Papa Benedikto XVI na uenezaji wa imani katika enzi za kidijitali
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Sifa yake kama mtaalimungu mkuu inakubaliwa kwa kauli moja, lakini Papa Mstaafu Joseph Ratzinger pia alikuwa mzungumzaji wa ajabu, mwenye hadhi yake mashuhuri, ambaye urithi wake bila shaka utavuka kikomo cha muda cha kuwepo kwake duniani. Uhakika ni kwamba Papa Benedikto XVI hakuwa mwasilianaji kwa watu wengi wazima tu lakini pia alivutia usikivu wa mamilioni ya vijana wakati wa Siku za Vijana Ulimwenguni ambapo haupunguzi kwa vyovyote vile thamani ya mtindo wake wa mawasiliano. Kwanza kabisa, kama mtaalimungu, alionesha kwamba hata mada za kiakili sana zinaweza kuelezewa kwa mtu wa kawaida na zinaweza kufikiwa na hadhira kubwa, sio wataalamu tu. Mafanikio ya kitabu chake cha (Introduction to Christianity), Kuingizwa wa Ukristo ambacho kipo hadi leo hii, zaidi ya miaka 50 baada ya kuchapishwa, ni kitabu ambacho kinachouzwa zaidi ulimwenguni pote katika uchapishaji wa kidini, kinaonesha uwezo wa kuzaliwa wa Ratzinger wa kutoa sababu za imani katika Yesu Kristo na kufanya hivyo kwa hoja zilizo wazi na zenye kuvutia. na lugha ya kusadikisha.
Hilo linawezekana kusemwa kwa utatu wa Yesu wa Nazareti, kazi ambayo Joseph Ratzinger alijimimini nafsi yake yote, akifanikiwa kuikamilisha kabla ya kung’atuka, licha ya taabu za kutawala Kanisa la ulimwenguni. Kwa hiyo inawezekana kusema kwamba Benedikto XVI alikuwa shuhuda mkuu wa Imani kwa mawazo yake makuu na ,kwa upendo kama ilivyojitokeza hivi karibuni katika Wosia wake wa kiroho uliotolewa mara tu baada ya kufariki kwa sababu ya jinsi alivyoweza kuuwasilisha. Alifanya hivyo hasa kupitia maandishi yake, hotuba (baadhi ya kukumbukwa, kama wengi katika siku hizi wanavyokumbuka), na mahubiri, yaliyofafanuliwa kama “makuu” na Padre Federico Lombardi, SJ, (aliyekuwa mkurugenzi wa Radio Vatican , na msemami wa Vyombo vya Habari kwa mapapa wa hivi karibuni ) kwa upatanisho wenye hekima kati ya taalimungu, ujuzi wa Maandiko, na mambo ya kiroho. Hata hivyo, Papa Benedikto mzaliwa wa Ujerumani hakuwahi kushindwa kwa ujasiri kuthubutu katika uwanja mpana wa mawasiliano. Ni yeye aliye kuwa Papa wa kwanza kukutana na waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia na makasisi, suala lenye umuhimu sana na mkubwa katika uwezo wa kimawasiliano ambapo Ratzinger aliweka umakini wa usikilizaji katikati.
Namna yake ya kusikiliza, iliyoshuhudiwa katika mikutano wakati wa ziara zake za kimataifa iliwekwa alama ya huruma, hali zote mbili muhimu za kufanya mchakato wa uongofu kwa moyo ambao pia Papa Francisko anauendeleza kwa imani na ambao ulikuwa msingi mnamo mwezi Februari 2019 katika kilele cha Mkutano kuhusu Ulinzi wa Watoto na watu wazima waathirika. Ingawa ukosoaji haukukosekana kutoka vyombo fulani vya habari kuhusu baadhi ya maamuzi yake, Papa Benedikto XVI daima alidumisha mtazamo chanya kuelekea ulimwengu wa tasnia ya mawasiliano. Mazungumzo yake na mwandishi wa habari wa Ujerumani Peter Seewald yaliweka Nuru katika Ulimwengu, kwenye kitabu cha mahiojiano ambacho kinagusa masuala yote nyeti ya upapa wake, hata kuhusu kujiuzulu kwake.
Papa Benedikto XVI pia alikuwa Papa wa kwanza kutuma ujumbe mfupi (kwa vijana katika Siku ya vijana (WYD) huko Sydney), kwa mazungumzo na wanaanga kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga, kujibu maswali kwenye Televisheni, Ijumaa Kuu (mnamo mwaka 2011), na kuandika tahariri katika gazeti la ‘Financial Times’ wakati wa Noeli kwa kuzingatia ushiriki wa Wakristo katika ulimwengu mambo leo. Zaidi ya yote, Benedikto XVI alikuwa Papa wa kwanza kukabiliana na matukio ya mitandao ya kijamii, ambayo yalirekebisha kwa kina katika muktadha wa mawasiliano ya kimataifa kwa usahihi katika miaka ya upapa wake. Si chini ya ujumbe wake mara tano katika Siku za Mawasiliano Duniani ambao umetengwa kwa ajili ya uwanja huo wa kidijitali. Kwa pamoja zinajumuisha aina ya muunganisho wa Majisterio ya Kanisa juu ya ukweli huu mpya ambao umebadilika, sio tu jinsi tunavyowasiliana bali pia jinsi tunavyohusiana na wengine. Papa Benedikto XVI alikuwa wa kwanza kuelewa maana ya mapinduzi ya mitandao ya kijamii, ambayo si njia sana ya kutumika kama mazingira ya kukaliwa. Kwa hiyo alibuni neno la “bara la kidijitali” kwa mitandao ya kijamii, kwa kubainisha kuwa , kama zile za kijiografia, bara la kidijitali linahitaji kujitolea kwa waamini, hasa walei, sambamba na njia ya Inter Mirifica, kueneza uinjili katika eneo hilo jipya la utume. Papa Mstaafu pia alielewa kwamba tofauti ya uongo katika mtandao na halisi lazima ziondolewe, kwani kile kinachoshirikishwa na kuingiliana nacho, kwenye majukwaa mapya kina matokeo halisi katika maisha ya kila siku ya watu.
Papa mstaafu Benedikto XVI aliwahimiza Wakristo kuwa mashuhuda wa kidijitali badala ya kuwa washawishi, ili kubadilisha mitandao ya kijamii kuwa milango ya ukweli na imani. Kwa maana hiyo aliwahimiza wawe kweli wainjilishaji kidigitali. Na hakufanya hivyo kwa maneno tu. Kwani ilikuwa ni mnamo tarehe 12 Desemba 2012, akawa Papa wa kwanza kutuma ujumbe wa Twitter kupitia akaunti ya @Pontifex iliyofunguliwa siku chache kabla. Uamuzi wake wakati fulani umelinganishwa na Papa Pius XI aliyeanzisha Radio Vatican. Sio kila mtu aliyeidhinisha kitendo chake, akihofia kufichuliwa na Papa kwa ukosoaji na kuchukizwa, lakini Papa Mstaafu Benedikto XVI alishawishika kwa chaguo lake la kufuata mwelekeo wa uinjilishaji mpya. Kwa mara nyingine tena, Papa alitambua jinsi ya kunyakua uwezo wa uvumbuzi wa kiteknolojia ili kuwafikia watu ambao wangebaki kutengwa na utangazaji wa Injili.
Wiki chache baada ya akaunti kufunguliwa, Papa Msaafu Benedikto XVI aliacha huduma yake ya Upapa. Akaunti ya Twitter ya @Pontifex, baadaye “ilifunguliwa upya” na mrithi wake, Papa Francisko, ambaye leo hii, kupitia tweets zake katika lugha 9, anawafikia zaidi ya wafuasi milioni 50 kila siku. Kwa hiyo, katika karibu miaka 8 ya upapa wake, Papa mstaafu Benedikto XVI aliwasiliana kwa kutumia njia mbalimbali za mawasiliano kwa ubunifu na ujasiri. Baadaye, katika karibu miaka 10 kama Papa Mstaafu, mawasiliano yake yalichukua sura tofauti, isiyoonekana lakini yenye ufanisi zaidi kwenye ukimya na sala.