Msaada wa Kipapa kukarabati Parokia ya Mtakatifu Francis huko Honduras
Na Angella Rwezaula;– Vatican
Mchango wa Papa Francisko ulifika hadi Luquigüe, huko Yoro (Honduras), ili kuwezesha urejesho wa Kanisa la Mtakatifu Francis wa Assisi, lililojengwa zaidi ya miaka 400 iliyopita, ambalo linawakilisha urithi wa kiutamaduni na usanifu wa nchi kwa karne za mwisho. Mpango huo pia unajumuisha urejesho wa monasteri ya Wafransiskani waliofika katika nchi hizo kuinjilisha jumuiya mbalimbali za kiasili za Tolupan katika eneo hilo. Kuna maneno ya shukrani kutoka kwa Askofu Héctor David García Osorio wa Jimbo la Yoro, Paroko wa kanisa hilo, Padre Marcio Mejía; na waendelezaji wa mpango huo: Flora Castro, mzaliwa wa nchi na balozi wa zamani wa Vatican, Carlos Cordero. Kanisa na monasteri zinaonesha uharibifu unaosababishwa na unyevunyevu, mimea na tetemeko, ambalo lilisababisha nyufa na mipasuko hadi kuanguka kwa sakafu na dari.
Kuinjilisha katika nchi ambazo ni vigumu kufikiwa
Kutoka katika ardhi hiyo Padre Marcio Mejía, padre pekee katika eneo hilo, anawajibika kwa jumuiya 55, na kila siku anasafiri kwenye barabara ambazo ni vigumu kuzifikia, kusherehekea misa, ubatizo na kipaimara, kufikia jumuiya zote za kiasili. Kama kuhani alisema, hekalu liliachwa katika ujenzi wake, lakini sio kwa ibada ya waamini wake, ambapo Ekaristi iliadhimishwa kila Dominika. Na sasa kazi ya urejeshaji inaendelea, jumuiya nzima imehamia kusalia kwenye darasa katika shule ya kijiji, iitwayo Flora Castro. Kila Dominika ya tatu ya Pasaka, waamini na makasisi wa Jimbo la Yoro pamoja na Askofu wao Héctor David García Osorio, hukusanyika katika hekalu la Luquigüe kuadhimisha "Siku ya Jimbo.".
Msaada wa Papa
Mpango huo uliendelezwa na Flora Castro, mwenye asili ya nchini humo, ambaye aliomba ubalozi huo wa nchi yake unaowakilishwa Vatican usaidizi katika kutekeleza marejesho hayo. Papa Francisko kwa maana hiyo, alipopata habari hiyo, alitaka kutoa mchango kwa jimbo la Yoro ili kuanza kazi hiyo. Kulingana na Askofu García, Papa alituma pesa hizo moja kwa moja katika jimbo mnamo tarehe 16 Aprili 2021. Kazi zilianza kuchelewa kutokana na taratibu nyingi ambazo hazikutarajiwa ambazo zilipaswa kufanywa kabla ya kuanza. Walilazimika kuomba vibali kutoka Taasisi ya Historia na Anthropolojia kisha kuajiri mtu ambaye alitakiwa kufuatilia mpango huo, alisema. Kwa hiyo, baada ya ya tarehe 24 Mei tu kazi ya kukarabati na kujenga upya ilianza. Askofu pia alieleza kwamba kuna awamu tatu katika ujenzi au ukarabati wake, kuanzia hatua ya paa,ambayo imeanza kwa pesa za Papa, kwa sababu ilikuwa ni kwa haraka sana maana ilianza kuanguka.