Tafuta

2023.01.05 Misa ya Mazishi ya Papa Benedikto XVI. 2023.01.05 Misa ya Mazishi ya Papa Benedikto XVI.  (Vatican Media) Tahariri

“Iangaze nuru ya Kristo,sio yako binafsi”

Katika moyo wa Mafundisho ya Ratzinger kuna uso wa Kanisa moja ambalo halitafuti nguvu,mafanikio na idadi kubwa.Na ufunguo wa"uinjilishaji mpya”.

Na Angella Rwezaula, - Vatican

Benedikto XVI alikufa akiwa amestaafu na akazikwa kama Papa. Bahari ya maombi iliamsindikiza na ibada ya mazishi iliyoongozwa na Papa Francisko katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Maombi ya shukrani ambayo yameinuliwa kwa Mungu  kutoka ulimwengu wote, kwa uhakika kwamba Joseph Ratzinger hatimaye anaweza kufurahia uso wa Bwana ambaye alimpenda na kumfuata katika maisha yake yote, na ambaye alitoa maneno yake ya mwisho kabla ya kuingia kwenye uchungu kwamba: “Bwana nakupenda!” Kuna sifa ya kipekee inayomuunganisha Benedikto XVI kwa mrithi wake na tunaweza kuipata katika maneno ambayo, hadi kufikia ujumbe wake wa kwanza wa Urbi et orbi, asubuhi ya siku iliyofuata ya uchaguzi, Papa Ratzinger alisema: “Katika kutekeleza majukumu ya huduma yake, Papa mpya anajua kwamba wake kazi ni kufanya nuru ya Kristo iangaze mbele ya wanaume na wanawake wa siku hizi: sio nuru binafsi, bali ile ya Kristo.” Sio nuru ya mtu binafsi, umbele, umbele, mawazo ya mtu, ladha ya mtu, lakini katika mwanga wa Kristo. Kwa sababu, kama vile Benedict XVI alivyosema, “Kanisa si Kanisa letu, bali ni Kanisa lake, Kanisa la Mungu. Mtumishi lazima kutambua jinsi alivyosimamia mema ambayo amekabidhiwa. Hatuwafungi watu kwetu, hatutafuti nguvu, heshima, upendeleo wa sisi wenyewe. Inafurahisha kuona jinsi ambavyo tayari kama kadinali, kwa miaka mingi, Ratzinger alikuwa ameonya Kanisa juu ya ugonjwa ambao umelisumbua na bado unalitesa: l kuamini miundo, katika mpangilio. Hiyo ya kutaka “kuhesabu” kwenye ulimwengu ili kuonekana zaidi”.

Mnamo Mei 2010 huko Fatima, Benedict XVI aliwaambia maaskofu wa Ureno: “Wakati, kwa maoni ya wengi, imani ya Kikatoliki sio tena urithi wa kawaida wa jamii na, mara nyingi, inaonekana kama mbegu iliyopunguzwa na kufunikwa na 'miungu' na mabwana wa dunia hii, itakuwa vigumu sana kwake kugusa mioyo kupitia hotuba rahisi au mwaliko wa maadili na hata kidogo kupitia mwaliko wa jumla wa maadili ya Kikristo”. Kwa sababu “kauli ya ujumbe huo uliotangazwa haifikii undani wa moyo wa mtu, haigusi uhuru wake, haibadilishi maisha yake. Kinachovutia zaidi ya yote ni kukutana na waamini ambao, kwa imani yao, wanavutia kwenye neema ya Kristo, wakimshuhudia.” Si hotuba, hoja kuu au mareje mahiri ya maadili yanayogusa mioyo ya wanawake na wanaume wa leo hii”. Haihitajiki mikakati ya utume w masomo ya  kidini na wa kugeuza watu imani. Wala Kanisa la leo haliwezi kufikiria kuishi katika kujutia yaliyopita kwa umuhimu na nguvu liliyokuwa nayo hapo awali. Kinyume chake kabisa,  wote wawili Benedikto  XVI wa na mrithi wake Papa Fransisko wamehubiri na kushuhudia umuhimu wa kurejea mambo muhimu, kwa Kanisa lenye utajiri tu katika mwanga ambao linaupokea kwa uhuru kutoka kwa Bwana wake.

Na hasa pale kwa  kurudi huku katika muhimu ndio ufunguo wa  utume. Joseph Ratzinger alisema hayo alipokuwa bado Mwenyeketi wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzau ya Kanisa, wakati wa katekesi mnamo Desemba 2000, ambayo ilinukuliwa hivi karibuni na Gianni Valente, mkurugenzi wa Shirika la Habari za Kimisionari (FIDES). Ratzinger alianza kutoka kwenye msukumo wa mfano wa kiinjili wa Ufalme wa Mungu, ukilinganishwa na Yesu na mbegu ya haradali, ambayo “ni ndogo kuliko mbegu zote lakini, mara tu inapokua, ni kubwa kuliko mimea mingine katika bustani na kuwa mti.” Alieleza kwamba akizungumzia “uinjilishaji mpya” katika jamii zisizo za kidini ilikuwa ni lazima kuepuka “kishawishi cha kukosa subira, kishawishi cha kutafuta mafanikio makubwa mara moja, kutafuta idadi kubwa”. Kwa sababu hiyo  “siyo mbinu ya Mungu”. Uinjilishaji mpya, aliongeza, “hauwezi kumaanisha: kuvutia umati mkubwa mara moja ambao wamejitenga na Kanisa kwa mbinu mpya, zilizosafishwa zaidi”. Historia ya Kanisa lenyewe, kwa mujibu wa Kardinali Ratzinger alibanisha kuwa inafundisha kwamba “mambo makubwa daima huanza na nafaka ndogo na harakati za molekuli ni za kudumu”. Kwa sababu Mungu “hahesabu kwa wingi; na nguvu ya nje sio ishara ya uwepo wake.

Mengi ya mifano ya Yesu huonesha muundo huu wa utendaji wa kimungu na hivyo kujibu mahangaiko ya wafuasi, ambao walitarajia mafanikio zaidi na ishara kutoka kwa Masiha, mafanikio ya aina ambayo Shetani alitoa kwa Bwana. Wakristo, Benedikto XVI wa baadaye alikumbusha kuwa “Wa, walikuwa jumuiya ndogo ndogo zilizotawanywa ulimwenguni pote, zisizo na maana kulingana na vigezo vya kilimwengu. Kiuhalisia walikuwa ni vijidudu vinavyopenya kwenye unga kutoka ndani na walibeba ndani yao mustakabali wa dunia”. Kwa hiyo, si suala la “kupanua nafasi” za Kanisa ulimwenguni: “Hatutafuti kujisikiliza wenyewe, hatutaki kuongeza nguvu na upanuzi wa taasisi zetu, bali tunataka kutumikia mema ya watu na ubinadamu kwa kutoa nafasi kwa Yule ambaye ni Maisha. Kujifua huku kwa nafsi ya mtu katika kuitoa kwa Kristo kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, ndiyo hali  kimsingi ya kujitolea kwa dhati kwa Injili”.

Ufahamu huu ndio umesindikiza Mkristo, mtaalimungu, askofu na Papa Benedikto XVI wkatika kipindi chote cha uhai wake. Ufahamu unaorejea katika nukuu ambayo mrithi wake na ambaye kila mara alimhakikishia “heshima na utii”, alitaka kujumuisha katika mahubiri yake kwenye mazishi. Imechukuliwa kutoka katika “Kanuni ya Kichungaji” ya Mtakatifu Gregory Mkuu: “Katikati ya dhoruba za maisha yangu, ninafarijiwa na imani kwamba utaniweka juu ya meza ya maombi yako, na kwamba, ikiwa uzito wa makosa yangu unaniangusha na kunifedhehesha, utanikopesha msaada wa sifa zako ili kuniamsha”. “Ni ufahamu wa Mchungaji, amettoa maoni Papa Francisko kwamba hawezi kubeba peke yake kile, ambacho kiukweli, hawezi kamwe kustahimili peke yake na, kwa hiyo, anajua jinsi ya kujikabidhi  mwenyewe katika sala na huduma ya watu waliokabidhiwa kwake.” Kwa sababu bila Yeye, bila Bwana, hatuwezi kufanya lolote”.

05 January 2023, 17:21