Tafuta

Papa Francisko amemtuma mwakilishi wake Krajewski Ischia Papa Francisko amemtuma mwakilishi wake Krajewski Ischia 

Papa Francisko anamtuma mwakilishi wake Krajewski huko Ischia

Kisiwa kilichogubikwa na maporomoko ya ardhi mnamo Jumamosi tarehe 26 Novemba,kitatembelewa na Mwakilishi wa Kipapa,aliyetumwa na Baba Mtakatifu kuonesha ukaribu wake katika wakati huu wa machungu ya kupoteza maisha ya watu 12.

Na Angella Rwezaula;  – Vatican.

Katika siku ya maombolezo kwenye manispaa sita za kisiwa cha Ischia, nchini Italia kwa mujibu wa taarifa kutoka Baraza la Kipapa la Upendo, limetangaza kuwasili kwaKardinali Konrad Krajewski Dominika tarehe 8 Desemba 2022.  Katika taarifa hiyo inabainisha kwamba  ziara ambayo, katika Maadhimisho Siku Kuu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili inakusudia kuwa kitulizo na faraja kwa familia zilizojaribiwa kwa kuondokewa na wapendwa wao kutokana na maparomoko yaliyokumba kisiwa hicho na kupoteza maisha ya watu 12.

Mwakilishi wa  Papa  kwa maana hiyo atatembelea kila familia ya wafiwa  ili kutoa kwa kila familia, “Rozari iliyobarikiwa na Papa Francisko,na kusudi wanafamilia hao  waweze kuhisi faraja ya sala yake na kujikabidhi kwa matumaini kwa Mama Bikira. Hata hivyo maombi yameinulia Jumatano tarehe 7 Desemba katika Kanisa la Mtakatifu Maria wa Neema huko Lacco Ameno ambapo mazishi ya wachumba wawili  Eleonora Sirabella na Salvatore Impagliazzo yaliadhimishwa na Askofu Gennaro Pascarella wa Ischia,  ambao ni  watu wawili kati ya waathrika 12 waliosombwa na maporomoko ya ardhi kutoka Mlimani Epomeo tarehe 26 Novemba 2022,

Tarehe 5 Desemba hatimaye uligunduliwa mwili mwisho wa Maria Teresa Arcamone, mwanamke mwenye umri wa miaka 31 ambaye alikuwa anafanya kazi kama mhudumu katika bar huko Forio. Miongoni mwa waathirika pia kuna watoto kadhaa, kama vile Francesco, Maria Teresa na Michele, watoto wa Valentina Castagna na Gianluca Monti, mtoto wa wiki tatu ambaye alikufa pamoja na wazazi wake Maurizio Scotto na Giovanna Mazzella, vile vile na  Nikolinka Gancheva Blangova.

Tetemeko la ardhi katika kisiwa cha Ischia mnamo 2015

Kardinali Krajewski, tayari mnamo Desemba 2015, alikuwa amekwenda kwenye kisiwa hicho  Ischia, miezi 4 baada ya tetemeko la ardhi la daraja la nne katika kipimo cha Richter, tena kwa agizo la Papa Francisko. Tetemeko hilo lolisababisha vifo vya watu wawili na kuharibika kwa majengo mengi  ya watu yakiwemo ya Casamicciola, Lacco Ameno na Forio, yenye karibu  watu 2,500 waliokimbia makazi yao. Baadaye Msimamizi wa sadaka ya Kitume alikutana nao, akisikiliza historia zao ngumu na kwa kupeleka mkumbatia kwao kutoka kwa papa Francisko.

07 December 2022, 17:34