Tafuta

Muonekano wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro  na nje yake . Muonekano wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na nje yake . 

Mifuko ya kifedha ya Vatican chini ya udhibiti wa vyombo vya kiuchumi vya Curia

Hiyo imeanzishwa na Papa kwa barua binafsi ya Motu Proprio ambayo inahusu vyombo vyote vilivyozaliwa ndani ya taasisi za Curia ambavyo hadi sasa vilifurahia uhuru fulani wa utawala.Sheria mpya pia imepanuliwa kwa mashirika ambayo yao chini ya makao makuu ya mji wa Vatican.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kwa kuchukua kifungu cha Kiinjili kisemacho “Aliye mwaminifu katika mambo madogo ni mwaminifu katika mambo makubwa pia, Papa Francisko amenukuu sura ya 16 ya Injili ya Luka katika kutambulisha Barua  yake binafsi ya Motu Proprio ambayo inahusu watu muhimu wa kisheria, kwa upande wa  mifuko ya kifedha, vyama vya mifuko , na   mashirika yote yaliyojisajiri Vatican katika orodha iliyorejewa katika kifungu cha 1 § 1 cha Sheria ya nchi chha Baraza la Uchumi na lenye makao yake katika mji wa Vatican.

Udhibiti na ufuatiliaji

Katika maandishi yake Papa,  anafafanua kuwa: ”ngawa vyombo hivi vina mikitadha tofauti ya kisheria na uhuru fulani wa kiutawala,  lakini ni lazima vitambuliwe  na kwamba ni muhimu katika utimilifu wa malengo yanayofaa kwa taasisi za Curia Romana katika huduma ya Mrithi wa Petro na kwa hiyo, wao pia ni, isipokuwa kama imeoneshwa vinginevyo na sheria ambayo imeanzishwa  kwa namna fulani, mashirika ya umma ya Vatican. Kwa hiyo, kwa kuwa mali zao za muda ni sehemu ya urithi wa Kiti cha Kitume, ni lazima ziwe chini ya usimamizi wa taasisi ya Curia ambazo wanazitegemea, lakini pia chini ya udhibiti na usimamizi wa vyombo vya kiuchumi vya Curia Romana. Kwa njia hiyo, vyombo hivyo muhimu vya kisheria vitatofautishwa wazi na mifuko, vyama na mashirika mengine yasiyo ya kiserikali ambayo yamezaliwa kutokana na mpango wa watu binafsi na sio muhimu katika utambuzi wa malengo sahihi ya taasisi za Curia. Mashirika ya kisheria yaliyopo yatalazimika kutii masharti ya Motu Proprio ndani ya miezi mitatu baada ya kuanza kutumika, inayotarajiwa kuanzia tarehe 8 Desemba 2022.

Jukumu la Sekretarieti ya Uchumi

Barua binafasi ya Motu Proprio imeundwa na makala nane. Ibara ya Tatu inahusu usimamizi na udhibiti katika masuala ya uchumi na fedha, na kubainisha kuwa Sekretarieti ya Uchumi inasimamia na kudhibiti vyombo muhimu vya kisheria kwa mujibu wa sheria yake na, ndani ya upeo wa uwezo wake, kupitisha au kupendekeza kupitishwa na serikali, watu muhimu wa kisheria wa hatua za kutosha  ya kuzuia na kulinganisha shughuli za uhalifu. Ibara ya nne na ya tano, zinajikita katika kumbukumbu za hesabu na ubadilishanaji wa taarifa, zikibainisha pamoja na mambo mengine kwamba wahusika wa kisheria lazima wawasilishe bajeti na salio la mwisho kwa Sekretarieti ya Uchumi ndani ya masharti yaliyowekwa na Sekretarieti hiyo hiyo na kutoa masharti kwamba Sekretarieti ya Uchumi na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu inaweza kila wakati kufikia rekodi za uhasibu, nyaraka za usaidizi na taarifa zinazohusiana na miamala ya fedha.

Matumizi ya Motu Proprio kuanzia tarehe 8 Desemba

Ibara ya 6 inahusu kutoweka na kugawiwa kwa mali na kubainisha jinsi watu wenye mamlaka muhimu wanavyokandamizwa na kuwekwa katika kufilisishwa kwa amri ya Taasisi ya kiutamaduni ambayo wanaitegemea kisheria, wakati madhumuni yamefikiwa au imekuwa haiwezekani au kinyume na sheria, au, kwa upande wa vyama, wakati kupunguzwa kwa idadi ya wanachama kunazuia utendaji wao.  Kwa kuzingatia hitaji la kutoa nidhamu ya muhimili na kusasishwa  kwa vyombo muhimu vya kisheria vilivyoko Vatican,  Tume ya Kipapa ya  serikali ya mji wa  Vatican imetangaza sheria, tarehe 6 Desemba 2022 ambayo pia itaanza kutumika tangu tarehe 8 Desemba 2022,  ambayo inapanua matumizi ya barua ya  Motu Proprio kwa vyombo vya mashirika ya Vatican. Taasisi za curia na ofisi za Curia Romana, taasisi zinazohusiana na Vatican,  Gavana wa mji wa Vatican na mashirika yanayoshughuli za kifedha kitaaluma hazijajumuishwa katika wigo wa matumizi ya sheria. Kifungu hicho ni sehemu ya mageuzi yaliyoaidhinishwa na Papa katika Katiba ya Kitume Praedicate Evangelium.

06 December 2022, 16:21