Tafuta

2023.01.01 Sala ya Malaika wa Bwana Mosi Januari 2023. 2023.01.01 Sala ya Malaika wa Bwana Mosi Januari 2023.  (Vatican Media)

Papa Francisko:Hapana vita,Mzozo wa Ukraine hauvumiliki!

Papa Fransisko baada ya Sala ya Malaika wa Malaika ya Kwanza kwa Mwaka 2023 na sambamba ya Maadhimisho ya Siku ya 56 ya Amani Duniani,amezindua kwa upya kilio cha watu wa dunia wanaoteseka kwa sababu ya fujo na ghasia.Baada amezindua wito wake kwamba rasilimali ziende kwenye maendeleo,afya,lishe,elimu na kazi.

Na Angella Rwezaula; -Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, mara baada ya tafakari na sala ya malaika wa Bwana, kwa waamini na mahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican, Dominika tarehe Mosi Januari 2023 ambapo Mama Kanisa anaadhimisha Siku Kuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu, sambamba na Siku ya 56 ya Amani duniani amesema kuwa: “Kwa wote mliopo hapa na kwa wanaofuatilia kupitia vyombo vya habari, ninawatakia heri ya mwaka mpya. Ninatoa shukrani zangu za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Italia, Mheshimiwa Sergio Mattarella, nikiwaombea ustawi kwa watu wa Italia; kwa matashi hayo hayo pia kwa ajili ya  Rais wa Serikali.

Malaika wa bwana ya Kwanza kwa mwaka 2023
Malaika wa bwana ya Kwanza kwa mwaka 2023

Baba Mtakatifu akiendelea amesema: “Katika siku hii, ambayo Mtakatifu Paulo VI alitaka itolewe  kwa sala na tafakari kwa ajili ya amani duniani, tunahisi hata kwa nguvu zaidi na bila uvumilivu wa tofauti ya vita, ambavyo katika Ukraine na maeneo mengine mengi yanaendelea kupanda kifo na uharibifu. Hata hivyo, tusikate tamaa, kwa sababu tuna imani kwa Mungu, ambaye katika Yesu Kristo ametufungulia njia ya amani. Uzoefu wa janga la uviko, limetufundisha kwamba hakuna mtu anayeweza kujiokoa peke yake, lakini kwamba kwa pamoja tunaweza kutembea katika njia za amani na maendeleo”.

Malaika wa Bwana ya Kwanza kwa mwaka 2023
Malaika wa Bwana ya Kwanza kwa mwaka 2023

Baa Mtakatifu Francisko aidha amesema "Katika Ulimwenguni kote, na katika watu wote, kilio kinaongezeka: kwamba hapana vita! Hapana kuongeza silaha tena! Rasilimali ziende kwa ajili ya maendeleo, afya, lishe, elimu na kazi. Miongoni mwa mipango isiyohesabika aidha iliyohamasishwa na jumuiya za Kikristo, inakumbusha yale maandamano ya  Kitaifa yaliyofanyika tarehe  31 Desemba 2022, huko Altamura, baada ya misafara minne iliyopeleka mshikamano nchini Ukraine”. Baba Mtakatifu Francisko vile vile amewasalimia na “kuwashukuru marafiki wengi wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio ambao wamekuja tena mjini Vatican mwaka huu kushuhudia ahadi yao ya “amani katika nchi zote”, na katika miji mingi ya ulimwengu. Asante, kaka na dada wapendwa wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio!”

Malaika wa Bwana  ya kwanza kwa mwaka 2023
Malaika wa Bwana ya kwanza kwa mwaka 2023

“Ninatoa salamu kwa bendi mbili zinazoandamana kutoka Virginiana Alabama, nchini Marekani, tutafurahi kuzisikia baadaye!, alisema Papa. "Ninawasalimu vijana wa Harakati la Regnum Christi,  asante! Wanasikika kutoka nchi mbalimbali za Amerika na Ulaya; pamoja na watoto na familia za Jumuiya ya Cenacolo, baraka kwa Mama Elvira na kwa jumuiya zote. Ninawatakia wote Dominika njema na mwaka mpya wenye furaha". "Mlo mwema na kwaheri ya kuonana."

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana Mosi Jan 2023
01 January 2023, 13:33