Papa:Dini zote pamoja zisali kwa ajili ya mama Ukraine anayeumwa sasa
Na Angella Rwezaula;- Vatican.
Hakuna Mkraine Myahudi, Mkraine wa Kikristo, Mkraine wa Kiorthodox, Mkraine wa Kikatoliki Mkraine wa Kiislamu. Hakuna, kwa sababu kuna Mkraine mmoja, ‘mama’ tu ambaye anaumwa, anateseka kwa kuona unyama uliofanyiwa watoto wake kwa takriban mwaka mmoja. Kutokana na ‘mama’ huyo Papa ameomba sala, huku akihakikishia mawazo ya kudumu na ukaribu wake kwamba wasiwe na shaka kwa sababu anawabeba moyoni mwake na anamwomba Mungu awahurumie watu hao wajasiri. Baba Mtakatifu Francisko alieleza mawazo hayo asubuhi Jumatano tarehe 25 Januari 2023, kwa ujumbe kutoka Baraza la Makanisa na Mashirika ya Kidini ya Kiukreni, aliokutana nao kabla ya katekesi yake, ambapo pia mara baada ya katekesi wakati wa kutoa salamu, aliwasalimia na kuwaomba waamini wasali pamoja kwa ajili ya amani ya uhakika katika mateso ya nchi hiyo.
Safari ya mkutano Roma
Mkutano wa wajumbe wa kidini hao jijini Roma ulianza tangu tarehe 24 Januari na utahitimishwa 26 Januari 2023. Hata hivyo wajumbe hao mbali mbali watashiriki katika Masifu ya jioni katika Siku kuu ya Uongofu wa Mtakatifu Paulo, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta, ambapo Papa Francisko ataongoza masifu hayo, sambamba na kufunga Juma la Kuombea Umoja wa Kikristo lililoanza tarehe 18 -25 Januari ambapo madhehebu mbali mbali yatashiri. Hata hivyo tarehe 24 Januari 2023, wajumbe kutoka Ukraine walikutana na wakuu wa baadhi ya Mabaraza ya Kipapa likiwemo Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini na la Mawasiliano. Katika mkutano pamoja na Papa kwenye Ukumbi mdogo wa Paulo VI, katika fursa ziara ya Baraza hilo walikuwapo pamoja wengine Askofu mkuu Sviatoslav Shevchuk, Padre na Mkuu wa Kanisa la Kigiriki-Katoliki, lakini pia Askofu wa Kilatini Vytaly Kryvyc'kyi wa Kyiv, pamoja na wawakilishi wa Kanisa la Kiorthodox la Ukraine, Makanisa ya Kitume ya Kiarmenia na Kilutheri, jumuiya za Wayahudi na Waislamu;pia pamoja na Jumuiya ya Biblia, ambayo ni ya madhehebu mbalimbali.
Mfano wa majadiliano
Ujumbe huo ulikuwa ni kikeleza kikubwa cha mazungumzo na kuishi pamoja kwa amani ambao Papa Francisko ameweza kufafanua. Katika miezi hii ya vita, Baraza la Kiukrene limekuwa likifanya mipango ya kawaida, ikiwa ni pamoja na matamko ya umma na kuingilia kati katika maeneo yenye migogoro, tangu 2015. Na zaidi katika miezi ya hivi karibuni, wajumbe wa Baraza hilo pia walikuwa wametuma barua kwa Papa. Kwa maana hiyo Papa akizungumza bila maandiko amesisitiza kuwa hilo kwake ni neema ya Mungu na kwamba ya kuamua juu ya mipango hiyo yote na kuendeleza pamoja, kama ndugu. Huu ni ushuhuda thabiti wa amani katika nchi inayokumbwa na vita, alisisitiza Papa Francisko katika hotuba aliyowakabidhi. Hatua yao, iliyofanywa kuwa imara na ujasiri, ambayo inajiandaa vyema kwa ajili ya kesho ya amani, ambayo hatimaye maslahi ya kiuchumi na kisiasa ambayo yanaleta vita, yatatoa nafasi kwa ajili ya manufaa ya watu wote. Papa Francisko aidha amesema anavyoomba hilo kila siku. “Mimi nipo pamoja nanyi katika kutetea haki za waamini wa kila jumuiya ya kidini, hasa wale wanaoteswa na kuteseka”, amebainisha katika hotuba yake aliyokabidhi.
Kila mmoja apate kuzungumza
Papa Francisko hata hivyo alipendelea kuweka kando maandishi yaliyotayarishwa na sio tu kwa sababu alivyosema kwamba: “sisi ni watumwa wa kizuizi cha wakati”, ikizingatiwa kwamba saa 3.00–5.00, alikuwa lazima awepo tayari kuanza katekesi ambayo waamini wasingeweza kungojea, lakini pia kwa sababu mapenzi yake yalikuwa kutaka kusikiliza kila mtu aliyekuwepo hapo akizungumza. Kwa hakika Papa aliwaomba kila mtu azungumze kwa kifupi na kwamba: “Samahani, ningekaa nanyi asubuhi yote lakini sisi pia ni watumwa wa wakati”.
Kuwasiliana na serikali na wajumbe wa idadi ya watu
Katika hotuba yake fupi bila kusoma, Papa Francisko alibainisha kwa mara nyingine kwamba yeye yuko karibu nao na kueleza kwamba yeye anapokea mara kwa mara wajumbe kutoka kwa Rais Volodymyr Zelensky na kwamba yuko katika mazungumzo na wawakilishi wa watu wa Ukraine. Hiyo inamruhusu kuwasikia na kusali kwa ajili yao. Amewashukuru umoja huo na kwamba ni jambo kubwa kwake, kama watoto wa familia ambao wako mmoja, mmoja mbali, lakini ‘mama’ yao akiwa mgonjwa (wao) wote wanakuwa pamoja. Haijalishi sana kuhusu Ukraine wa Kiyahudi, Ukraine wa Kikristo, Ukraine wa Kiorthodox, Ukraine wa Kikatoliki, Ukraine wa Kiislamu... hapana! Nia ya Ukraine ni kama ‘’mama Ukraine na wote kwa pamoja! Na hiyo inaonesha muundo wa rangi yao. Ni mfano mbele ya mambo mengi ya juu juu ambayo yanaonekana katika utamaduni wetu.
Ukraribu wa Papa kwa Ukraine
Ukaribu wa Papa Francisko kwa Ukraine una mizizi kutoka mbali, kwani amesimulia tangu alipokuwa mtoto na huko Buenos Aires alihudumia Misa kwa Padre Stefano wa Ukraine. Kwa hiyo anajua historia yao na akimwonesha Askofu Mkuu Shevchuk, ambaye kwa miaka mitatu alikuwa msaidizi wa Mtakatifu Maria wa ukraine katika mji mkuu wa Argentina. Pamoja na Padre Stefano, Papa wa baadaye amesisitiza kwamba alijifunza kutumikia Misa ya kiukraine na kusema: “Nilikuwa na umri wa miaka 11 na kutoka wakati huo huruma yangu na Ukraine ilianza kukua. Ni huruma ya zamani ambayo imekua na hii inanileta kuwa karibu na ninyi.” “Msiwe na shaka! Nina waombea! Papa baadaye aliwahakikishia kwamba: “Ninawabeba moyoni mwangu na ninamwomba Mungu awahurumie watu hawa wajasiri. Asante kwa ziara hii, asante!
Wito wake kwa waamini kusali kwa ajili ya Ukraine
Mwishoni mwa mkutano huo, kabla ya kuhamia katika Ukumbi wa Paulo VI, Baba Mtakatifu Francisko aliwasihi kila mmoja “kusali kwa ukimya, kila mmoja kwa namna yake, yaani kwa namna yake ya kusali, kwa ukimya lakini kwa pamoja kwa ajili ya ‘mama Ukraine”. Ombi lile lile lililotolewa kwa waamini na mahujaji kutoka pande zote za dunia waliounganika katika Ukumbi wa Paulo VI, mwishoni mwa katekesi yake. Kwamba: “ Ukraine iliyopigwa, ambayo inateseka sana, isikose katika mawazo na sala zetu”. Vile vile Papa akiwa katika katesi amesema jinsi ambavyo kabla yake alikutana na viongozi wa madhehebu mbali ya dini kutoka nchini Ukraine ambao waliweza kumwambia maumivu ya watu wao. Kwa hiyo alipyaisha wito wake kwamba wasisahau kamwe kila siku kusali kwa ajili ya uhakika nchini Ukraine.