Tafuta

Papa Francisko:vurugu dhidi ya wanawake ni kukashifu Mungu

Mara kadhaa Baba Mtakatifu amekuwa akizungumzia juu ya ukiukwaji wa mwili wa wanawake katika mafundisho yake kupitia mahojiano,tweets,hotuba na ujumbe mwingi.Katika Siku ya Kimataifa ya Kupinga vurugu dhidi ya Wanawake,video fupi inakumbusha maneno ya mahubiri tarehe Mosi Januari 2020:Jinsi tunavyochukulia mwili wa mwanamke,ndivyo tunatambua kiwango chetu cha kibinadamu.

Na Angella Rwezaula; – Vatican.

“Ubinadamu, ubinadamu…”,  linasikika neno hilo kwa baadhi ya nyuso za wanawake wanaofanya kazi katika Baraza la Kipapa la Mawasiliano wakirudia kuseka kwa sauti mbali mbali na lugha mbali mbali, nyeti na nguvu, kwa kufanya kuwa mwangwi kwenye video ya maneno ya Baba Mtakatifu Francisko aliyotamka wakati wa mahubiri yake katika siku ya kwanza mnamo tarehe Mosi Januari 2020, katika Siku Kuu ya Mama Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu sambamba na Siku ya Amani duniani. Katika kusisitiza sentensi hiyo ndogo sana ya 'ubinadamu', inawezekana kabisa kuleta umakini na kufupisha kile ambacho zaidi ya wanawake wengi hawana uwezo hata wa kutamka kwa sababu,  wamefungwa na kashfa ya namna mbali mbali na nzito ya mnyororo wa kisaikolojia.

Na katika ujumbe wa miaka miwili iliyopita wakati wa kufungua mwaka, ujumbe wa kulinda hadhi ya wanawake, pia ulikuwa ni mada ambayo tayari kwa wakati uliopita na kila wakati Papa amezidi kusisitiza sana katika hotuba nyingi, ujumbe, tweets na mahojiano. Baba Mtakatifu alisema: "Kuzaliwa kwa upya ubinadamu ulianzia na mwanamke. Mwanamke ni kisima cha maisha. Pamoja na hayo anazidi kukiukwa haki yake, anapigwa, analawitiwa, anapelekwa kwenye ukahaba na kukandamizwa hadi kifikia kutolewa nje kiumbe kilichomo ndani ya umbu lake. Kila vurugu itolewayo kwa mwanamke ni kukashifu Mungu aliyezaliwa na mwanamke. Kutoka katika mwili wa mwanamke wokovu ulifikia kwa ajili ya ubinadamu. Kwa maana hiyo kadiri tunavyouchukulia mwili wa mwanamke, tunaelewa kiwango chetu cha ubinadamu".

Siku ya Kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake ambayo inaadhimisha kila mwaka bado kwa mara nyingine tena ni fursa inayojikita kurudi katika muktadha huo pendwa wa Papa Francisko. Mnamo tarehe 25 Novemba 2021,  katika ukurasa wa @pontifex  alitaja "aina mbalimbali za unyanyasaji ambao wanaoteswa wanawake wengi na kwamba ni woga na udhalilishaji kwa wanaume na kwa wanadamu wote". Na alitualika tusitazame upande mwingine, yaani kugeuza kisogo majanga kama hayo. Ni jamii kwa ujumla ambayo Papa  Fransisko aliitaka na anaitaka leo hii ili isikubali kutojali, na kuchukua hatua madhubuti dhidi ya jambo lenye mikunjo ya hila na ya kulazimisha.

Hakuna kifo na unyonyaji tena! Katika ziara yake ya hivi karibuni  huko Kazakistan, kwenye Kongamano la Viongozi wa kidini, Papa Francisko alitoa  wito kwa viongozi wa kidini na  kusisitiza kwa nguvu kwamba: "wanawake lazima waheshimiwe, watambuliwe na washirikishwe. Kuna mahali ambapo hiyo ni kama  ndoto".  Kwa mfano fikiria Mexico ambako Papa alikwenda mwaka wa 2016, katika ziara ya kitume hadi mipakani na Marekani ambapo aliomba katika nchi isiyojulikana kwa ajili ya umati wa wahamiaji ambao wanapata majaribio ya mara kwa mara ya kulazimishwa kuondoka, lakini kwa bahati mbaya, inayojulikana kwa mauaji ya wanawake, ambapo kwa karibu miaka thelathini kiwango cha juu zaidi cha vifo vya wasichana wadogo kimerekodiwa, kiasi kwamba jambo hilo limefafanuliwa na wengi kuwa ni mauaji ya kweli ya jinsia. Kutoka huko Ciudad Juarez, akiwa na misalaba ya waridi inayoonesha wazi mateso haya ya kikatili, Papa Francisko aliomba na kusema: "Tunaweza kusema nini kuhusu wanawake wengi ambao maisha yao yamechukuliwa isivyo haki? Tumwombe Mungu wetu zawadi ya uongofu, zawadi ya machozi; tumuombe ili mioyo yetu iwe wazi kama watu wa Ninawi kwa wito katika nyuso za mateso za wanaume na wanawake wengi. Hakuna kifo na unyonyaji tena!"

https://youtu.be/LgHrzHaILLE

Papa:Siku ya Kupinga ukatili dhidi ya wanawake
25 November 2022, 09:28