Januari 22:Papa ataadhimisha Misa ya Dominika ya Neno la Mungu
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko anatarajia kuadhimisha misa katika Dominika ya Nne ya Neno la Mungu mnamo tarehe 22 Januari 2023 katika siku ambayo aliianzisha mnamo tarehe 30 Septemba 2019. Kauli mbiu ya toleo la mwaka huu limetolewa katika kifungu cha barua ya kwanza ya Yohane kisemacho: “Tunawatangazia ninyi tuliyoyaona” (1 Yoh 1, 3). Kwa maana hiyo majira ya saa 9.30 asubuhi ya Ulaya, Dominika ijayo, Baba Mtakatifu ataongoza maadhimisho hayo katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican na katika lengo la kufufua wajibu walio nao waamini katika maarifa ya Maandiko Matakatifu, atawakabidhi wale watakaohudhuria Injili ya Mtakatifu Mathayo. Wakati wa maadhimisho hayo, hata hivyo Huduma ya usomaji itakabidhiwa kwa wanaume na wanawake hasa watu watatu na wengine saba huduma ya Makatekista. Ni waamini walei wanaokusudia kuwawakilisha Watu wa Mungu na wanatoka nchini Italia, Congo DRC, Ufilipino, Mexico na Wales
Msaada wa kiliturujia wa kichungaji kwa ajili ya kuliishi Neno la Mungu
Tukio hilo litaoneshwa moja kwa moja na Vyombo vya Habari vya Vatican na litatangazwa katika tovuti zote za Vatican News na moja kwa moja na vituo vikuu vya televisheni duniani. Nchini Italia, miongoni mwa zingine ni Televisheni ya Taifa (Rai) na Televisheni ya Baraza la Maaskofu Italia (Tv2000). Sehemu ya Maswali Msingi ya Uinjilishaji katika Ulimwengu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji iliyopewa dhamana na Papa kwa kuendeleza tukio hilo, limetoa msaada wa mwongozo wa kiliturujia na kichungaji muhimu kwa ajili ya kuishi Neno la Mungu katika jumuiya, katika familia na binafsi.
Mwongozo unapatikana kwenye mtandao
Mwongozo huo unapatikana kwa lugha ya Kiitaliano katika toleo la karatasi, iliyochapishwa na Toleo la Shalom na kwa lugha za Kiingereza, Kihispania, Kireno na Kifaransa unapakuliwa mtandaoni kwenye tovuti: www.evangelizatio.va, katika muundo wa dijitali. Ni chombo kinachotoa hatua za kuhimiza kukutana kwa kina na Neno la Mungu katika jumuiya, katika familia, katika maisha ya kila siku,na pia inajumuisha makala, tafakari, maandiko kuhusu Kuabudu, shughuli za watoto na mapendekezo ya kichungaji.
Mfululizo wa vitabu vidogo kuhusu ‘Dei Verbum’
'Dominika ya Neno la Mungu' inataka kuweka nuru ya uwepo wa Bwana katika maisha ya watu. Kiukweli tayari anatembea pamoja nasi na yuko kwa njia ya Neno lake, kama inavyooneshwa katika nembo ya Dominika iliyoongozwa na historia ya Biblia ya Wanafunzi wa Emau, katika safari yao, ili kufuatilia tena Maandiko pamoja na Bwana, akiruhusu mwenyewe kufundishwa na kuangazwa. Kwa maana hiyo ili kujiandaa kwa Jubilei ya 2025, Papa Francisko aliwataka waamini kusoma tena hati nne za Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican. Baraza la Kipapa la Uinjilishaji limeamua kuunda mfululizo wa vitabu vidogo vidogo katika mfululizo mmoja wenye kichwa: “Quaderni del Concilio”, yaani “Daftari za Mtaguso, vilivyotolewa katika maduka ya vitabu na maduka ya mtandaoni tarehe 8 Desemba 2022. Katika fursa ya Dominika ya Neno la Mungu, kwa hiyo linapendekeza usomaji kwa upya wa Dei Verbum pia kupitia vitabu vidogo vitano vya kwanza vya mfululizo vilivyotolewa kwa usahihi kuhusu hati hiyo ya Mtaguso.