Tafuta

2022.12.18 Mahojiano ya Papa 2022.12.18 Mahojiano ya Papa 

Papa:Nilisaini kujiuzulu kwangu ikiwa inatokea vipingamizi vya kiafya

Katika mahojiano na ABC ya Hispania,Papa alibainisha jinsi alivyo kabidhi kwa katibu wa Vatican,Kardinali Bertone,kwa wakati ule barua ya kujiuzulu ikiwa kuna hali ya kiafya inayomzuia kutekeleza majukumu.Papa Paulo VI alikuwa amefanya hivyo.Ameelezea vita Ukraine na pia uwezekano wa mwanamke kuwa mkuu wa Baraza la Kipapa.

Na Angella Rwezaula; -Vatican.

Takriban miaka kumi iliyopita, mwanzoni mwa Upapa  manamo  mwaka wa 2013 (wakati Kadinali Tarcisio Bertone bado alikuwa katibu wa Vatican), Papa Francisko alikabidhi barua yake kwa kesi ya  kujiuzulu ikiwa kuna  kikwazo kwa sababu za kiafya. Uamuzi huu, ambao Papa Paulo VI alikuwa tayari ameuchukua, umefunuliwa na Papa Francisko mwenyewe katika mahojiano ya kina yaliyotolewa katika gazeti la Uhispania la ABC, ambayo ndondoo zake zilikuwa zimetolewa Jumamosi tarehe 17 Desemba 2022. Papa, katika mazungumzo na Julián Quirós mkurugenzi na mwandishi wa Vatican, Javier Martínez-Brocal, anazungumzia masuala mengi kuhusu hali ya sasa ya Kanisa na ulimwengu na miongoni mwake: vita vya Ukraine ambavyo Papa anasema haoni mwisho wake kwa muda mfupi kwa sababu ni vita vya ulimwengu na baadaye kesi za nyanyaso, jukumu la wanawake katika Curia Romana (ambapo amesema ndani ya miaka miwili inawezekana mwanamke kuwa Mkuu wa Baraza la Kipapa ‘Dicastery’), Lula na Catalonia, kujiuzulu kwa Papa Benedikto XVI 2013 na hatimaye kujiuzulu.

Kujiuzulu

Katika suala hilo, Papa alibainisha kuwepo kwa barua hiyo. Kwa sababu alisema kwamba “Tayari nilitia saini kujizulu. Ilikuwa wakati Tarcisio Bertone alipokuwa katibu wa Vatican. Nilitia saini hati hiyo na  kumwambia: 'Iwapo nitakuwa na kikwazo cha matibabu au chochote, hapa kuna barua yangu ya kujiuzulu. Anayo. Sijui Bertone alimpatia nani, lakini nilimpatia alipokuwa Katibu”. “Je, unataka jambo hili lijulikane?” Waliuliza wanaohoji. “Ndiyo maana ninakuambia,” Francisko alijibu, akikumbuka kwamba Papa Paulo VI pia alikuwa ameacha barua ya kujiuzulu kwake imeandikwa ikiwa kungekuwa na  kizuizi na kwamba hata Papa  Pius XII alikuwa amefanya hivyo. “Ni kwa mara ya kwanza ninasema hivyo”, aliongeza Papa. “Sasa labda kuna mtu atakwenda kumuuliza Bertone: 'Nipe barua hiyo'... (Amecheka). Kwa hakika atakuwa aliikabidhi kwa Katibu  mpya wa Vatican. Nilimpatia  kama Katibu wa Serikali

Barua ya Fransisko na mtangulizi wake Paulo VI

Mnamo mwaka wa 2018, katika kitabu kilichohaririwa na Monsinyo Leonardo Sapienza, barua hiyo ilikuwa inatajwa ambayo mnamo 1965 Papa Montini alitangaza kwamba angeacha ikiwa angekuwa  na ugonjwa au ulemavu ...

vita katika Ukraine - ukatili mkubwa

Hata hivyo, mazungumzo hayakukosa kutafakari juu ya mzozo unaoendelea nchini Ukraine, ambao Papa amezungumza zaidi ya mara mia moja. Hata katika mahojiano na ABC amesema kwa uwazi: “Kinachotokea Ukraine ni cha kuogofya. Kuna ukatili mkubwa sana. Ni jambo zito sana... Kwa upande Papa Francisko, “mwisho kwa muda mfupi hauonekani: "Ni suala la vita vya dunia. Tusisahau hilo. Tayari kuna mikono kadhaa inayohusika katika vita. Ni ya kimataifa. Ninaamini vita hupiganwa wakati himaya inapoanza kudhoofika, na wakati kuna silaha za kutumia, kuuza na kujaribu. Inaonekana kwangu kuna maslahi mengi kati yao”. Papa amekumbusha kwamba amejieleza zaidi ya mara mia moja dhidi ya vita: “Ninafanya niwezalo. Hawasikii,”Na anaongeza: “Kinachotokea Ukraine ni cha kuogofya. Kuna ukatili mkubwa sana. Ni mbaya sana. Na hii ndio ninayokemea kila wakati.” Aidha amethibitisha kwamba anapokea na kusikiliza kila mtu: “Sasa Volodymir Zelensky amenitumia mmoja wa washauri wake wa kidini kwa mara ya tatu. Ninawasiliana, ninapokea, ninasaidia…”

Papa amesema "wengine huondoa maneno yangu nje ya muktadha ili kunipeleka wanakotaka”

Kazi ya Papa inakwenda sambamba na ile iliyofanywa katika ngazi ya kidiplomasia na Vatican. Katika suala hilo, waliokuwa wanamhoji wanauliza kwa nini Vatican iko makini sana katika kuelezea dhidi ya tawala za kiimla kama ile ya Ortega huko Nicaragua au Maduro huko Venezuela. Papa alijibu kwamba: “Vatican  siku zote hutafuta kuokoa watu. Silaha yake ni mazungumzo na diplomasia. “Vatican hakiondoki yenyewe. Inafukuzwa. Inajaribu kila wakati kuokoa uhusiano wa kidiplomasia na kuokoa kile kinachoweza kuokolewa kwa uvumilivu na mazungumzo.” Hakuna diplomasia, kinyume  kwa upande wa Papa inaweza kunyanyapaa kesi za unyanyasaji za makasisi: “Ni uchungu sana, uchungu sana”, alisema akimaanisha mikutano na waathirika ambao wameweka alama za upapa. “Hawa ni watu waliharibiwa na wale ambao walitakiwa wawasaidie kukomaa na kukua, hii ni ngumu sana, hata ingekuwa kesi moja tu, ni jambo la kutisha kwamba mtu anayepaswa kukuongoza kwa Mungu anakuharibia njia. Na  katika hili hakuna mazungumzo yanayowezekana

Jukumu la wanawake

Katika mazungumzo na ABC, mwelekeo hubadilika hadi mada za asili ya 'kikanisa' zaidi, kuanzia na jukumu linalowezekana la mwanamke katika Curia Romana. Papa amebainisha kwamba: “Kutakuwa. Nina nia moja kwa Baraza la Kipapa ambalo litakuwa wazi baada ya miaka miwili. Hakuna kikwazo kwa mwanamke kuongoza Baraza la Kipapa ambapo mlei anaweza kuwa Mwenyekiti”. “Ikiwa ni Barza la  asili ya kisakramenti, lazima liongozwe na padre au askofu”,  Papa alifafanua

Kuhusu uchaguzi wa baadaye

Baadaye  walizungumzia juu ya kile kinachoelezwa kwamba kuna utata juu ya ukweli kwamba kazi ya uchaguzi w baadaye unaweza kufanywa kwa ugumu kutokana na ukosefu wa ujuzi kati ya makadinali aliowachagua, wote wakitoka sehemu tofauti na mbali. “Ni kweli, inaweza kuwa na matatizo kutokana na mtazamo wa kibinadamu, lakini ni Roho Mtakatifu anayefanya kazi uchaguzi”, Papa alitoa maoni. Na alikumbuka pendekezo la Kadinali mmoja wa Ujerumani katika mikutano ya Agosti kuhusu Praedicate Evangelium ambaye alisema katika uchaguzi ni makadinali tu wanaoishi Roma washiriki katika uchaguzi wa Papa mpya. “Je, huu ndio umoja wa Kanisa? aliuliza Askofu wa Roma.

Benedikto XVI:mtakatifu, mtu mkuu

Ilirudi tena mada ya  uhusiano na mtangulizi wake Papa Benedikto XVI, ambaye alimfafanua kuwa ni ‘mtakatifu’ na ‘mtu wa maisha ya juu ya kiroho’, na  akafichua jinsi ambavyo Yeye humtembelea mara kwa mara na daima hujisikia kujengeka na macho yake ya uwazi. “Ana ucheshi mzuri, ni mtu mwenye akili timamu, mchangamfu sana, anaongea kwa upole lakini anafuatilia mazungumzo. Namshangaa uhai wake .Yeye ni mtu mkubwa” Papa baadaye ali sema kwamba hana nia ya kufafanua hali ya kisheria ya Papa mstaafu: “Nina hisia kwamba Roho Mtakatifu hana nia ya mimi kushughulika na mambo hayo”.

Papa kwa Kanisa la Ujerumani:kutembea pamoja, wakiongozwa na Roho

Kuhusiana na  Kanisa nchini Ujerumani, likikabiliana na mchakato wa sinodi ambao ulikuwa umeibua  na kuamsha hisia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na zile mbaya, Papa Francisko alikumbuka barua ya wazi sana iliyoandikwa mnamo mwezi Juni 2019: “Niliiandika mwenyewe. Ilinichukua mwezi mmoja. Ilikuwa barua kana kwamba inasema: 'Ndugu, jitafakarini’.

Suala la Catalonia

Papa Francisko  amefafanua katika mahojiano kwamba safari ya Marseilles kwa ajili ya Mkutano wa Mediterania iko katika mipango, huku akibainisha kwamba sio safari ya Ufaransa na kwamba kipaumbele, kwa safari zake za kitume, ni kutembelea nchi Ndogo zaidi barani Ulaya. Alipoulizwa kuhusu swali la Catalonia, Papa alithibitisha kwamba “kila nchi lazima itafute njia yake ya kihistoria ili kutatua matatizo haya. Hakuna suluhisho moja.” Baadaye alitaja kisa cha Makedonia Kaskazini au Tyrol Kusini, nchini Italia, na sheria yake yenyewe. Na kuhusu jukumu ambalo Kanisa linapaswa kudumisha katika jambo hilo, badala yake alisisitiza kwamba: “Kile ambacho Kanisa haliwezi kufanya ni kuegemea upande mmoja au mwingine, bali linaweza kusindikiza watu ili wapate suluhisho la uhakika”. Katika hali hiyo hiyo, Papa alisisitiza kwamba: “Padre anapojihusisha na siasa, sio vizuri... Padre ni mchungaji. Ni lazima kuwasaidia watu kufanya maamuzi mazuri. Kusindikizana nao. Lakini hasiwe mwanasiasa. Ukitaka kujihusisha na siasa, hacha ukuhani na uwe mwanasiasa.”

Kusoma kwa upya sanaa ya  historia ya wakati ili kuleta maana iliyokusudiwa

Alipoulizwa kuhusu tafsiri mbaya ya Ugunduzi wa Amerika, Papa Francisko alitoa mwaliko wa  kutafsiri tukio la kihistoria na sanaa ya ujumbe ulio kusudiwa wa  wakati huo na sio ya sasa. “Ni dhahiri kwamba watu waliuawa huko,  ni dhahiri kwamba kulikuwa na unyonyaji, lakini Wahindi pia waliuana. Mazingira ya vita hayakusafirishwa nje na Wahispania. Na ushindi ulikuwa wa kila mtu. Ninatofautisha kati ya ukoloni na ushindi. Sipendi kusema kwamba Uhispania 'ilishinda' tu. Inaweza kujadiliwa, kwa kile mnachotaka lakini ilitawala.”

Suala la  Lula nchini Brazili

Kesi nyingine  yenye mfano  iliyoletwa na Papa ni ile ya rais mpya wa Brazil, Inácio Lula. Inashangaza kwa sababu mchakato wa kusikilizwa kwa kiongozi huyo wa kisiasa aliyepatikana na hatia ya ufisadi wa kawaida, kwa siku 580 gerezani, alizuiwa kuwa mgombea katika uchaguzi wa rais wa 2018, hadi 2021, wakati Mahakama Kuu ilipobatilisha hukumu zote ilianza na habari za uwongo. Haya, yalitengeneza mazingira ambayo yalipendelea mchakato wake…. Tatizo la habari za uongo kuhusu viongozi wa kisiasa na kijamii ni kubwa sana. Wanaweza kumuangamiza mtu”, Papa alithibitisha, Katika kisa maalum cha Lula, kulingana na Papa Francisko, halikuwa suala la jaribio linalostahili. Kwa maana hiyo alionya kwamba “Jihadharini juu ya wale wanaounda hali kwa ajili ya mchakato, wa chochote kinachoweza kuwa. Wanafanya hivyo kupitia vyombo vya habari kwa namna ya kuwashawishi wale wanaopaswa kuhukumu na kuamua. Kesi lazima iwe safi iwezekanavyo, na mahakama za daraja la kwanza ambazo hazina maslahi mengine isipokuwa kuweka haki safi.”

Suala la Opus Dei

Katika kutazama suala la Motu Proprio ya Ad Charisma mwezi Julai uliopita kwa ajili ya Opus Deui, kwa mujibu wa Papa alisema “Baadhi wamesema: 'Hatimaye Papa amewapa Opus Dei...!'. Sikumpatia chochote. Na wengine, kwa upande mwingine, walisema: 'Ah, Papa anatuvamia!' Hakuna lolote kati ya haya. Hatua hiyo ni uhuishaji  ambao ulihitaji kutatuliwa. Si sawa kuzidisha jambo hilo, wala kuwafanya wahanga, ma ala kuwafanya wawe na hatia kwamba wamepata adhabu. Tafadhali. Mimi ni rafiki mkubwa wa Opus Dei, ninawapenda sana watu wa Opus Dei na wanafanya kazi vizuri Kanisani. Mema wanayofanya ni makubwa sana”.

Mahojiano ya Papa na ABC
18 December 2022, 16:24