Papa Francisko:Mungu kumwita jina Umejaa Neema,anafunua siri kubwa!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika siku ambayo Mama Kanisa anaadhimisha Siku Kuu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili, Baba Mtakatifu Francisko ametoa tafakari yake kwa waamini na mahujaji waliofika kwa wingi katika uwanja wa Mtakatifu Petro, Alhamisi tarehe 8 Desemba 2022. Baba Mtakatifu akianza tafakari amesema, “Injili ya Siku Kuu inatoa utangulizi katika nyumba ya Maria ili kutusimulia upashanaji(Lk 1,26-38). Malaika Gabrieli alimsalimia Bikira namna hii: “ furahi, uliyejaa neema, Bwana yuko Nawe (Lk 1,28). Hakumwita kwa jina lake Maria, lakini kwa jina jipya, ambalo yeye hakulijua, yaani umejaa neema. Umejaa neema na kwa njia hiyo inaondoa dhambi, ni jina ambalo Mungi anamwita na ambalo sisi leo hii tunalisheherekea. Lakini tufikirie kwa mshangao wa Maria. Ni wakati huo tu yeye aligundua utambulisho wake wa kweli zaidi. Kiukweli kwa kumwita jina hilo Mungu anamfunulia siri kubwa zaidi, ambayo kwanza aliidharau. Kitu kama hicho kinaweza kujitokeza hata kwetu. Kwa maana gani? Katika maana kwamba hata sisi ni wadhambi tulipokea zawadi ya kwanza ambayo ilitujaza maisha, ambayo ni kubwa zaidi ya yote, tulipokea neema asilia. Sisi tunazungumza sana kuhusu dhambi ya asili, lakini pia tulipokea neema asili ambayo mara nyingi licha ya yote hatuitambui.
Je hiki ni kitu gani, neema hii asili? Kile ambacho tulikipokea katika siku ya Ubatizo wetu, ambao inakuwa vizuri kuikumbuka na hata kuisheherekea! Papa ametaka kuuliza swali : Neema hii iliyopokelewa siku ya Ubatizo ni muhimu. Lakini ni wangapi wenu mnakumbuka tarehe ya Ubatizo wenu, ni tarehe ngapi ya Ubatizo wenu? Fikirieni. Na ikiwa humkumbuki, njiani nyumbani, muulize bibi, babu, baba au mama: "Nilibatizwa lini? Kwa sababu siku hiyo ni siku ya neema kubwa, ya mwanzo mpya wa maisha, ya neema ya asili tuliyo nayo”. Mungu alishuka katika maisha yetu siku ile, na tangu siku ile tumegeuka daima watoto wake wapendwa. Na ndiyo uzuri wetu asili ambao ni wa kufurahia! Baba Mtakatifu Francisko amesema, leo hii Maria akishangazwa na neema ambayo ilimfanya kuwa mzuri tangu awali ya maisha yake, anatupelekea kushangazwa na uzuri wetu. Tunaweza kuupokea kupitia picha ile ya vazi jeupe la Ubatizo; hilo linatukumbusha kuwa , chini yake ambapo tumechafuliwa kwa miaka mengi, ndani mwetu kuna wema ulio mkubwa zaidi ya mabaya yaliyojitokeza.
Tusikilize mwangwi wake, tuhisi Mungu ambaye anatueleza “ Mwana, binti, ninakupenda na niko nawe daima, wewe ni muhimu kwangu, maisha yako ni yenye thamani. Hiyo ndio hotuba ya Mungu kwetu. Ikiwa mambo hayaendi na tunakata tamaa, ikiwa tunaanguka chini na kuhatarisha kuhisi wa bure, au wakosaji, tuhisi hili katika neema asilia. Na Mungu yuko nasi, Mungu yuko nami tangu siku ile. Ni vema kufikiria tena”, Papa ameshauri. Baba Mtakatifu amekazia kusema kwamba leo hii Neno la Mungu linatufungulia jambo jingine muhimu, kwamba katika kuhifadhi uzuri wetu, unahitaji gharama, na kuwa na mapambano. Injili inatuenesha kiukweli ujasiri wa Maria ambaye alisema “ tazama mimi hapa ” kwa Mungu ambaye alichagua hatari ya Mungu; na andiko la Kitabu cha Mwanzo, kuhusiana na dhambi ya asili, linatueleza juu ya mapambano dhidi ya mshwishi na vishawishi vyake (Mw 3,15). Lakini hata uzoefu ambao tunatambua. Ni gharama kuchagua wema, kuhifadhi wema uliomo ndani mwetu. “Hebu tufikire ni mara ngapi tumeipoteza kwa kujipendekeza kwa maovu, kwa kuwa wajanja kwa ajili ya maslahi yetu au kwa kufanya jambo ambalo lingeichafua mioyo yetu; au hata kupoteza muda kwa mambo yasiyo na faida na madhara, kuahirisha maombi na kusema “siwezi” kwa wale waliotuhitaji, wakati badala yake tungeweza”.
Baba Mtakatifu akiongeza amesema lakini mbele ya yote hayo, leo hii tunayo habari njema. Maria ndiye kiumbe pekee cha binadamu hasiye na dhambi katika historia, yupo pamoja nasi katika mapambano, ni kama dada na zaidi ya yote Mama. Na sisi ambao inakuwa vigumu kuchagua mema, tunaweza kumwamini yeye. Kwa kumkabidhi Mama basi tusema “ Nishike mkono, Mama niongoza wewe, kwako wewe nitakuwa na nguvu ya kupambana dhidi ya ubaya, kwako wewe nitagundua uzuri wangu asili”. Tumkabidhi Maria leo hii, tumkabidhi Maria kila siku kwa kurudia “ Maria, ninakukabidhi maisha yangu, ninakukabidhi famila yangu, kazi yangu, ninakukabidhi moyo wangu na mapambano yangu. Ninajiweka kwako wakfu” Mkingiwa utusaidiea kushida mabaya katika uzuri wetu.