Tafuta

2023.01.31 Papa kabla ya kuondoka amesali katika mnara wa wahanga wa KIndu huko Fiumicino 2023.01.31 Papa kabla ya kuondoka amesali katika mnara wa wahanga wa KIndu huko Fiumicino  (Vatican Media)

Kinshasa:Ni kivumbi na jasho kumpokea Papa,Balestrero,ni faraja kwa watu!

Mabango,na bendera za"Bienvenue Pape François”kwenye mitaa ya Kinshasa ili kusherehekea kuwasili kwa Baba Mtakatifu katika ardhi ya Congo.Kwa siku hizi wanawake na wanaume wamekuwa wakijishughulisha na maandalizi bila kikomo ya kumkaribisha Papa baadaya ya miaka 37 tangu Yohane Paulo II.Askofu Mkuu Balestrero:Mto wa chuki unapita ndani ya bahari ya haki na upatanisho.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Hatimaye Ziara iliyotarajiwa kwa muda mrefu imeanza asubuhi Jumanne tarehe 31 Januari 2023 ambapo Papa Francisko ameondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Fiumicino saa 2.29 asubuhi na shirika la Ndege la Ita ambapo anatarajia kutua katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mida ya saa 9.00 alasiri. Papa hatimaye ameanza ziara yake ya 40 ya  kitume ambapo kwanza ni mji mkuu Kinshasa DRC  na baadaye  huko Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini kuanzia tarehe 3-5 Februari 2023. Hata hivyo kwa mujibu wa waandishi wa habari wa  Vatican News, walioko tayari Kinshasa, wanatuhabarisha kile kinachoendelea kwa kukutana na viongozi wa Kanisa, wenyeji na mazingira kwa ujumla

Ziara ya Kitume ya Papa Francisko huko DRC na Sudan Kusini imeanza 31 Januari

 

Kwa maana hiyo“Pape François engumba Kinshasa eyambi yo na esengo” ni miongoni mwa maneno yaliyoandikwa kwenye mabango ambapo katika mitaa yenye vumbi ya Kinshasa, iliyokandamizwa na malori ya rangi za manjano ambayo yanazuia kupita foleni  hata za wanawake na vikapu vya matunda vichwani mwao, taxi, pikipiki zilizo na abiria hata wanne, lakini  zaidi ya hayo yote uso wa Papa Francisko unaonekana kila mahali, ukiambatana na maneno ya “Bienvenue” yaani “Karibu”. Bendera, mabango zenye sura za Papa pamoja na za wanasiasa wa eneo hilo, lakini pia hata mabanda  ya ununuzi wa vitu yamejaa  bendera, fulana na vifaa vingine vya kusherehekea ujio wa Papa. Papa Francisko anatarajia kutua alasiri saa 9 hivyo katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Ni ziara inayaofuata baada ya miaka 37 tangu Mtakatifu Yohane Paulo II alipoitembelea nchi hiyo. Na hii kwa maana hiyo ndiyo ziara ya kwanza ya mwaka 2023 ya Papa Francisko na ambayo itaendelea Sudan Kusini, iliyotarajiwa na Papa kwa muda mrefu iliyokuwa imepangwa mwezi Julai 2022 ikaahirishwa kwa sababu za kiafya.

Mahali ambapo Papa ataadhimisha Misa tarehe 1 Februari Congo DRC
Mahali ambapo Papa ataadhimisha Misa tarehe 1 Februari Congo DRC

Papa Francisko kwa maana hiyo ametimiza ahadi yake ya kwenda kutembelea idadi hii ya watu wapatao milioni 100, asilimia 49 kati yao wakiwa ni Wakatoliki, wanaokabiliwa na umaskini uliokithiri ambao unachukua sura ya maduka na masoko ya vyakula na nyumba zilizo zamishwa kwenye matope na uchafuzi unaofanywa na blanketi ambalo giza linapoingia, huiba rangi za kitongoji hicho cha jiji  kubwa la Afrika. Hata hivyo ni Mashariki  mwa nchi ambapo majeraha ya nchi hiyo yanavuja damu zaidi, na maslahi yake yanachukuliwa na  mataifa yenye nguvu duniani na vita na nchi jirani kuhusu madini na chuki za kikabila ambazo husambaratisha maisha ya watu.

Balozi wa Vatican nchini Jamhuri ya Congo DRC

Watu waliuawa alisema dereva wa Kikongo, ambaye, wakati wakizunguka kati ya magari yaliyojaa zaidi kuliko uwezo wao na wafanyabiashara wa mitaani wanaouza ndizi, chupa za maji, leso, fimbo za selfie na sigara,  aliwasindikiza wanahabari wa Vatican kutoka uwanja wa ndege wa Ndolo, mahali ambapo Papa ataadhimisha Misa Takatifu ambayo takriban watu milioni 2 wanatarajiwa kuwapo hadi manispaa ya Gomba. Katika eneo hilo la Kinshasa, linalochukuliwa kuwa katika wilaya ya mji mkuu, kuna makao makuu ya taasisi nyingi, ikiwa ni pamoja na Ubalozi wa Vatican. Ni Moja ya Ubalozi mkubwa zaidi barani Afrika, kwa maelezo,  kwa sababu wamesema kuwa lilikuwa, jengo la kikoloni lililopendekezwa, ambalo limezungukwa na hekta kadhaa za bustani, ambayo itakuwa makazi ya Papa wakati wa kukaa kwake katika jiji la Congo hadi 3 Februari 2023

Mkutano na waathirika: 'tayari kusamehe'

Moja ya matukio muhimu zaidi ya ziara yake Papa akiwa katika Ubalozi huo atakutana na waathirika wa ghasia wa sehemu ya mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ikifuatiwa na mazungumzo na watu wa kujitolea na shughuli za upendo.  Hao ni wawakilishi kutoka majimbo yaliyokumbwa na ghasia zaidi. “Tutasikia ushuhuda wa maisha halisi ambao unatoa kipimo cha ukweli wa nchi na tutaona watu ambao wameweka haya yote, lakini wako tayari kusamehe,” alisema hayo Askofu Mkuu Balestrero, ambaye ni Balozi nchini DRC na ambaye atakuwa pamoja na Papa wakati wote katika hatua za ziara yake huko  Kinshasa. “Kuna haja kubwa ya mto huu wa chuki na ghasia kuingia katika bahari kubwa, kama Mto Congo unavyofanya Bahari, ambayo ni ya haki, ambayo lazima ifanyike, lakini pia bahari ya upatanisho.” Alisisitiza Askofu mkuu wakati wa mahojinao na wawakilishi wa  Vatican News waliofika huko DRC mapema katika ujio wa Papa Francisko na walikutana katika ukumbi ambao mkutano huo utafanyika, uliopambwa tayari na bango na bendera, wakati familia ya ubalozini ilikuwa bado inapanga viti kwa ajili ya wageni mbalimbali.

Mkutano na wawakilishi wa kazi za upendo

Kwa hiyo baada ya waathirika, mahali pale pale  Papa Francisko pia atakutana na wawakilishi wa shughuli za upendo nchini humo, ambapo  tukio hili ni  hai na kwamba Kanisa lipo katika nyanja zote za maisha ya kijamii na kielimu, kwa mujibu wa Askofu Mkuu Balestrero.  “Asilimia 40 ya kazi za afya zinasimamiwa na wafanyakazi wa Kikatoliki. Takriban wanafunzi milioni 7 wanahudhuria shule za umma zinazoendeshwa na wahudumu wa dini ya Kikatoliki. Chini ya kukumbatiwa na Papa kutakuwa na walemavu, wenye ukoma, wagonjwa wa UKIMWI, viziwi, watoto walioachwa na hata watawa wa ndani kwa sababu sala ni aina ya juu sana ya upendo", alifafanua Askofu Mkuu Balestrero. Aidha “Kutakuwa na watoto vipofu ambao wataimba na wengine ambao wanasoma shule hapa Kinshasa na ambao wataripoti uzoefu wao, au tuseme kile ambacho wamepata kutoka kwa kazi za upendo za Kikatoliki ambazo wamefikiwa. Kwa hiyo tutagundua jinsi upendo hautangazwi tu bali unafanyiwa uzoefu na jinsi mwili wa Kristo ambao, kama Papa anavyotufundisha, ni watu hawa wote, unaguswa kweli, hutunzwa na kukaribishwa na watu wengi. Wakongo au kutoka nje wanaokuja kujitoa na kujitolea ni kwa ajili ya mateso ya nchi hii”.

Vijana washiriki katika maandalizi hayo

Askofu Mkuu Balestrero pia alitoa maoni yake juu ya matarajio ya ujio wa Papa Francisko,na maandalizi ambayo yamekuwa yakiendelea kwa wiki kadhaa ambayo yameowaona vijana sana vinginevyo alisema wanazunguka tu, kwenye vilabu na kasino au mitaani kutafuta kazi za hapo na pale na kazi za mchana. “Siyo kusubiri tena lakini ni nyuzinyuzi. Watu mitaani wanaimba wimbo uliotungwa hasa kwa ajili ya Papa, na kuna mabango ambayo yanaongezeka, waamini wengi wanawasili kutoka sehemu nyingine za Congo na kutoka nchi jirani”.

Faraja

Ukweli ni kwamba uwepo wa Papa ni faraja kubwa kwa nchi ya Congo, kwa sababu ni nchi inayoteseka, ni mwathirika wa vurugu nyingi na sasa, kwa angalau siku 3-4, atasikika Papa akimimina mafuta katika majeraha ambayo kwa bahati mbaya ni ya kina sana. Pia kuna furaha ya Balozi kuona  jumuiya ya Kikatoliki ambayo inataka kweli kumpa Mungu nafasi katika maisha yake, lakini ambayo inahitaji kupokea msukumo kutoka kwa Papa ili kuepuka mgawanyiko kati ya imani inayotangazwa na maisha. Ziara ya Papa inaweza kuwa, hakika na itakuwa hatua muhimu ya kupokea miongozo ya uinjilishaji bora zaidi na wa kina" alisisitiza.

Balozi wa Vatican nchini DRC aelezea ziara ya Papa
31 January 2023, 11:28