Tafuta

Mazishi ya Papa Mstaafu yatafanyika tarehe 5 Januari. Mazishi ya Papa Mstaafu yatafanyika tarehe 5 Januari.  (ANSA)

Ratzinger na imani kama mchakato wa safari

Benedikto XVI shuhuda na Mwalimu wa majadiliano na wote!

ANDREA TORNIELLI

Ikiwa kuna mtaalimungu  na Papa ambaye katika maisha yake yote alitafakari na kufundisha juu ya usawaziko wa imani, alikuwa ni Joseph Ratzinger. Si kwa bahati mbaya  kwamba yeye pia alizungumzia juu yake katika mistari ya mwisho kuhusu wosia wake wa   kirohon ,ambao ulitolewa  siku ya kifo chake: “Nimeona na ninaendelea kuona jinsi usawaziko wa imani umetokea na unaibuka tena kutoka kwenye mkanganyiko huo. Yesu Kristo ndiye njia, ukweli, na uzima  na Kanisa, pamoja na mapungufu yake yote, ni mwili wake.”

Mwili wa Papa Benedikto XVI katika Kanisa kuu la Mt. Petro
Mwili wa Papa Benedikto XVI katika Kanisa kuu la Mt. Petro

Walakini, msisitizo huu uliorudiwa haukumaanisha kamwe kwa Ratzinger, kupunguza imani katika “mfumo" wa kifalsafa, kwa usanifu wa mawazo, hadi orodha ya kanuni za maadili, na kuishia kusahau kwamba imani ya Kikristo ni kukutana na Mtu, kama sisi, kwa kusoma katika utangulizi wa Waraka wake wa  Deus caritas est. Katika mahojiano yaliyoandikwa na gazeti la kila mwezi la Ujerumani, la Herder Korrespondenz, lililochapishwa mnamo Julai 2021, Papa Mstaafu alisema: “ Mwamini  ni mtu anayejiuliza ... Kwa maana hii, wazo la 'kukimbia kwenye mafundisho safi' linaonekana kwangu, lisilo la kweli kabisa. Fundisho ambalo lingekuwapo tu kama aina ya hifadhi ya asili, iliyotenganishwa na ulimwengu wa kila siku wa imani na matakwa yake, lisingewakilisha kwa njia fulani kukana imani yenyewe. Fundisho lazima likue katika imani na kuanzia ndani yake na sio kando yake.

Papa: Tuungane sote kumshukuru Mungu kwa zawadi ya Benedikto XVI Katika sala ya Malaika wa Bwana, alimkubuka Papa  Francisko tena marehemu mtangulizi wake, kama alivyokuwa amefanya katika  Sala ya Kushukuru “Te Deum” na Misa ya asubuhi tarehe Mosi Januaro 2023. Jumanosi, muda mfupi baada ya kifo chake, Papa alikwenda huko. Na  tayari kama Kadinali, mnamo 2001, Papa Ratzinger alikuwa ametamka maneno yaliyo wazi kabisa ili asianguke katika upunguzaji huo wa imani, ambao unapaswa kupendekezwa tena leo hii kuhusu: “Asili ya imani kwamba sio  kuanzia wakati fulani ambapo mtu anaweza kusema: Ninayo, na wengine hawana... Imani inabaki kuwa mchakato wa safari”.

Waamini wakiheshimu Papa Mstaafu Benedikto XVI
Waamini wakiheshimu Papa Mstaafu Benedikto XVI

Katika kipindi chote cha maisha yetu, mchakato wa safari unabaki, na kwa hivyo imani inatishiwa kila wakati na iko hatarini. Na pia ni kiafya kwamba kwa njia hiyo inaepuka hatari ya kugeuka kuwa itikadi inayoweza kubadilishwa. Katika hatari ya kutufanya tuwe wagumu na kutufanya tushindwe kushiriki tafakari na mateso pamoja na ndugu ambaye ana mashaka na anajiuliza. Imani inaweza kukomaa tu kwa kiwango ambacho unastahimili na kuchukua jukumu la dhiki na nguvu ya kutoamini katika kila awamu ya kuwepo na hatimaye kuweza kuwa na nguvu tena katika enzi mpya.

Waamini wakiheshimu Mwili wa Papa Benedikto XVI
Waamini wakiheshimu Mwili wa Papa Benedikto XVI

Imani, kama vile alivyokumbusha Papa Benedikto XVI mwenyewe na kama anavyopenda kurudia  kusema Papa Francisko hupitishwa kwa mvuto tu na si kwa kugeuza imani au kulazimishwa. Mwamini sio yule ambaye “anamiliki” kitu ambacho anaweza “kusimamia”. Mkristo hatoi majibu yaliyowekwa tayari kueleza kila kitu kwa kila mtu. Mkristo anaweza kurudisha cheche fulani ya zawadi tu ambayo amepokea bila kustahili, na hii inapotokea ni kwa neema safi. Kwa hiyo anaitwa kumtafuta Mungu kwa mazungumzo na mtu yeyote, kwa kubeba mzigo wa mashaka na majeraha ya kuwepo kwa wale wasioamini, akiongozana na kila mtu, bila kujiona kuwa “amefika”. Joseph Ratzinger alikuwa shuhuda  na mwalimu katika hili pia.

Ushuhuda wa Papa Benedikto XVI
02 January 2023, 16:47