Tafuta

Maneno yake ya Mwisho ya Papa Benedikto XVI: "Bwana ninakupenda". Maneno yake ya Mwisho ya Papa Benedikto XVI: "Bwana ninakupenda". 

Maneno ya mwisho ya Papa Benedikto XVI:“Bwana ninakupenda”

Askofu Gänswein amesimulia kile ambacho Papa Mstaafu alisema usiku ule kabla ya saa yake ya kufa.Ni hasa hutafutaji wa Yesu mpendwa,ambayo ilikuwa ndiyo huduma ya kikuhani ya Joseph Ratzinger,kwa hakika na kama alivyokuwa amekumbusha Papa Francisko mnamo 2016.

ANDREA TORNIELLI

Maneno ya mwisho ya Papa Mstaafu Benedikto XVI yamekusanywa katika  moyo wa usiku ule na muuguzi wake wa karibu sana. Ilikuwa saa 9 za mkesha wa tarehe 31 Desemba 2022, masaa machache kabla ya kifo chake. Ratzinger muda huo alikuwa bado hajaingia kwenye mateso, na wakati huo wahudumu wake na wote waliokuwa wanamsaidia walikuwa wanabadilisha zamu. Katika wakati huo muhimu hasa kulikuwako na muuguzi ambaye hajuhi kijerumani. Kwa njia hiyo akizungumza Katibu wake Askofu Georg Gänswein muda baada ya kifo,  alisema kwamba: “Benedikito XVI kwa sauti ya chini kabisa lakini ambayo ilieleweka alisema kwa kiitaliano maneno haya: ‘Signore ti amo!’ yaani “Bwana ninakupenda”. Hayo ndiyo yalikuwa maneno yake ya mwisho yaliyokuwa yanaeleweka, kwa sababu baadaye hakuwa tena na uwezo wa kujieleza”.

“Signore ti amo!” yaani, “Bwana ninakupenda” kwa hiyo ni ufupisho wa maisha ya Joseph Ratzinger, ambayo kwa miaka mingi alikuwa anajiandalia wakati wake wa mwisho wa kukutana uso kwa uso na Muumba wake. Mnamo tarehe 28 Juni 2016, katika mwaka wake wa 65 wa kikuhani wa mfuasi wake Mstaafu, Papa Francisko, alikuwa amependa kusisitizia jambo msingi kuhusu  maisha yake marefu kihistoria ya ukuhani wa Ratzinger aliyokuwa amesistiza kwamba: “Katika kurasa nyingi ambazo amejikita katika ukuhani, alikuwa akisisitiza kama ile saa ambayo ni ya wito wa mwisho wa Simoni,  ambapo Yesu kwa kumtazama kiukweli alimuomba jambo moja:  “ Je unanipenda? Ni jinsi gani ilivyo nzuri na kweli hiyo! Kwa sababu katika neno  unanipenda? Ndiyo anataka kueleza jambo moja ambalo Bwana anaanzisha uchungaji, kwa sababu pakiwepo na upendo tu kwa ajili ya Bwana ndipo Yeye anaweza kuchunga kupitia kwetu… “Bwana, wewe unajua, yote, wewe unajua kuwa ninakupenda.”

Papa Francisko aidha alikuwa amesema kwamba: “hili ndilo neno ambalo linatawala maisha yote aliyotumia katika huduma ya upadre na taalimungu, ambayo kwake yeye, si kwa bahati, aliifafanua kuwa  ya 'kutafuta mpendwa'; hili ndilo aliloshuhudia daima na bado anashuhudia leo hii: kwamba ni jambo la kuamua hata katika siku zetu, ziwe za jua au za mvua, na kitu pekee ambacho kila kitu kingine pia kinakuja, ni kwamba Bwana yupo kweli na kwamba tunamtamani, kwamba kwa kina tuko karibu Naye, kwamba tunampenda, na kwamba tunamwamini kweli kwa undani na kwa kuamini kwamba tunampenda Yeye kweli. Upendo huu ndio unaoijaza mioyo yetu kweli, kuamini huku ndiko kunatufanya tutembee salama na utulivu juu ya maji, hata katikati ya dhoruba, kama ilivyotokea kwa Petro”.

MANENO YA MWISHO YA PAPA MSTAAFU BENEDIKTO XVI
02 January 2023, 10:24