Papa:Wafanyakazi Wakristo lazima wafungue milango wazi katika jumuiya za Kanisa
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wanachama wa Harakati ya Kikristo ya wafanyakazi , Ijumaa tarehe 9 Desema 2022 mjini Vatican, ameshukuru kufika kwao na kwamba miaka 50 iliyopita walianza hatua ya kwanza kwa kupewa baraka na Mtakatifu Paulo VI. Leo hii wamefika kushirikushana kumbukizi hilo kwa shukrani. Amewashukuru kwa wema ambao wamepanda kwa miaka hii ya maisha ya chama hicho. Aidha jitihada ambazo wamejikita nazo katika huduma kwa Jamii ya Italia kwa njia ya shughuli za mafunzo, vilabu, umakini kwa ulimwengu wa kazi katika nyanja mbalimbali na utumishi wa umma. Miaka hamsini pia ni kipindi cha kutazama uhalisia wa historia binafsi ambazo zinajikita katika kujitolea kwao sana; na hata ugumu katika ushuhuda wa kikristo. Ni muhimu kutojachia katika mitindo ya kujisifia, lakini kwa kuwa na utambuzi wa matendo katika Roho Mtakatifu, kati ya mikunyato ya historia zao, na sio katika matukio ya kustaajabisha, lakini zaidi ile ya unyenyekevu na kila siku. Katika kumbukizi hilo, Papa amesema linaweza kuwasaidia kutembea katika mielekeo miwili: kazi ya kujitakasa na upandaji wa mbegu kwa upya.
Papa Francisko akufafanua mielekeo hiyo miwili amesema, kujitakasa daima ni kwa lazima katika zoefu zote za kibinadamu. Sisi ni wadhambi na tunahitaji huruma kama vile kuwa na hewa safi tunayoivuta. Uwezekano wa kuongoka, na kujitakasa ni ishara ya ujasiri, ya nguvu na sio udhaifu. Hii ni njia ya kukaribisha mapya ya roho bila kuweka vizingiti, kuhusu vijana ili wapate nafasi, ambayo inalindwa na kushirikishwa na roho wa bure, kiasi kwamba mpango wa mwanzo haupotei katika kupendelea chaguzi za kutia moyo ambazo hazisaidii kupata mambo mapya ya nyakati. Wao ni Harakati ambayo ilinzishwa baada ya Mtaguso wa Pili II na hivyo wanaweza kusimulia matunda ya kipindi kile cha Kikanisa na kijamii. Papa amewatia moyo wapate shauku ya mwanzo, inayoonekana na ambayo wanaishi na uhusiano wa kikanisa katika maeneo na katika huduma ya bure ya mahitaji ya wafanyakazi. Mtaguso ulitoa mwaliko wa kusoma alama za nyakati, na hasa ulitoa mfano, kwa maana hiyo, kwa utambuzi wa maendeleo ya kijammi wanaweza kujiuliza ikiwa wao ni waaminifu katika huduma ya wafanyakazi leo hii? Jinsi gani ya kuuisha jitihada ya uongofu kiikolojia na utakaso? Jinsi gani ya kuuisha jamii ya Italia katika nyaja ya kiuchumi, kisiasa, kikazi kwa kutoa mchango wa kufanya maamuzi na mantiki ya ikolojia fungamani na udugu?
Kwa maana hiyo amesisitiza kuwa hiyo ndio sababu ya kupanda upya mbegu ambayo inawasubiri. Wakati wanasheherekea kumbukizi hilo wanapaswa kutazama mbele. Kiukweli sio kipindi cha kuvuna matunda tu, lakini ni kipidi cha kupanda kwa upya. Hali hiyo inaeleweka katika vipindi vigumu tunavyoishi. Papa Francisko amesema ni janga la uviko na vita ambavyo vimesababisha hali ya kijamii kuwa nyeusi na ngumu. Hali hiyo inawaalika kuwa wapandaji wa matumaini. Kwa kuanzia na wao binafsi, muhimili mzima wa chama, ambacho katika milango yao inapaswa iwe wazi; na kwamba vijana wasihis kuwa wageni tu, lakini kama kuwa mstari wa mbele kwa uwezo wao wa ubunifu wa kuwazia jamii tofauti. Papa amependa kupendekeza jitihada maalum juu ya mada kazi. Wao ni Harakati ya wafanyakazi na wanaweza kusaidia kupeleka wasiwasi wao ndani ya jumuiya ya Kikristo. Ni muhimu wafanyakazi wawe nyumbani katika parokia, vyama, vikundi na harakati, kiasi kwamba matatizo yao yachukuliwe kwa uzito; ili wito wao wa mshikamano usikike. Kiukweli, kazi inapitia awamu ya mabadiliko ambayo lazima yasindikizwe. Kutokuwa na usawa wa kijamii, aina za utumwa na unyonyaji, umaskini wa familia kutokana na ukosefu wa kazi au kazi yenye malipo duni ni hali halisi inayopaswa kusikilizwa katika mazingira yote ya kikanisa. Papa amewasihi kuweka hilo akili na moyoni mwao wazi kwa wafanyakazi, hasa maskini na wasio na ulinzi; kwa kutoa sauti kwa wasio na sauti; si kuhangaikia sana wanachama wao peke yao , bali kuwa chachu katika mfumo wa kijamii wa nchi, chachu ya haki na mshikamano.
Kutoka katika mfano wa Injili wa watenda kazi walioitwa kwa saa tofauti za siku (rej. Mt 20:1-16) Papa amesema tunajifunza kwamba kila msimu wa historia, kama kila saa ya siku, ni wakati mwafaka wa kutoa mchango wa mtu na kujaribu kutoa jibu. Hakuna mtu anayepaswa kuhisi ameachwa bila kazi. Kwa maana hiyo wao wasikose dhamira yao ya kuhamasisha kazi za wanawake, kuhimiza kuingia kwa vijana kazini, kwa mikataba ya heshima na sio ya njaa, kulinda wakati na nafasi ya kupumua kwa familia, kwa kujitolea na kwa utunzaji wa mahusiano. Katika hilo, Papa Papa Francisko amefafanua jinsi anavyojua kwamba wanarejea juu ya Mafundisho jamii ya Kanisa, kwa njia hiyo amewasihi wafanye tena ikiwezekana, na bora zaidi. Kanuni za mshikamano na usaidizi, zikiunganishwa kwa usahihi, ni msingi wa jamii inayojumuisha, na wala haimtupi mtu yeyote na inahimiza ushiriki. Bila kanuni hakuna mshikamano wa kweli, kwa sababu kuna hatari ya kutotoa sauti kwa uwezo, kwa vipaji vinavyostawi katika vyombo vya kati na katika Familia, vyama vya ushirika, biashara, ni nyenzo hai ya jamii.
Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwapa nafasi na sauti kunamaanisha kukomboa nguvu na manufaa ya wote ni matokeo ya kujitolea na mshikamano miongoni mwa yote. Waraka wa Frattelli tutti, “Shukrani kwa Mungu vyama vingi na mashirika ya asasi za kiraia yanasaidia kufidia udhaifu wa jumuiya ya kimataifa, ukosefu wake wa uratibu katika hali ngumu, ukosefu wake wa kuzingatia haki za msingi za binadamu na hali mbaya sana za baadhi ya makundi. Kwa hivyo kanuni ya usaidizi inapata usemi thabiti, ambao unahakikisha ushiriki na hatua ya jamii na mashirika ya kiwango cha chini, ambayo inakamilisha hatua ya serikali kwa njia inayosaidia”.(Ft 175). Papa ameongeza kusema kwamba vita ya tatu ya dunia ambayo inaendelea inatufanya kuwa na utambuzi wa upyaisho ambao unaanzia chini, mahali ambamo panaishi husiano na mshikamano na imani. Kwa njia hiyo wasiache kuibiwa na ujasiri wa mambo mapya ya upatanisho na udugu. Kwa kuhitimisha, Papa Francisko amewashukuru tena kufika kushehereka nusu karne ya kunzishwa kwa shughuli chama chao. Mtakatifu Yosefu awongoze daima kushi kazi na imani na upendo mkuu. Kwa moyo amewabariki wote na familia zao, na kuwatakia Noeli njema lakini wasisasaua kusali kwa ajili yake.