Ujumbe wa Papa Francisko kwa Watu wa Kujitolea WYD 2023! Msiogope
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko ametoa ujumbe wake kwa njia ya video kwa lugha ya kisipanyola, kwa watu wa kujitolea wa Siku ya Vijana duniani(WYD)2023 kuanzia tarehe 1-6 Agosti, huko Lisbon nchini Ureno, ili kuwashukuru katika fursa ya Siku ya Kimataifa ya Watu wa Kujitolea ifanyikayo kila tarehe 5 Desemba ya kila mwaka.
Katika ujumbe wake Baba Mtakatifu amesema: “Moja ya mambo ambayo yamenishangaza zaidi ni kuona baadhi ya Makanisa yana nguvu ya watu wa kujitolea. Ndio kuna maaskofu, mapadre, watawa, walei, na wengineo. Lakini watu wa kujitolea ni kitu kingine, kujitolea kati ya mambo mengini ni nguvu isiyo vunjika, ni kuondokana na mantiki ya kitu, na ni kuunganisha ili kuendeleza mbele kitu. Kujitolea kuna uhifadhi huu wa kupelea kitu mbele”.
Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na ujumbe wake kwa njia ya video amesema kwamba: “kwa mfano kujitolea na wagonjwa ni wanaume na wanawake ambao wapo hapo siku nzima, katika wakati ambao wana nafasi, na wananya kazi na wagonjwa. Kujitolea ni uhakika wa Mungu. Kujitolea ni neema ya Mungu. Tafadhali tia bidii kwa nguvu”. Baba Mtakatifu amewambia watu wa kujitolea kwamba wao ni nguvu ya Kanisa, wao ni sehemu nyingi ya matendo ya Kanisa. “Msiwe na hofu. Asante kwa ukarimu, kwa ukarimu ambao kila mwanakujitolea wa kike na kiume. Mungu awabariki. Tafadhali mniombee.”