Papa Francisko:Inawezekana kuchanganua kati ya chaguzi njema na mbaya
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Jumatano tarehe 7 Desemba 2022 ameendeleza mada ya utambuzi katika katekesi yake kwa waaamini na mahujaji waliounganika katika ukumbi wa Paulo VI. Papa Francisko akianza tafakari hiyo amesema ni muhimu katika mchakato wa utambuzi kubaki makini hata katika hatua ambayo inafuata maamuzi yaliyochukuliwa. Katika kuchukua maamuzi, na utambuzi, kuna hisia za dhidi na kusali… kwa maana hiyo unaishi mchakato na kuchukua maamuzi na sehemu hiyo inafikia hatua makini. Hiyo ni ni kutazama ishara ambazo zinathibitisha na ambazo zinakwenda kinyume. Katika maisha kuna maamuzi ambayo sio mema na kuna ishara ambazo zinzpingana na uthibitisho mwema. Baba Mtakatifu alisema kwamba kiukweli alikwisha bainisha jinsi ambavyo kipindi cha muktadha msingi kwa ajili ya kujua sauti ya Mungu katikati ya sauti nyingine nyingi.
Ni Bwana peke yake tu wa wakati, kwa maana katika yeye kuna chapa ya uhakika wa asilia ambayo inamtofautisha na wale wanaomuiga kwa kusungumza kwa jina lake bila kuweza. Moja ya ishara zinazo tofautisha Roho njema ni kwamba zinawasilisha amani ambayo inadumu katika wakati. Ikiwa una fanya maamuzi, mchakato na baadaye unauchukua, na ikiwa aina hii inakupatia amani ambayo inadumu, ni ishara njema, ambayo ni njia ya kufuatilia. Ni amani ambayo inapelekea maelewano, umoja, shauku, na ari. Inakusaidia katika mchakato wa kufanya vizuri zaidi ya ulivyokuwa. Baba Mtakatifu ametoa mfano kwamba ikiwa unachukua maamuzi ya kujikita nusu saa zaidi katika sala, na baadaye unagundua jinsi unaishi vema na wengine katika siku nzima, mwenye utulivu, bila wasi, ninatenda kazi zangu kwa uangalifu na haki hata uhusiano na baadhi ya watu wagumu inakuwa afadhali. Kwa maana hiyo hizi zote ni ishara muhimu za wema wa maamuzi yaliyochukuliwa. Maisha ya kiroho ni mzunguko kwani, wema wa chaguzi ni heri kwa mikitadha yote ya maisha yetu. Kwa sababu ni ushiriki wa ubunifu wa Mungu.
Tunaweza kujua baadhi ya mantiki muhimu zinazotusaidia kusoma wakati mwingine ujao baada ya maamuzi kama uwezekano wa kuthibitisha wema wake. Kipindi stahiki, kinachofuata, kinathibitisha wema wa maamuzi. Kwa mfano, Baba Mtakatifu amekumbusha jinsi ambavyo hayo yamekwisha elezwa kwa namna fula katika mchakato wa katekesi hizi, lakini sasa unapata nafasi zaid. Mtazamo wa kwanza ni ikiwa uamuzi unakuja kuzingatiwa kama uwezekano wa ishara ya jibu la upendo na la ukarimu ambao Bwana anao mbele yetu. Hauzaliwi na hofu, hauzaliwi kuwa kutishia au kulazimisha, lakini inazaliwa kwa shukurani ya wema uliopokelewa, mabo unafanya moyo uweze kuisho kwa uhuru katika mahusiano na Bwana.
Jambo jingine muhimu ni uwelewa wa hisia katika nafsi ya Maisha, ile ya utulivu. Je niko katika nafasi yangu? kuhusu sehemu ya ishara kubwa zaidi ambayo inazingatiwa kutoa mchango binafsi. Katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kuna ncha mbili sahihi iitwayo duaradufu, ambapo nguzo za Bernini zinaweza kuonekana zikiwa zimeunganishwa kikamilifu. Sambamba na hiyo, mtu anaweza kujua kwamba amepata kile ambacho alikuwa anatafuta, wakati siku yake inakuwa na utaratibu zaidi mzuri, anahisi kukua na ufungamanishwaji kati ya mapendeleo yake mengi binafsi, msimamo stahiki wa mamo mambo yake muhimu na anaweza kuishi yote kwa urahisi, akikabiliana na upyaisho wa nguvu na roho ya nguvu katika matatizo ambayo yanajiwakilisha. Hizi ndizo ishara ambazo mtu anakua nayo katika maamuzi mema.
Ishara nyingine nzuri, kwa mfano, ya uthibitisho ni ukweli wa kubaki huru kuhusiana na kile kilichoamuliwa, kuwa tayari kujihoji tena, hata kukataa mbele ya kukanusha iwezekanavyo, kujaribu kupata ndani yake fundisho linalowezekana kutokea. Hii sio kwa sababu Mungu anataka kutunyima kile tunachopenda, lakini ni kuishi kwa uhuru, bila kushikilia sana. Ni Mungu peke yake tu anayejua ni kitu gani kweli kilicho chema kwetu sisi. Kushikilia sana ni adui ya wema na unaua matokeo, hivyo Papa ametoa onyo la kuwa makini na hili suala la kushikilia sana; katika kesi nyingi za vurugu, katika muktadha wa familia, ambapo kwa bahati mbaye habari zinaendelea, zinazaliwa karibu na majivuno ya kushikiria matokeo ya mwingine, utafutaji wa usalama hakika ambao unatoa uhuru na kukandamiza maisha, na kunyanyapaa madai ya kumiliki mwingine ambayo hufanya maisha kuwa kuzimu”.
Tunaweza kupenda tu kwa uhuru, ameongeza Papa, kwa sababu hiyo ndio maana Bwana alituumba huru, huru hata kusema hapana kwake. Kumtolea kile tunachothamini zaidi ni kwa faida yetu, huturuhusu kuishi kwa njia bora zaidi katika uhuru, kama zawadi ambayo ametupatia, kama ishara ya wema wake wa bure, tukijua kwamba maisha yetu, kama zawadi, pamoja na historia nzima, wema uko mikononi mwake. Ni kile ambacho Biblia inakiita hofu ya Mungu, yaani, heshima kwa Mungu, hakuna Mungu anayenitisha, hapana, heshima ni sharti la lazima la kukubali zawadi ya Hekima. (Sira 1,1-18). Ni hofu inayofukuza hofu nyingine zote, kwa sababu imeelekezwa kwa yule Bwana wa kila kitu. Mbele yake hakuna kinachoweza kutusumbua. Ni tukio la kustaajabisha la Mtakatifu Paulo, ambaye alisema: “Nilijifunza kuwa maskini na nilijifunza kuwa tajiri; Nimeanzishwa katika kila kitu, kwa kila njia: kushiba na njaa, wingi na ukosefu. Nayaweza yote katika yeye anitiaye nguvu”(Fil 4,12-13).
Baba Mtakatifu amesema kuwa huyo ni mwanaume huru ambaye nabariki Bwana wakati mwema na usio mwema na hivyo ahimidiwe na twende mbele. Kutambua hilo ni muhimu kwa uamuzi mzuri, na hutuhakikishia juu ya kile ambacho hatuwezi kudhibiti au kutabiri kama vile afya, siku zijazo, wapendwa na mipango yetu. Kilicho muhimu ni kwamba tumaini letu limewekwa kwa Bwana wa ulimwengu, ambaye anatupenda sana na anajua kwamba Kwake yeye tunaweza kujenga kitu cha ajabu sana, kitu cha milele. Maisha ya watakatifu yanatuonesha hilo kwa njia nzuri zaidi. Kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu ameomba kuelendelea mbele kwa kutafuta kufanya maamuzi namna hiyo, katika sala na kuhisi nini kinatokea katika moyo wote na kwenda mbele taratibu kwa ujasiri.