Tafuta

Papa:Mungu anajibu ndoto katika migogoro na kutoa peo nyingi!

Unapofanya uzoefu wa mgogoro bila kuangukia kwenye kujifunga binafsi,hisia,woga kwa kubaki kidete na ufunguzi wa mlango wazi kwa Mungu,Yeye anaweza kuingilia kati.Yeye ni mtaalamu katika mabadiliko ya mgororo wa ndoto.Ni Tafakari ya Papa kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana,akitazama sura ya Mtakatifu Yosefu.

Na Angella Rwezaula; - Vatican

Katika Dominika ya Nne ya Majilio tarehe 18 Desemba 2022, kama kawaida, waamini na mahujaji  kutoka sehemu mbali mbali za dunia wamekusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, kuungana na Baba Mtakatifu katika Tafakari na Sala ya Malaika wa Bwana. Katika kuanza tafakari hiyo kwa kuongoza na Injili ya Siku, Baba Mtakatifu amesema: “Leo hii ni Dominika ya nne ya Majilio ambapo liturujia inatuwakilisha sura ya Mtakatifu Yosefu (Mt 1,18-24). Ni mwanaume wa haki ambaye alikuwa anakaribia kuoa. Tunaweza kufikiria ndoto gani alikuwa anaota ya wakati ujao kama vile ya kuwa na  familia nzuri ya  mke wa upendo, watoto wema wengi na kazi yenye hadhi, kwa wastani  ndoto rahisi na nzuri. Ndoto za watu rahisi na wema. Kwa ghafla, lakini ndoto hizo zikamgeukia kuwa na ugunduzi mmoja usiotarajiwa na wa mashaka, kwani mchumba wake Maria ni mjamzito na mtoto huyo sio wa kwake!

Papa Francisko katika sala ya Malaika wa Bwana 18 Desemba 2022
Papa Francisko katika sala ya Malaika wa Bwana 18 Desemba 2022

Ni kitu gani alihisi  Yosefu? Kwa uhakika, mashaka, uchungu, mshituko, mahangaiko na labda hata hasira na kukata tamaa… Dunia ulimwangukia! Je Yeye anaweza kufanya nini? Sheria inampatia uwezekano wa aina mbili: Kwanza kumtangaza Maria na kumfanya alipe fidia ya kutokuwa mwaminifu; Pili kubatilisha uchumba wao kwa siri bila kutoa taarifa ya kashfa ya Maria ambaye matokeo  yangekuwa mazito mno kwake. Lakini kwa kubeba uzito wa aibu hiyo Yosefu anachagua njia ya pili: njia ya huruma”. Baba Mtakatifu Francisko amebanisha kwamba na tazama ndiyo hiyo  katika moyo wa mgogoro, kwani  wakati yeye anafikiri na kutathimini yote, ndipo Mungu aliwasha katika moyo wake ile nuru mpya ya ndoto ambayo inamtangazia kuwa umama wa Maria hautokani na usaliti, lakini unatokana na kazi ya Roho Mtakatifu, na mtoto atakayezaliwa ni Mwokozi (rej Mt 1,20-21). Maria atakuwa mama wa Masiha na yeye atakuwa mlinzi wake. Alipoamka Yosefu akajua kuwa hiyo ni ndoto kubwa sana zaidi ya kila mwisraeli wa ibada kuu, ya kuwa baba wa Masiha, ambaye yuko anatimiza kwake kwa namna isiyotarajiwa kabisa.

Waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kwa sala ya Malaika wa Bwana 18 Desemba 2022
Waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kwa sala ya Malaika wa Bwana 18 Desemba 2022

Ili kutimiza hilo, kiukweli haimtoshi kuwa sehemu ya uzao wa Daudi tu  na kuwa mwaminifu wa kutii sheria, lakini anapaswa atumainie kwa Mungu zaidi ya yote, ampokee Maria na mtoto wake kwa namna tofauti kabisa na jinsi alivyokuwa anatazamia, na tofauti na jinsi ilivyozoeleka hapo awali. Kwa maneno mengine, Yosefu atapaswa ajikane uhakika wake wa usalama, mipango yake kikamilifu, matarajio yake halali na kujifungulia kwa wakati ujao ambao ni wote wa kuweza  kugundua. Na kwa upande wa  Mungu anayepangua mipango na amuomba aamini, na Yosefu anajibu Ndiyo. Papa Francisko ameongeza kusema kuwa “Ujasiri wake ni wa kishujaa na anautimiza katika ukimya; anaamini, anaupokea, yuko tayari, na wala haulizi uhakika kwa undani”.

Waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kwa sala ya Malaika wa Bwana 18 Desemba 2022
Waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kwa sala ya Malaika wa Bwana 18 Desemba 2022

Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu Francisko ameendelea kusema kuwa:  “Je Yosefu leo hii anataka kutueleza nini? Hata sisi pia tunazo ndoto na labda wakati wa Noeli tunafikiri zaidi na tunazungumza pamoja. Labda tunaanza kujutia baadhi ya ndoto zilizoharibika na tunaona kuwa zilizo bora zinazosubiriwa na  mara nyingi lazima zikabiliwe na hali halisi isiyotarajiwa, na zenye mashaka. Lakini hayo yanapotutokea, Yosefu anatuelekeza njia. Kwa hakika sio kuangukia kwenye hisia hasi, hasira na kujifungia binafsi,  kwa sababu hiyo, ni njia yenye makosa!  Kinachotakiwa  badala yake ni kukaribisha mshangao wa maisha katika  migogoro, kwa umakini; Ikiwa huko kwenye mgogoro husichukue uamuzi kwa haraka, au kwa sababu ya mhemko, lakini kufanya kama Yosefu, kwa “kuzingatia mambo yote (Mt 1,20 ) na kuegemezwa katika kigezo cha msingi ambacho ni  huruma ya Mungu.

Waamini katika Sala ya Malaika wa Bwana 18 Desemba 2022
Waamini katika Sala ya Malaika wa Bwana 18 Desemba 2022

Unapofanya uzoefu wa mgogoro bila kuangukia kwenye kujifungia binafsi, hisia, woga na kubaki kidete na ufunguzi wa mlango  wazi kwa Mungu, Yeye anaweza kuingilia kati. Baba Mtakatifu ameongeza “Yeye ni mtaalamu katika mabadiliko ya mgororo wa ndoto. Ndiyo, Mungu anafungua migogoro katika matazamio mapya, labda si kama tulivyokuwa tunasubiri, na wala kufikiria lakini kama Yeye anavyojua. Hizo ndizo peo za Munguambazo  ni za kushangaza lakini zililizo pana sana ambazo haziishi na nzuri sana kwetu!” na Bikira Maria atusaidie kuishi mishangao ya Mungu.

Tafakari ya Papa wakati wa sala ya Malaika wa Bwana 18 Desemba 2022
Baada ya Sala ya Malaika wa Bwana
18 December 2022, 14:15