Tafuta

2022.12.08 Papa ametao heshima kwa Bikira Maria Mkingiwa wa dhambi ya asili  na kumkabidhi ulimwengu mzima. 2022.12.08 Papa ametao heshima kwa Bikira Maria Mkingiwa wa dhambi ya asili na kumkabidhi ulimwengu mzima. 

Papa Francisko amesali kwa Mama Maria kwa ajili ya ulimwengu wote

Papa Francisko amesali kwa ajili ya ulimwengu wote mbele ya Picha ya Bikira Maria katika Siku Kuu ya Bikira Maria Mkingiwa wa Asili:"Ninakuleta tabasamu za watoto,shukrani za wazee na watu wazima,mahangaiko ya familia, ya mababa na mama wasio jua kukabiliana na changamoto.Ninakukabidhi ndoto na wasi wasi za vijana hasa ambao wamehisi zaidi janga la uviko”.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kwa mwaka huu, imewezekana kufanya ibada ya watu wa Roma katika siku kuu ya Mkingiwa dhambi ya Asili tarehe 8 Desemba 2022, ambapo Baba Mtakatifu Francisko kwanza alikwenda katika Kanisa Kuu la Bikira Maria Mkuu na kusali mbele ya Picha ya Bikira Afya ya Warumi na baadaye kwenda uwanja wa Hispania kutoa heshima yake katika Picha iliyoko kwenye kinara. Chini ya miguu hiyo ya Picha ya Mama Baba Mtakatifu amesali sala kwa kumkabidhi Yeye ambayo inajikita kwenye hali zote za maisha ya kila siku duniani.

Tukio la sala ya Papa katika siku kuu ya Bikira Maria mkingiwa dhambi ya asili
Papa amesali kwa Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya asili akimkabidhi matakwa ya ulimwengu
Papa amesali kwa Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya asili akimkabidhi matakwa ya ulimwengu

Sala ya Baba Mtakatifu ameanza: Mama Yetu Mkingiwa, leo watu wa Roma wanakusanyika kwako. Maua yaliyowekwa kwenye miguu yako na hali halisi ya uzalendo inayoeleza upendo na ibada kwako ambaye unakesha kwa ajili yetu sote. Wewe unaona na kupokea hata maua yasiyoonekana ambayo ni maombi mengi, maombi mengi ya kimya, ambayo wakati mwingine yamesongwa, yamefichika lakini si kwako, ambaye ni Mama. Baada ya  kuja miaka miwili kukuheshimu tu katika mapambazuka ya siku, leo hii nimerudi kwako pamoja na watu wa Kanisa hili na Mji huu. Ninakuletea shukrani zangu na maombi ya wana wako wote, wa karibu na mbali. Wewe huko mbinguni ambako Mungu alikupokea, unatazama mambo ya dunia  vema kuliko sisi; lakini kama Mama sikiliza maombi yetu, ili uyawakilishe kwa Mwanao, katika moyo wake uliojaa huruma. Awali ya yote ninakuletea upendo wa kimwana wa wanawake na wanwaume wengi, na sio tu wakristo, ambao wanamwilishwa kwako utambuzi mkubwa sana, kwa ajili ya uzuri wako wote wa neema na unyenyekevu: kwa sababu katikati ya mawingu meusi, wewe ni ishara ya tumaini na ya faraja. 

Ninakuleta tabasamu za watoto, ambao wanajifunza jina lake mbele ya picha yako, wakiwa kwenye mikono ya mama yao na bibi zao, na wanaanza kujua kwamba wanaye hata Mama wa Mbinguni. Na ikitokea kwamba katika maisha zile tabasamu zinaacha nafasi ya machozi, ni jinsi gani ilivyo muhimu  kukutambua wewe na kuwa na zawadi ya umama wako! Ninakuleta shukrani za wazee na watu wazima: neema ambayo inafanya kitu kimoja kwa maisha yao, kiungo cha kumbu kumbu, cha furaha na uchungu, cha matarajio ambayo wao wanatambua vizuri ya kwamba wamefikia kutokana na msaada wako, kwa kushikiliwa  mkono kwa mkono wako.

Ninakuletea mahangaiko ya familia,  ya mababa na mama ambao mara nyingi inakuwa ngumu kuweka mzani sawa wa nyumba, na kukabiliana siku kwa siku changamoto ndogo na kubwa ili kwenda mbele. Kwa namna ya pekee ninakukabidhi wenzi vijana kwa sabababu ya kukutazama wewe na Mtakatifu Yosefu, wanaweza kwenda kukabiliana na maisha kwa ujasiri, kwa kuamini katika Mungu mpaji. Ninakukabidhi ndoto na wasi wasi za vijana, waliowazi katika wakati ujao lakini wakisimamishwa na utamaduni tajiri ya mambo na maskini wa thamani, wakijazwa pomoni na habari na kushuka kwa elimu, wenye kushawishiwa katika kudanganya na wasio  na huruma katika kukatisha tamaa. Ninakukabidhi hasa vijana ambao wamehisi zaidi janga la uviko, ili pole ple waweze kuinuka na kuanza kufungua mabawa yao na kupata thamni ya kweli ya juu.

Bikira Mkingiwa, nilitaka leo hii nikuletee shukrani kwa watu wa Ukraine kwa  sababu ya amani ambapo kwa kipindi kirefu tunaomba kwa Bwana. Kinyume chake bado tena ninawakilisha maombi ya watoto, wazee, mababa , mama na vijana ambao wanateseka katika ardhi ile. Lakini kiukweli sisi tunaelewa kwamba wewe huko na wao wanaoteseka wote, hivyo kama ulivyokukuwa karibu na mtoto wako msalabani. Asante Mama Yetu! Kwa kukutazama wewe, usiye na dhambi, tunaweza kuendelea kuamini na kutumaini kuwa chuki inashindwa na upendo, ukweli unashinda uongo, msamaha hushinda mkosaji, na amani inashinda vita. Na iwe hivyo.

Sala ya Papa mbele ya picha ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya asili 8 Desemba 2022
08 December 2022, 17:13