Mgogoro wa kivita unaendelea kati ya Ukraine na Urussi Mgogoro wa kivita unaendelea kati ya Ukraine na Urussi 

Papa Francisko vita na mauaji ya kimbari:historia inajirudia huko Ukraine

Katika salamu kwa mahujaji waliofika katika katekesi yake Papa ameomba faraja ya Bikira Maria,katika mkesha wa maadhimisho ya Siku Kuu ya Bikira Mkingiwa kwa ajili ya watu wa Ukraine na kwa wale ambao leo hii wanajaribiwa na ukatili wa vita.Papa alikumbuka tukio la kutisha la Operesheni Reinhardt, 1942 ya Wanazi wakati wa Vita vya II vya Dunia.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya katekesi yake tarehe 7 Desemba 2022 amesali  kwa Bikira Maria, katika mkesha wa maadhimisho Siku Kuu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili ambapo ni ombi ya faraja kwa wale ambao leo  hii wanajaribiwa na ukatili wa vita, hasa kwa Ukraine inayoteswa, lakini pia kwa sababu kumbukumbu ya ukatili wa miaka 80 iliyopita,  ili kuweza kuchochea  kila mtu shauku thabiti ya amani.

Papa akumbuka mauaji ya kimbari

Akiwasalimia mahujaji wa Poland, Papa alisisitiza kwamba siku mbili zilizopita Kituo cha Mahusiano ya Wakatoliki na Wayahudi cha Chuo Kikuu Katoliki cha Lublin kiliadhimisha kumbukumbu ya “Operesheni Reinhardt”, iliyoamuliwa na utawala wa Kinazi wa Ujerumani ambao, wakati wa Vita vya Pili vya Dunia kati ya Julai na Oktoba 1942” “Hiyo ilisababisha kuangamizwa kwa karibu wahanga milioni mbili, hasa wa asili ya Kiyahudi. Kumbukumbu ya tukio hilo la kutisha iamshe maazimio na vitendo vya amani ndani yetu sote. Na historia inajirudia.  Ebu tutazame kinachotokea leo hii huko Ukraine. Tuombe amani”.

Maombi kwa ajili ya watu waliouawa Ukraine

Katika kuhitimisha salamu pia kwa waamini wanaozungumza Kiitaliano, Papa ameombema kwa mama Mkingiwa dhambi ya Asili kwamba: “Tunakuomba, Mama mtamu zaidi, uwe faraja kwa wale waliojaribiwa na ukatili wa vita, hasa kwa Ukraine inayoteswa. Tuwaombee hawa mashahidi wanaoteseka sana!”

Salamu kwa Harakati ya Wafocolari

Hata hivyo muda mfupi alikuwa amewasalimia walimu wa seminari za wilaya za Makanisa mapya, huko Roma kwa ajili ya kozi iliyoandaliwa na Baraza la Kipapa kwa ajili ya uinjilishaji, na washiriki katika shule ya mafunzo ya  Harakati ya Wafocolari na akaongeza, “baada ya furaha yao  huwa wanatabasamu, hawa”. Hatimaye, wale wanaoshiriki katika mkutano uliohamaishwa na Pax Christi International, na miongoni mwa wengine waamini wa Pontecurone, mji alikozaliwa Mtakatifu Luigi Orion.

Sikukuu ya  Mkingiwa: tutafute mapenzi ya Mungu katika kila jambo

Katika lugha mbalimbali, Papa alikumbusha  kuwa tarehe 8 Desemba, ni Siku kuu Mkingiwa dhambi ya Asili. “Kwa macho yake akiwa amemwelekeza Bikira Maria, muwe  na  ujasiri katika kuhamasisha maadili ya roho”. Aidha aliwaalika Wareno kuomba neema ya kutafuta mapenzi ya Mungu katika kila kitu na juu ya kila kitu. “Wakati Eva alijiruhusu kushawishiwa na kutomtii Mungu, Bikira Maria alijiruhusu kushawishiwa na Malaika kutii: Na iwe kwangu kama ulivyonena. Hivyo akawa sababu ya Wokovu wetu, akitupatia Mwokozi ... na ikawa Noeli.  Kama Maria tunatayarisha mioyo yetu kumkaribisha na kumtolea Yesu wakati wa Noeli”.  Kwa hiyo hayo ndiyo yalikuwa ni  matakwa yake Papa na kuwapatia  baraka za Mungu.

Baba ya Katekesi 7 Desemba 2022
07 December 2022, 16:04