Papa amefika DRC kuanza ziara 40 ya kitume&ya tano barani Afrika!
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Hatimaye Jumanne tarehe 31 Januari 2023, kile mabacho tulikitazamia kwa siku nyingi, kimetimia! Hata Baba Mtakatifu Francisko Dominika tarehe 29 Januari 2023 alikuwa amewaomba waamini kusali kwa ajili ya ziara hiyo. Papa alibainisha kuwa: "Ni muda mrefu ninasubiri kutembelea Nchi hizo mbili ambazo zimo ndano ya moyo wangu kwa namna ya pekee na ambapo ninatarajia kwenda kama muhujaji wa amani na upatanisho. Ardhi zile, zilizoko katikati ya Bara kubwa la Kiafrika, zimejaribiwa kwa muda mrefu na mizozo: Mfano Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inateseka hasa huko Mashariki mwa nchi na mivutano ya kisilaha na kwa unyonyaji; wakati huo huo Suda Kusini, inasumbuliwa kwa miaka na vita, hawaoni wakati vurugu hizo zinaisha ambazo zimesaabisha watu wengi kuishi wamerundikana na hali ngumu sana”.
Ndege ya Shirik la Ndege ITa iliyomsafirisha Papa iliondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Fiumicino Roma saa 2:29 asubuhi kwa saa za Ulaya, Jumanne asubuhi, ikiwa imebeba hata waandishi wa habari 70 kutoka mataifa mbali mbali na ambao aliweza kuzungumza nao na kuwasalimia huku akiwaomba wawaombee hata wahamiaja ambao wanakatisha jangwa la Sahara, wakiwa katika matazamio ya kutafuta hali bora. Baba Mtakatifu analitembelea taifa hilo kwa mara ya kwanza kuanzia tarehe 31 Januari hadi 3 Februari 203, kwa kufuata nyayo za Baba Mtakatifu Yohane Paulo II, aliyeitembelea nchi hiyo mnamo mwaka 1980 na 1985, na hivyo ni baada ya miaka 37.
Ziara ya Papa Francisko katika mataifa ya Afrika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Sudan Kusini inafikisha ziara za kitume 40 za nje ya nchi na ikiwa ni kwa mara ya tano, anakwenda barani Afrika. Kama ratiba inavyoonesha mara baada ya kufikia kuna: ziara ya heshima kwa Rais Felix Tshisekedi na kuhutubia mamlaka ya nchi, mashirika ya kiraia na mashirika ya kidiplomasia. Na tarehe 3 hadi 5 atakuwa Sudan Kusini katika mji mkuu wake Juba.
Katika kukamilika ziara yake ya kitume mnamo Dominika tarehe 5 Februari akiwa barani Afrika, atakuwa ametembelea nchi 60 tangu kuanza utume wa kiti ha upapa. Ikumbukwe kwamba ilikuwa ni mnamo mwaka 2015, alipokwenda Kenya, Uganda na Jamhuri ya Afrika ya Kati, na mnamo mwaka 2017 alitembelea nchi ya Misri. Baadaye mnamo mwezi Machi 2019, alifanya ziara yake ya Kitume nchini Morocco, na baadaye Msumbiji, Madagascar na Mauritius mnamo mwezi Septemba 2019.