Tafuta

2022.11.10 Kasula wa wafungwa waliyo mzawadia Papa Francisko. 2022.11.10 Kasula wa wafungwa waliyo mzawadia Papa Francisko. 

Wafungwa wa Secondigliano wamzawadia Papa Francisko kasula

Papa Francisko alikutana na wawakilishi wa wafungwa wa Gereza la Secondigliano,Napoli mara bada ya katekesi yake ambao ni washiriki wa Maabara mpya iitwayo,“Albus sacer” ya ushonaji wa mavazi.Katika fursa hiyo walimletea na kumzawadia kasula mpya katika matazamio ya Siku ya Maskini duniani itakayofanyika tarehe 13 Novemba.Papa amewatia moyo.

Na Angella Rwezaula, – Vatican.

Watu wa mwisho wanaofikiria walio wa mwisho ndivyo walivyo na ujumbe ambao wamependelea kuuleta kutoka kwa wafungwa walioko kwenye Magereza ya Secondigliano huko  Napoli kwa shauku yao kwamba wanaomba aweze kuivaa katika fursa ya Siku ya Maskini Duniani itakayoadhimishwa katika  Dominika ya 33 ya Kipindi cha Mwaka tarehe 13 Novemba  2022. Ilikuwa ni kipindi cha pekee cha furaha kibinadamu na kiroho kwa mujibu wa maelezo ya  Padre Raffaele Grimaldi, Afisa Msimamizi wa Vikanisa vya Magereza nchini Italia aliyesindikiza uwakilishi huo pamoja na Msimamizi wa Kikanisa cha magereza ya  Secondigliano, Padre Giuseppe Russo na Mkurugenzi wa Gereza hilo Bi Giulia Russo. Maabara hiyo mpya ya mavazi ya kiliturujia imefunguliwa hivi karibuni na hivyo Baba Mtakatifu  Papa aliwatia moyo wa kwenda mbele na wasikate tamaa. Aidha aliwahakikishia kwamba daima amekuwa  na furaha alipokuwa akiingia katika magereza yoyote  kwa sababu kuna uwezekano wa kufunga majeraha ya watu wengi na kukutana na wageni ambao ni  Uso wa Kristo.

Katika jina la Maria daima na kila mahali

Katika kuelezea juu ya Kasula  mpya waliyomzawadia Papa, wamesema waliweka hata alama ya rangi ya  Bikira Maria ambaye anaelezea maana ya mchakato huo walioanza. Maria ni yule anayesindikiza kila mmoja wetu katika maisha, ni yule ambaye anatualika kufanya mapenzi ya Baba na kutuongoza kuelekea kwake  Kristo, alisema Padre Grimaldi. Kazi ya ushonaji ifanywayo na wafungwa ni tunda hata la mafunzo ya kina yenye msingi wake katika Taasisi hiyo. Utaalam ule wa kutengenezaji mavazi ya kiliturujia ambayo ni stola na kasula kwamba ni zoezi linalo karibia zaidi na zaidi katika magereza nyingi katika ulimwengu wa kidini, na itakuwa ni ushuhuda wa ndani na nje katika mchakato unaofanyika.  Katika muktadha kama huo, ulio wazi, si tu wa kutoka katika matukio mengi ya wale wanaojiua, na ambapo kwa mwaka huu wamebainisha hadi sasa nchini Italia wamefikika takribani wafungwa nchini Italia 74,  na kwa maana hiyo kuna haja  ya kufanya uzoefu ili kuepuka majanga mengi na hivyo  kupambana na uzoefu kama huo kwa kujaza vipindi vya utupu kwa  wafungwa ili kuwaondolea mbali na mawazo mabaya ambayo yanaweza kusababishia mabaya walio wadhaifu.

Kazi katika  gerezani inaunda zawadi ya wakati ujao wa mfungwa

Mpango mpya huo unatokana na mchakato ambao tayari unajulikana huko Secondigliano,  Napoli ambao ni ule wa kushona uitwao  “RicuciAMO” na ambao kikweli wakati wa kipinidi cha Janga la Uviko 19 walikuwa wametengeneza barakoa zaidi ya 10,000 ambazo ziligawiwa bure kwenye  mji wote. Kwa maana hiyo Magereza mara nyingi kuna maisha magumu, yasiyo na mpangilio katika jamii kwa mujibu wa Padre Raffaele na kwa niaba ya jina ina maana ya kusisitiza wazi juu ya  lengo la kutaka kushinda, na kuunganisha watu hawa katika maisha na katika jamii. Na kwa upande wa kazi kwa yule anayeishi gerezaji anajua wazi kamba ni chombo muhimu sana na kinachofaa katika lengo  hilo. Kazi kila wakati inaunda na kutoa zawadi ya wakati ujao wa mtu mfungwa, lakini pia inafanya kuwa kiini msingi cha  maisha ambayo hayana budi kupyaishwa licha ya mateso na wakati mwingine hata unyenyekevu. Kwa njia huyo Kanisa linapaswa kuwasindikiza katika kazi ambayo inaokoa kwa sababu kama anavyorudia kusema Papa, kwamba  hakuna anayeweza kujiokoa mwenyewe.

Wafungwa wamzawadia Papa Kasula
11 November 2022, 16:50