984 aliposema: “ Leo hii dharura ya uinjilishaji unasaidia kwamba Wanachama washiriki kwa kina na zaidi moja kwa moja katika shughuli  ambazo Kanisa linatimiza ili kupeleka mwanga, ukombozi, neema ya Kristo kwa watu wa nyakati zetu (Jibilei ya Wanachama Wa Ibadaza wa watu wa Mungu, 1 Aprili 1984). Katika muktadha wa uinjilishaji moja ya ibada za watu, inaunda kiukweli nguvu kubwa ya kutangaza, ambayo inawapatia wanaume na wanawake wa nyakati zetu (Wosia wa Evangelii Gaudium,126).

Papa Francisko amebainisha kuwa kifungu cha 126 lakini, kuhusu  Ibada za Watu wa Mungu,  kuna  moja ambayo inaendelea kuwa maandishi yenye nguvu zaidi na  ambayo husaidia sana, ni ya Mtakatifu Paulo VI, katika Evangelii nuntiandi. Katika kurejea andiko hilo liliweka wazi wazi nafasi ya Ibada za  Watu wa  Mungu  katika maisha ya Kanisa. Na kisha, Wosia huo wa Evangelii nuntiandi bado unatumika leo hii kwa sababu ni wosia wa kinabii, hati ya kitume ya  kinabii ambayo inasaidia, na mbayo  bado inakwenda mbele. Kwa njia hiyo, Baba Mtakatifu Francisko amewatia moyo kukuza jitihada ya ubunifu na mwendelezo wa maisha ya kivyama na katika uwepo wao wa upendo, ambao ni msingi mkuu wa zawadi ya Ubatizo ambayo inapelekea michakato ya safari ya ukuaji chini ya mwongozo wa Roho Mtakatifu. Waache waongozwe na Roho na watembee kama wanavyofanya katika maandamano ya kikanisa, wafanye hivyo katika maisha yao ya kijumuiya. Utajiri na kumbu kumbu ya historia yao, isiwe kamwe sababu ya kujikunja binafsi, ya kusheherekea kwa masikitiko ya yaliyopita,  ya kufunga kwa yale yaliyopo au ugumu wao kwa wakati ujao; badala yake  viwe chachu ya nguvu na inayowekeza leo hii katika urithi wao, kiroho, kibinadamu, kiuchumi, kisanaa, kihistoria na hasa kitamasha, kwa kujifungulia ishara za nyakati na mishangao ya Mungu.

Papa Francesko amekutanana Wajumbe wa Wanachama wa Ibada za Watu wa Mungu Italia
Papa Francesko amekutanana Wajumbe wa Wanachama wa Ibada za Watu wa Mungu Italia

Ni kwa imani hiyo na kwa ufunguzi huo wa awali ambao waliowatangulia na kutoa asili katika wakati wao wa nawachama washirika. Bila imani hiyo na ufunguzi huo, leo hii wasingekutana hapo na idadi kubwa namna hiyo ili kumshukuru Bwana kwa wema walioupokea na kutimiza. Baba Mtakatifu aidha amependa kuwaaalika katika mchakato wao safari kwa mujibu wa misingi mikuu mitatu: Uinjilishwaji, kikanisa na kimisionari. Maelekezo hayo ameyafupisha kwa namna hii; Kutembea katika nyayo za Kristo, kutembea pamoja na kutembea kutangaza Injili na kwa hiyo washirika na ibada za watu wa Mungu wanapaswa kutangaza. Awali ya yote kutembea katika nyayo za Kristo. Papa amewashauri wakuze kiini cha Kristo katika maisha yao, kwa kusikiliza kila siku neno la Mungu. na hii ni muhimu sana: ukaribu na Injili. Ni lazima wasome Injili kila siku.

Baba Mtakatifu amewashauri: muwe na kitabu cha mfukoni cha Injili, mbebe mfukoni au mkoba wako kisha ukiwa na (una) muda fulani (wakati), unasoma jambo  wakati wa mchana. Kipande kidogo, lakini hii kila siku...Injili inawafanya mkue...mnafanya moyo wenu ukue. Mgusano wa kimwili na Injili na kisha kuwasiliana kiroho. Ninawasihi kukuza ukuu wa Kristo katika maisha yenu, katika kusikiliza Neno la Mungu kila siku”, alisisitiza Papa.  Akiendelea alisema kuandaa na kushirikisha kawaida vipindi vya malezi na bila kukosa kwenye sakramenti, katika ushiriki wa kina wa sala binafsi na zile za kiliturujia. Utamaduni wao wa kisazami wa kiliturujia na ibada viongozwe kwa shauku maisha yao ya kiroho na jitihada za dhati katika kutoa upendo.  Papa amehimiza kuwa wasiwe na hofu ya kujisasisha katika umoja na katika safari ya Kanisa, kwa sababu wanaweza kuwa zawadi inayowezekana na kueleka kwa wote na katika miktadha ambayo wao wanaishi na kuhudumia na  ile chachu ya kukaribisha kwa imani hata walio mbali.

Papa amekutana na Wajumbe wa Wanachama wa Ibada za Watu nchini Italia
Papa amekutana na Wajumbe wa Wanachama wa Ibada za Watu nchini Italia

Pili kutembea pamoja, ambapo Baba Mtakatifu ameifafanua kuwa historia ya wanachama hao wa ibada za Mungu wanatoa kwa Kanisa uzoefu wa kisekulari wa kisinodi,  na kuelezea kwa njia ya vyombo vya kijumuiya vya malezi, vya utambuzi na mashauriano, na kwa mawasiliano mazuri na Kanisa mahalia, na Maaskofu na majimbo. Mabaraza yao na mikutano yao kama alivyo waomba Mpendwa Papa Mstaafu benedikito XVI kwamba zisipinguzwe kamwe  kuwa mikutano ya kiutawala au maalum; daima, zaidi ya yote, pawe mahali pa kumsikiliza Mungu na Kanisa, na kwa mazungumzo ya kidugu, yenye hali ya sala na mapendo ya dhati. Ni kwa njia hii tu ndipo wataweza kukusaidia kuwa ukweli hai na kutafuta njia mpya za huduma na uinjilishaji”.

Na mantiki ya tatu inawapeleka katika ukuu wa safari yao, yaani kutembea kwa kutangaza Injili, kwa kushuhudia na imani yao, na kuwatunza ndugu hasa katika umaskini mpya wa nyakati zetu, kama walio wengi wao walivyoonekana katika kipindi cha Uviko. “Fanyeni utafiri muombe ni umaskini gani mpya. Sisis labda hatujuhi lakini upo na mwingi sana umaskini mpya”. Historia ya Washirika ina maana hiyo kubwa ya urithi wa kikarama. Kwa njia hiyo wasiache urithi huo upotee! Wahuishe karama ya huduma na ya utume , kwa kujibu kwa ubunifu na ujasiri kwa wenye kuhitaji wa wakati wetu. Papa alipenda kumalizia kwa kutoa mwaliko kwa upendwa wa  kuwa "wamisionari wa upendo na huruma ya Mungu [...] wamisionari wa huruma ya Mungu, ambao husamehe daima, wanangoja daima, na wanapenda sana!" (Mahubiri  Siku ya Washirika na Ibada za Watu wa  Mungu 5 Mei 2013). Mama Yetu, ambaye kwa vyeo vingi unamheshimu kama Mama yako, akulinde na kukuongoza kila wakati. Ninawabariki kwa moyo mkunjufu, ndugu na dada wote na familia zenu.

Papa na wajume wa Ibada za Watu wa Mungu Italia
16 January 2023, 16:40