Tafuta

Papa amekutana na wafanyakazi mjini Vaticana na kuwaonya wasisengenyane bali kuwa na ujasiri wa kukabiliana uso kwa uso. Papa amekutana na wafanyakazi mjini Vaticana na kuwaonya wasisengenyane bali kuwa na ujasiri wa kukabiliana uso kwa uso. 

Fransisko kwa wafanyakazi wa Vatican:kazi mnayofanya iwe ni mchango wa amani!

Papa amekutana kiutamaduni kutakiana heri ya Noelli na wafanyakazi wa Vatican katika Ukumbi wa Paulo VI na kuwashukuru kwa kazi wanayofanya Vatican.Amewatakia utulivu kwa familia baada ya janga la uviko-19 lakini mawazo maalum kwa vijana wote kuelewa kuwa migogoro ni sehemu ya ukuaji katika maisha.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Alhamisi 22 Desemba 2022 amekutana na  kiutamaduni wa kutakiana heri ya Noeli na wafanyakazi wa Vatican katika Ukumbi wa Paulo VI na kuwashukuru kufika kwenye mkutano huo ambapo ni wa kubadilishana salamu za Noeli takatifu. Awali ya yote ni lazima kumshukuru Bwana kwa sababu, kwa msaada wake, amesema tumeshinda awamu muhimu ya janga la uviko hivyo  tusisahau. Wakati wa karantiki hakuna aliyejua itakuwaje na lini tutaweza kuwa huru kuzunguka na kukutana. Kisha, mara tu mambo yalipobadilika, tukaoteza kumbukumbu zetu na kuendelea kana kwamba hakuna kilichotokea. Na labda hata hatumshukuru Bwana! Huyu si Mkristo na hata si binadamu, Papa amebainisha na kumbe lazima kushukuru kwa sababu tuliweza kurejea kazini, na pia kujaribu kushinda matatizo fulani makubwa zaidi au machache ambayo yalikuwa yametokea katika kipindi kigumu zaidi.

Papa Francisko amekutana mjini Vatican na wafanyakazi wa Vatican na  Familia zao
Papa Francisko amekutana mjini Vatican na wafanyakazi wa Vatican na Familia zao

Hatupaswi kusahau, kwa sababu kipindi kirefu cha janga hilo kimeacha alama zake. Sio tu nyenzo, matokeo ya kiuchumi; pia imeacha ishara katika maisha ya watu, katika mahusiano, katika utulivu wa familia. Na kwa sababu hiyo baba Mtakatifu amewatakia wote utulivu, kwa kila mmoja wao na kwa familia zao. Utulivu haimaanishi kuwa kila kitu kinaendelea vizuri, kwamba hakuna shida, hapana, haimaanishi hivyo. Familia Takatifu ya Yesu, Yosefu na Maria inatuonesha hilo. Tunaweza kufikiria, walipofika Bethlehemu, Mama Yetu alianza kuhisi maumivu, Yosefu hakujua aende wapi, alibisha hodi kwenye milango mingi, lakini hapakuwa na nafasi... Hata hivyo ndani ya mioyo ya Maria na Yosefu pale ulikuwa ni utulivu wa kimsingi, uliotoka kwa Mungu, na ulikuja kutokana na ufahamu wa kuwa katika mapenzi yake, kuyatafuta pamoja, katika sala na upendo kwa pande zote.

Papa Francisko amekutana na wafanyazi wa Vatican na Familia zao
Papa Francisko amekutana na wafanyazi wa Vatican na Familia zao

Hivyo Papa amewatakia kwamba kila mmoja wao awe na imani kwa Mungu na kwamba katika familia kuna urahisi wa kujikabidhi kwa msaada wake, kumwomba na kumshukuru. Papa Francisko amependa  kuwatakia amani ya utulivu hasa watoto wao, wavulana na wasichana, kwa sababu wameathiriwa sana na kutantini, wamekusanya mvutano mwingi. Ni kawaida, ni jambo lisilohepukika. Lakini hatupaswi kupuuza, ni lazima kutafakari, wajaribu kuelewa, kwa sababu kujitokeza bora kutoka kwenye mgogoro haufanyike kwa viinimacho, ni lazima kufanya kazi wenyewe, kwa utulivu, kwa uvumilivu. Watoto wanaweza kufanya hivyo pia, kwa kawaida kwa usaidizi wa wazazi wao na wakati mwingine watu wengine, lakini ni muhimu kwamba wao wenyewe wafahamu kwamba migogoro ni hatua za ukuaji na zinahitaji kazi juu yao wenyewe. Jambo hilo lilikuwa muhimu na la kwanza ambalo lilimjia akilia  kuanzia  na janga. Ametudia tena kuwatakia utulivu, moyoni mwao, katika uhusiano wa familia yao, katika kazi yao. Na la pili ameeleza jinsi ambavyo wote ni mashuhuda  na wafundi wa amani. Kwa wakati huu katika historia ya ulimwengu, tunaitwa kuhisi kwa nguvu zaidi jukumu la kila mmoja kufanya sehemu yake kujenga amani. Na hii ina maana maalum kwetu sisi tunaoishi na kufanya kazi katika Jiji la Vatican.

Mkutano wa Papa Francisko na wafanyakazi wa Vatican pamoja na familia zao

Si kwa sababu ya nchi hii ndogo sana ulimwengu ina uzito maalum, si kwa sababu hiyo; lakini kwa sababu tunaye kama Kichwa na Mwalimu Bwana Yesu ambaye anatuita kuunganisha kujitolea kwetu kwa unyenyekevu kila siku kwa kazi yake ya upatanisho na amani. Kuanzia katika mazingira tunamoishi, mahusiano na wenzetu, jinsi tunavyokabiliana na kutoelewana na migogoro inayoweza kujitokeza kazini; au nyumbani, katika mazingira ya familia; au hata na marafiki, au katika parokia. Hapo ndipo tunaweza kuwa mashuda na mafundi wa amani. Papa amewaomba kupanda amani. Je ni kwa jinsi gani? Kwa kujini “Kwa mfano: kuepuka kuwasema wengine vibaya nyuma ya migongo yao.

Papa amekutana na wafanyakazi wa Vatican  wakiwa na familia zao
Papa amekutana na wafanyakazi wa Vatican wakiwa na familia zao

Baba Matakatifu amebainisha kuwa "Ikiwa  hatutafanya hivyo, tutakuwa wabunifu wa amani kila mahali! “Ikiwa kuna kitu kibaya, hebu tuzungumze moja kwa moja na mtu anayehusika, kwa heshima, kwa uwazi. Sisi ni jasiri. Tusipuuze na  kisha kumsengenya na watu wengine. Tujaribu kuwa waaminifu na tuone ikiwa hii itafanya kazi”. Papa amehitimisha kwa kuomba wawasalime watoto wao, wazee wao nyumbani. Wao ni hazina katika familia, hazina ya jamii. Papa Papa ana kushukuru  Mungu kwa kila kitu wanachofanya mjini Vatican, kwa kazi yao na pia kwa uvumilivu wao, wakati mwingine, kwa sababu anajua kuna hali ambazo wanatumia uvumilivu: “Asante kwa hilo. Ni lazima sisi sote tusonge mbele kwa subira, kwa furaha, tukimshukuru Bwana atupaye neema hii ya kazi, lakini pia tukilinda kazi na pia kuifanya kwa heshima. Asante kwa hili, asante kwa mnachofanya hapa. Bila ninyi hakuna hata moja ya haya ambayo yangeendelea”, amehitimisha.

Heri ya Noeli kwa wafanyakazi wa Vatican 22 Desemba 2022
22 December 2022, 12:56