Papa:Uzito wa vita vya kinyama unaelemea watoto
Na Angella Rwezaula;– Vatican.
Uzito wa vita hii ya kinyama, ngumu sana iko kwenye mabega dhaifu ya watoto wa Kiukreni. Hebu tuwafikirie Noeli hii ambayo watoto wadogo na familia zao wataishi bila mwanga, bila joto. Hayo yamesema na Papa Francisko wakati wa kumaliza katekesi yake,Jumatano tarehe 21 Desemba 2022 akizungumza juu ya "Mungu aliyefanywa Mtoto ambaye Kanisa litaadhimisha wakati wa Noeli ambayo iko karibu kwenye milango yetu na hivyo, mawazo ya Papa Francisko yanakwenda moja kwa moja kwa watoto wa Ukraine wanaoteseka, sana kutokana na vita hivyo. Kama ilivyokuwa Jumatano iliyopita, ya katekesi pia katika hii , baada ya katekesi, Papa aliomba tena kutosahau wakati wa likizo nchi inayozidi kuharibiwa na watu wake.
Tufikirie watoto wa Ukraine
Papa amesema: “Katika sikukuu hii ya Mungu ambaye anakuwa mtoto, tufikirie watoto wa Kiukreni. Niliopowaona wengine hawa , lakini wao wengi hawawezi kutabasamu na mtoto anapopoteza uwezo wa kutabasamu ni mbaya. Watoto hawa wanabeba janga la vita ambalo ni la kinyama, gumu hivyo. Hebu tufikirie watu wa Ukraine Noeli hii, bila mwanga, bila joto, bila mambo muhimu ya kuishi", Papa Francisko anasisitiza. Tuombe Mungu alete amani haraka iwezekanavyo
Kiti kutupu cha meza kwa wakimbizi
Papa Francisko pia akitoa salma kwa Waponda, aliwakumbusha utamaduni wa kuacha kiti tupu mezani kwa ajili am geni asiyetarajiwa katika mkesha wa Noeli. Amesema kwamba kwa mwaka huu wao watajaliwa na wingi wa wakimbizi kutoka Ukraine, ambao umewafungulia milango ya nyumba zako kwa ukarimu mkubwa.