Papa kwa walimu wakatoliki:ukoloni wa kiitikadi unaharibu mwanadamu!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Papa Francisko akikikutana Jumamosi tarehe 12 Novemba 2022 na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Walimu Wakatoliki Ulimwenguni (Umec-Wuct), mtandao wa wafanyakazi katika taaluma na kama kaka na dada katika imani ambao Baba Mtakatifu amefafanua kama katika roho na mtindo wa urafiki, wa kukaribishwa, wa maarifa ya pamoja na ukuaji wa kawaida wa kiroho, na ambao wanajiweka katika huduma ya waalimu wote wa Kikatoliki ili kuhifadhi utambulisho wao na kutekeleza utume wao. Katika msisitizo wake Baba Mtakatifu amewaomba wawe makini kama walimu kueleweka katika kuthibiti jambo ambalo ni jipya la ukoloni wa kiitikadi. Leo hii ukoloni wa kiitikadi unaharibu utu wa binadamu na wanapoingia kwenye elimu husababisha majanga. Papa Francisko amethibitisha kwamba katika kazi hiyo wao ni “washiriki wa Papa”: na kwa hakika, utume wa Mrithi wa Petro ni ule hasa wa kuwaimarisha na kuwategemeza ndugu katika imani (rej. Lk 22:32). Kwa hivyo wao katika ulimwengu wa shule, wanawasilisha huduma ya Kanisa ili kusaidia walimu wa Kikatoliki katika imani, na kwa njia hiyo waweze kutekeleza kazi yao na ushuhuda wao kwa njia bora zaidi, katika hali ambazo mara nyingi ni ngumu juu ya kiwango cha uhusiano na kitaasisi. Kuwepo kwa waelimishaji Wakristo katika ulimwengu wa shule ni jambo la maana sana na mtindo wanaoutumia ndio wenye maamuzi.
Kiukweli, mwalimu wa Kikristo anaitwa kuwa mwanadamu kamili na Mkristo kamili kwa wakati mmoja. Hatakiwi kuwa wa kiroho na kutoka katika ulimwengu huu. Hakuna ubinadamu bila Ukristo. Na hakuna Ukristo bila ubinadamu. Kwa hiyo mwalimu Mkristo lazima asimike mizizi katika wakati uliopo, katika wakati wake, katika utamaduni wake. Ni muhimu kwamba utu wake uwe tajiri, wazi, mwenye uwezo wa kuanzisha uhusiano wa dhati na wanafunzi, kuelewa mahitaji yao ya kina, maswali yao, hofu za ona ndoto zao. Na kwamba awe pia na uwezo wa kushuhudia, kwanza kabisa kwa maisha na pia kwa maneno kwamba imani ya Kikristo inamkumbatia mwanadamu mzima, na inaleta nuru na ukweli kwa kila eneo la uwepo, bila kutenga chochote, bila kukatwa mbawa za ndoto za vijana, na bila kuwafukarisha matamanio yao. Umoja wa Walimu katoliki Ulimwenguni, Papa Francisko amekumbuka, umeishi katika nyakati ngumu katika historia yake ya hivi karibuni hata kwa nyakati za mashaka na kukatishwa tamaa" Lakini pia katika nyakati hizo za dhoruba, hapakuwa na ukosefu wa kujitolea katika roho ya imani ya na matumaini Kikristo.
Umoja huo [Umec] leo hii unaitwa kusaidia walimu wa kila kizazi na katika hali zote za kufanya kazi: wale walio na uzoefu wa muda mrefu, matajiri katika kuridhika lakini pia matatizo na vizazi vipya, walimu waliohuishwa na shauku na tamaa ya kufanya kazi, lakini kwa udhaifu na ugumu wa maisha kutokuwa na hakika ambao mara nyingi huashiria miaka ya kwanza ya ufundishaji . Walimu hawa wote ikiwa tunawatazama kwa mtazamo wa Kikristo, ambao wakati mwingine wao wenyewe hawaelewi kikamilifu wako katika nafasi ya kuacha alama, kwa uzuri au kwa ubaya, katika maisha ya watoto, barubaru na vijana ambao wamekabidhiwa kwa muda mrefu. Ni wajibu ulioje! Na ni fursa iliyoje ya kuwatambulisha, kwa hekima na heshima, katika njia za ulimwengu na za uzima, zikiambatana na akili zao kufungua kiukweli, kwa uzuri, kwa mafunzo! Papa Francisko amesisitiza.
Hatimaye, Papa akihutubia ametoa mwaliko kwa wanachama wa Umoja wa Walimu Wakatoliki Ulimwenguni. Kwamba mwaliko wake uliokuwa ni kutika moyoni sana na ni ule unaohusishwa na Mkataba wa Elimu ya Ulimwenguni, mpango unaolenga kuunganisha juhudi katika muungano mpana wa kielimu wa kutoa mafunzo kwa watu wazima, wenye uwezo wa kushinda mgawanyiko na migogoro na kujenga upya muundo wa mahusiano kwa ubinadamu wa kindugu zaidi . Papa amesema Nina imani na dhamira yenu ya kuwashirikisha walimu ambao ni wanachama wa Umec katika Mpango huu, ambao unalenga kuzingatia utu na uzuri wake, na familia kama masomo ya elimu ya msingi".
Historia na utambulisho wa Umec
Chimbuko la Umoja wa Walimu wa katoliki Duniani ni tangu mwaka 1908. Katika mwaka huu marais wa vyama vya walimu wa Kikatoliki vya Austria, Uholanzi, Uswisi na Ujerumani, wakati wa mkutano ulioandaliwa kushughulikia masuala ya elimu, walizindua wazo la kuwaleta pamoja walimu wa Kikatoliki katika ngazi ya kimataifa. Mnamo 1912 Weltverband katholischer Pädagogen yaani chama cha cha waelimishaji Wakatoliki ulimwenguni,zilikatika. Lakini shughuli za chombo hiki, kilichokatizwa kutokana na vita viwili vya dunia, kilianza tena mnamo mwaka wa 1951 na makao makuu Roma, kwa mpango wa viongozi wa vyama vya kitaifa kutoka nchi 17, za Umoja wa Walimu wa Kikatoliki. Lengo ni kujiweka katika huduma ya vyama vya kitaifa vya walimu wa Kikatoliki ulimwenguni kwa kuratibu shughuli zao za masomo na utafiti ili kufanya mafundisho ya Kanisa katika nyanja ya elimu.