Papa Francisko kwa waseminari:mwabudu Kristo katika sakramenti na Neno!
Na Angella Rwezaula;- Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 10 Desemba 2022, amekutana na Jumuiya ya Waseminari wa Barcellona nchini Hispania waolifika mjini Vatican, ambapo amezungumza nao moja kwa moja katika lugha ya kihispania na hotuba aliyokuwa ameiandaa amewakadhi. Katika hotuba yake aliyowakabidhi, Baba Mtakatifu anawashukuru na kuwakaribisha katika nyumba ya Petro ambayo amesema ni nyumba ya Kanisa lote. Ametambua jinsi walivyotamani sana mkutano huo na walivyomwomba Askofu Mkuu ili kuweza kukutana nao. Papa ameongeza kundika “Tazama sala isiyoisha inazaa matunda yake na hivyo wasisahau kamwe. Ni muhimu pia kuomba kwa njia ya Kanisa, kwa maana hiyo wasiache kamwe kuombea wachungaji wao na waamini wao, ili Mungu wajaliwe uvumilivu katika mchakato wa mema. Kwa upande wa walelewa, Baba Mtakatifu Francisko amekazia kusema kwamba, kuna aina mbili za vishawishi, kile cha kijikunjia juu ya mambo mabaya kwa kuzingatia uzoefu hasi tu na ile ya kutafuta kuwakilisha ulimwengu wa kufikirika na usio wa kweli. Ndio maana kwa kuzingatia mada hiyo ya sala ambayo wameanza, Papa Francisko ameonelea kwamba ni muhimu kutafakari kwa kina kitabu cha Askofu Mtakatifu wa ardhi yao, ambaye Mtakatifu Manuel González, ambaye anafafanua rozari ya kikuhani mambo mazuri na yale mabaya ambayo amesema ni kujiuliza, na kufanya kuwa sala ambayo kwa njia ya maombezi ya Mama Safi wa moyo wanawakilishwa kwa Mungu.
Baba Mtakatifu anaendelea kueleza kwamba wao ambao watakuwa makuhani, ulazima wao wa kwanza utakuwa ni maisha ya sala yanayozaliwa na shukrani kwa ajili ya upendo wa kuchaguliwa ambapo Mungu alijionesha kwao katika kuwaita kwenye huduma yake. Hiyo ndio huduma yao ya kwanza ya furaha ambayo kila kitu huzaliwa. Katika hatua ya malezi ambayo wao wamo, ingekuwa vizuri ikiwa katika sala zao wangeweza kuiga tabia za Bikira Mtakatifu na kujiuliza: Yeye alikuwa wapi wakati Mungu alimwita? Je mimi nilikuwaje? Itakuwa ni mantiki gani ya wakati wa maisha ya kikuhani yajayo? Kwa maana hiyo katika kujibu Mtakatifu Manuel anasema kwamba : “Nitainuka kama povu kwenye sufuria inayochemka upendo ili kupeleka Mungu katika ulimwengu? Nitakwea juu ya kilima, katika hali ngumu na yenye uchungu zaidi? Baba Mtakatifu ameongeza “Kuhani sio mtoaji wa roho kwa njia ya shaba na dhahabu… utajiri wake, uwezo wake tu ni fadhila katika jina la Yesu”, hiyo ina maana ya kumfanya uwepo wake katika Ekaristi, katika sakramenti, na katika neno ili azaliwe ndani ya mioyo ya watu, kuwa kila kitu, na daima kuwa chombo chake. “Kwa maana hiyo tunajitoa kama Yesu, katika hekalu, kama dhabihu, kwa ajili wokovu wa ulimwengu.
Na huduma ya mwisho ya furaha kuna wazo muhimu sana kwa ajili ya maisha yao yote, ambapo Papa amesema wasiache kamwe kwa kufikiria Yesu aliye potelea hekaluni, na kwamba ni kwa yule Yesu ambaye wao wanapaswa warudi kumtafuta katika Taberkulo. Wapotelee pale na Yeye, kwa kusubiri ndugu zao: kwa upande mwingine, maadamu wamebakiwa na macho ya kulia, mikono ya kujidharau na mwili wa kutesa, hawana haki ya kusema kuwa wamefanya kile walichopaswa kufanya kwa ajili ya roho walizokabidhiwa. “Kujitolea huku kunaonesha kile wanachoweza kutafakari katika Tendo la Huzuni. Mungu anatuomba kujitoa sadaka, sadaka ya moyo, ya kukataa mapenzi yetu, kama anavyo pendekeza huko Gethsemane; sadaka ya usikivu, katika hali ya kujinyima ambayo tunatafakari katika ulinganifu; sadaka ya heshima, ambayo kwa Kihispania, akifikiri , kama wanavyoimba katika wimbo wa Kwaresima kwamba kutafuta taji la heshima, la cheo kitaaluma, la sifa za kidunia hutuweka mbali na Mungu, na ni lazima afadhali kutamani taji za miiba zinazotutambulishe na Bwana”.
Katika hilo ni sadaka ya kukubaliwa kwa msalaba wake na kuanza mchakato wa safari, mara nyingi wa kujikabidhi ni sadaka ya maisha. Kwa kutazama msalaba, Baba Mtakatifu ameongeza: “tuinue macho yetu mbingu na kuona hatima yetu. Je mnafikiri ni ngumu? Sio, mambo rahisi yanatosha: kitanda kigumu, chumba nyembamba, meza ndogo na maskini, usiku karibu na kitanda cha wanaokufa, kuamka asubuhi na mapema ili kufungua Kanisa kabla ya kwenda bar na kusubiri, kusindikiza Yesu aliye pekee yake, kwa ajili ya wenye dhambi na waliojeruhiwa katika safari ya uzima. Baba Mtakatifu amesema na wanafikiri katika tendo la Utukufu ambalo ni matendo ya kushukuru kwa Misa ya Yesu juu ya Msalaba. Baada ya ushindi wa ufufuko, Yesu aliingia katika madhabahu ya mbingu na anaendeleza daima matendo ya kushukuru. Kwa kumwona amekaa kuume kwa Baba anatualika kwa matumaini na kutujaza furaha, kwa sababu anatuhakikishia mbingu. Hatimaye Mungu anatuma Roho Mtakatifu, wa pekee ambaye anaweza kufundisha huduma na siku moja anatawapatia wao zawadi ya kuwa makuhani wa Kristo.
Papa amesema Wasiache kamwe kuonja, na kuomba upendo huo wa kupendelewa, ambao umewafikia na utakuwa nao kwa wingi katika moyo wao na katika kuwekwa kwao wakfu, na katika mengine ya siku zao. Wasizime kamwe moto ambao unawafanya wawe vuguvugu katika kuhubiri Injili, watoe hazina ya huduma zenye thamani za kimungu. Mwili wao uungane na wa Yesu na Maria ili kujitoa pamoja naye katika sadaka ya Ekaristi, na pia katika utukufu wa ushindi wake. Kwa kuhitimisha, Baba Mtakatifu amewambia waseminari kuwa wachukue rozari zao, na kuomba Maria, Malkia na Mama wa Huruma awasaidie kugundua huduma za kikuhani ambazo Mungu anawaita, watafakari huduma za Mwanae, kwa kukubali kuwa furaha ya ufuasi na ukamilifu wa utambulisho juu ya Msalama ndiyo njia pekee kwa wajili ya utukufu. Amewabariki.