Tafuta

2022.11.10  Papa amekutana na Wakurugenzi na Walezi wa Seminari za Bara la Amerika Kusini. 2022.11.10 Papa amekutana na Wakurugenzi na Walezi wa Seminari za Bara la Amerika Kusini. 

Papa Francisko:Wafundwe mapadre wenye mapigo ya moyo wa Yesu

Katika hotuba iliyokabidhiwa kwa washiriki wa Kozi ya wakurugenzi na wafundaji wa seminari za Amerika ya Kusini na visiwa vya Carribien,Baba Mtakatifu,anasisitiza juu ya motisha halisi wa kitaaluma ambao ni kumfuasa Bwana na kukarabati Ufalme wa Mungu.Wote wanaohusika katika malezi ya kipadre wanaalikwa kuelimisha kwa ushuhuda wa maisha yao,zaidi ya maneno yao.

Na Angella Rwezaula -Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Alhamisi tarehe 10 Novemba 2022 amekutana mjini Vatican na washiriki wa Kozi ya Wakurugenzi  na Wafundaji wa Waseminari kutoka  karibu nchi zote za Bara la Amerika Kusini na visiwa vya Carribien. Papa Francisko amependa kuwakabadhi hotuba aliyoitayarisha  wajisomee na ambayo tunawaletea kile ambacho alitayarisha. Katika hotuba hiyo, kwanza kabisa ametoa salamu kwa Kardinali, maaskofu wote wanaowasindikiza. Ameshukuru Baraza la Kipapa la Makleri  walioandaa kozi hiyo na kwamba Mafunzo ya Kikuhani kwa namna ya pekee ya wachungaji wajao ni kiini cha Unjilishi, kwa kuwa katika miaka mingine ijayo wao watoa jibu  kwa hakika la wito wa maana ya  kuuishi na kuongoza Watu Watakatifu wa Mungu  ili kwamba Kristo aweze kuwa Sakramenti au ishara na chombo cha kina cha muungano na Mungu na cha umoja kwa binadamu wote. Ni jinsi gani ilivyo na ulazima wa kuwa na mafunzo  bora kwa wale ambao watakuwa ni uwepo wa Sakramenti ya Bwana katikati ya zizi lake, wakimwilisha na kutunzwa kwa Neno na kwa Sakramenti!

Papa amekutana na wakurugenzi na walezi wa Seminari kutoka bara la Amerika Kusini lote
Papa amekutana na wakurugenzi na walezi wa Seminari kutoka bara la Amerika Kusini lote

Papa Francisko anapenda kusisitiza kwamba Ratio fundamentalis institutionis sacerdotalis, yaani  zawadi ya wito wa kikuhani, inahifadhi msaada mkubwa wa Waraka wa Kitume wa Pastores dabo vobis, ambayo mwaka huu imetimiza miaka 30 tangu kuchapishwa kwake na Mtakatifu Yohane Paulo II, baada ya Mkutano Mkuu wa VIII wa Kawaida wa Maaskofu ambao walikabiliana na mada kuhusu “La formazione dei sacerdoti nelle circostanze attuali”, yaani Mafunzo ya kijibu haja ya muktadha wa sasa. Wosia ule ulitoa kwa namna wazi maono ya [kiantropolojia] ubinadamu fungamani  ambao unazingatia kwa maana ya  haraka na usawa, kwa mantiki nne zilizomo katika mtu, mseminari ambazo ni ubinadamu, akili, kiroho na kichungaji. Kwa upande mwingine, waraka huo huo Ratio fundamentalis ulithibitishwa tena matarajio ya mfuasi wake Papa Mstaafu Benedikto XVI ambaye kwa Motu  proprio Ministrorum institutio, aliweka bayana kwamba mafunzo ya waseminari yanafuata n ana  asili, katika malezi ya kudumu kwa makuhani  kwa kuwekwa katika hali zote sawa  hizo mbili.

Baba Mtakatifu Francisko hata hivyo amesisitiza kwamba msaada huo kwa sasa wa Ratio fundamentalis ni ambao unafafanua mchakato wa mafunzo ya kikuhani  tangu miaka ya kwanza ya malezi ya kisemiari kuanzia na misingi minne yenye tabia ya mafunzo ambayo inawakilishwa kama  njia pekee, fungamani, kijumuiya na kimisionari. Kwa pendekezo hilo, Papa Francisko amependa kujikita katika  kufafanua mafunzo ya kikuhana ambayo amesema yanatabia muhimu sana ya kijumuyia tangu asili yake, wito wa kikuhani kiukweli ni zawadi ambayo Mungu anaifanya kwa Kanisa na kwa ulimwengu, njia moja kwa ajili ya kujitakatifuza na kutakatifuza wengine ambayo haipaswi kueleweka kama ya kibinafasi, badala yake iwe njia ya kuhuishwa kupenda kwa dhati Watu wa Mungu. Katika hilo Baba Mtakatifu ameonesha  wazi moja ya changamoto muhimu zaidi ambayo leo hii wanapaswa wakabiliane naye katika nyumba za malezi ya kikuhani kwa sababu amesisitiza kuwa  lazima wawa jumuiya ya kweli ya kikristo, ambayo haitakiwi kuwa mpango wa mafunzo ya dhati tu, lakini hata idadi inayostahili ya waseminari na wafundaji ambao wanahakikisha uzoefi wa kweli wa jumuiya katika mantiki nzima ya mafunzo. Hata hivyo changamoto  haikosekani,  ambayo inahitaji jitihada za kuunda au kudumusha waseminari kijimbo, kimkoa au kikanda.  Hii ni kazi ambayo maaskofu lazima wawajibike katika Sinodi  kwa ngazi ya Baraza la Maaskofu wa Kikanda na  ya kitaifa, zoezi ambalo wao wanaitwa kushirikishana kwa uhalisia na ubunifuni. "

Papa Francisko anafurahi kwamba wakati wa mikutano yao, wamefakari juu ya mantiki za mafunzo ya mawazo, kwa kujikita juu ya maana ya ubinadamu na juu ya kufungamanisha mantiki nyingine ziwe za kiroho, kiakili na kichungaji. Kiukweli, ndani ya jumuiya ya Kikristo, Bwana anawaita baadhi ya wanafunzi wake kuwa makuhani, yaani, yeye huchagua baadhi ya kondoo kutoka katika kundi lake na kuwaalika wawe wachungaji wa kaka na dada zao. Kwa maana hiyoamesema kwamba hawapaswi kusahau kwamba wao kama makuhani wamechukuliwa kutoka kwa wanadamu ... kwa faida ya wanadamu katika mambo yanayomhusu Mungu (Taz. Waheb 5:1). Wao  ni “wanafunzi-wenza” wa Wakristo wengine waaminifu na kwa sababu hiyo hiyo wanashiriki mahitaji yale yale ya kibinadamu na ya kiroho,na wakati huo huo wako chini ya udhaifu huo huo, mapungufu na makosa. Kwa waseminari, kama katika kila mmoja wao wa mapadre Papa amebainisha, mambo mawili ambayo yanaingiliana na kuishi pamoja ambayo yanapaswa kukamilishana. Kwanza ni karama za neema na tabia za asili iliyojeruhiwa. Pili huduma ambayo lazima waifanye ni kuunganisha ukweli wote katika safari ya imani na ukomavu kamili. Wanahitaji kuwa waangalifu, kwani dhamira yako sio kufunda watu maarufu,  wanaodai kujua kila kitu  na kudhibiti kila kitu na kujitosheleza; kinyume chake, ni kufunda watu wanaofuata kwa unyenyekevu mchakato uliochaguliwa na Mwana wa Mungu, ambao ni njia ya Umwilisho. Ndiyo, kwa nguvu ya Umwilisho wa Mwana wa Mungu, wanapata kutoka  kwa Bwana wetu, Mungu na mwanadamu wa kweli, na sio mifano ya ubinadamu upya ya kuiga tu, lakini pia uwezekano wa kuingia katika umoja ulio hai pamoja Naye kuanzia na uwepo wao.

Papa amekutana na wakurugenzi na walezi wa Seminari kutoka bara la Amerika Kusini lote
Papa amekutana na wakurugenzi na walezi wa Seminari kutoka bara la Amerika Kusini lote

Wao wameponywa na kuinuliwa kwa ubinadamu mpya. Baba Mtakatifu ameongeza kwa kunukuu kifungu cha Paulo kwamba Bwana hutuwezesha sisi kumwiga na kufuata nyayo zake, kwa kuwa yeye anatujulisha zawadi ya neema yake, ambayo inaweza kubadilisha kila kitu tulivyo katika nafsi, mwili na roho (rej. 1 Thes 5:5).:23), kulingana na mpango wake wa utimilifu kwa kila mmoja wetu. Kwa hiyo, mwelekeo wa kibinadamu wa malezi ya kipadre si shule ya wema, ukuaji wa utu wa mtu au maendeleo ya kibinafsi tu, lakini pia  kwanza kabisa  unamaanisha ukomavu kamili wa mtu aliyeimarishwa na neema ya Mungu ambayo, wakati wa kuzingatia kibiolojia, hali ya kisaikolojia na nyanja za kijamii za kila mmoja, ni uwezo wa kubadilisha na kuinua, hasa wakati mtu na jamii wanajitahidi kushirikiana naye kwa njia ya uwazi na ukweli. Hatimaye, misukumo ya kweli ya kiutendaji, yaani, kumfuata Bwana na kuanzishwa kwa Ufalme wa Mungu, ni msingi wa mchakato ambao ni wa kibinadamu na wa kiroho. Kwa maana hiyo, moja ya kazi muhimu zaidi katika mchakato wa malezi ya kikuhani ni kusoma hatua kwa hatua kwa imani ya historia yake mwenyewe. Mwonekano huo  uangalizi wa safari ya mtu mwenyewe ndilo somo kuu la utambuzi wa kibinafsi na wa kikanisa wa wito wa mtu. Kwa hakika, kila mseminari kwanza na kila padre baadaye, kwa lugha yake ya kuzaliwa tofauti, lazima aendelee kusasisha, hasa katika mazingira muhimu zaidi ya safari yake ya kipadre (taz. RFIS, nn. 59 na 69). Mgongano na wale wanaosindikiza katika mchakato huo, katika maungamo ya ndani na nje, utamruhusu kushinda majaribu yoyote ya kujidanganya na itaruhusu tathmini ya mitazamo mipana zaidi na yenye lengo kuu zaidi. Ni lazima pia kufahamu matokeo ya  kimaumbile ambayo maisha na huduma ya waanzilishi kwa waseminari.

Papa amekutana na wakurugenzi na walezi wa Seminari kutoka bara la Amerika Kusini lote
Papa amekutana na wakurugenzi na walezi wa Seminari kutoka bara la Amerika Kusini lote

Kwa maana huyo Baba Mtakatifu amebainisha kwamba  wafundaji huelimisha kwa shuhuda ya maisha yao, zaidi ya maneno yao.  Kwa kawaida, ukomavu wa afya wa binadamu unaoendana na ujumuishaji wa wito na utume wa mtu, unaojumuisha hushinda kwa kawaida shida na vipindi vya shida, ambpo humruhusu kuhani  mfundaji kufanya  kwa upya kila wakati msingi ambao unajipyaisha kwake kwa Kristo, Mtumishi na Mchungaji Mwema na pia humkabidhi vyombo vyenye ufanisi zaidi kwa ajili ya utekelezaji wa huduma yake katika  malezi kwa waseminari, pamoja na watahiniwa kuhusu mchakato wao wa utambuzi, na pamoja na wafundaji wengine wa kikundi cha malezi na mawakala wengine wa malezi. Kwa hakika, maelewano ya kibinadamu na kiroho ya wakuu  hasa mkuu wa seminari, ni mojawapo ya upatanisho muhimu zaidi katika usindikizaji wa malezi. Moja ya viashiria vya ukomavu wa kibinadamu na wa kiroho ni ukuaji  na ujumuishaji wa uwezo wa kusikiliza na sanaa ya mazungumzo, ambayo kwa asili yanashikilia maisha ya sala, ambapo kuhani huingia katika mazungumzo na Bwana kila siku, hata kwa muda mfupi, na ya ukavu hadi kufikia kuchanganyikiwa. Kwa ajili ya huduma ambayo kuhani huwapatia kaka na dada zake, hasa kwa ajili ya kazi ya mtayarishaji, mfundaji,  husikiliza na uhurumia wengine, zaidi ya chombo cha uinjilishaji, na ndiyo hasa eneo ambalo  linapaswa kustawi na kuzaa matunda. Kwa ufupi maisha ya wafundaji, ukuaji usioisha wa kibinadamu na kiroho kama mfuasi- mmisionari wa Kristo na kama kuhani, anayesaidiwa na kuhamasishwa na neema ya Mungu bilashaka ni jambo msingi ambalo linahitajika kwa ajili ya kuweza kufanya huduma yake kwa waseminari na makuhani wengine katika kumfanana Kristo, Mtumishi na Mchungaji Mwema. Kiukweli maisha yake ya ushuhuda ambayo maneno yake na ishara zake zinataka kuelezea wazi kwenye mazungumzo na katika kuwasiliana na wenzake ambao anawafundisha katika mafunzo.

Papa Francisko amebainisha alivyo na utambuzi kuwa huduma wanayotoa katika Kanisa siyo rahisi, na mara nyingi haikosi changamoto za ubinadamu, kwa sababu mfundaji anao mwoyo asimilia mia moja wa kibinadamu na sio mara chanche anakumbana na majaribu, uchovu, hasira, na kukosa nguvu, na kutoka hapo ndipo kuna umuhimu wa kukimbilia kila siku kwa Yesu, kupiga magoti na kwa uwepo wake kujifunza kutoka kwake ambaye ni mpole na mnyenyekevu wa Moyo, kwa namna ambayo kidogo kidogo moyo wetu unafunguka na kudunda kama moyo wa Mwalimu. Sura za Injili hasa zile ambazo zinatoa muundo wa maisha  ya Yesu, na mitume wake, zinaruhusu kuona jinsi ambavyo Yesu alikuwa anajua kuonesha wakati uliopo au kutokuwapo, alijua kuwa ilikuwa wakati mwafaka wa kusahishisha au wa kusifu, wakati wa kusindikiza au fursa kwa ajili ya kutuma na kuacha kwamba mitume wanakabiliana na changamoto za kimisionari. Ni kati kati ya hao tunaweza kuiita hotuba za mafunzo ya Kristo kwa Petro, Andrea, YaKobo, Yohana na  wengine walioitwa, wakawa wafuasi wa kweli na kufanana taratibu, na moyo wao kama ule wa Bwana. Baba Mtakatifu Francisko amekumbusha alivyo elezea juu ya  nafasi ya malezi kama mkuu wa  Seminari kulinganisha na kaka zake wa  kikundi cha malezi  na katika uwajibikaji kwa wote katika mafunzo binafsi ya kikuhani. Mkurugenzi wa Seminari anapaswa ajionesha wasi wasi usiosha kwa ajili ya kila  mlezi kwa kuhifadhi mazungumzo yaliyofunguka na wazi kulingana  na maisha yake na huduma yake  bila kufuata mkubwa wa  mwangwi kwa umakini zaidi wa kibinafsi ambao mara nyingi unategemea kushinda matatizo ambayo yanaweza kuzaliwa ndani ya kikundi cha walezi.  Wafundaji lazima wawe karibu na mkuu wa seminari kama kaka yao wa karibu zaidi na  lazima awaelekeze kwa namna ya upendeleo wa  mazoezi ya upendo wa kichungaji.

Papa amekutana na wakurugenzi na walezi wa Seminari kutoka bara la Amerika Kusini lote
Papa amekutana na wakurugenzi na walezi wa Seminari kutoka bara la Amerika Kusini lote

Kwa upande mwingine mafunzo ya kikuhani yana kama chombo muafaka cha kusindikiza malezi na kiroho kwa wote na kila mfundaji wa waseminari kulingana na wote na kila mseminari kwa namna ya kuhakikisha kwamba kuna upendo na msaada mbali mbali kwa upande wa jumuiya ya wafundaji, bila ubaguzi na wala upendeleo, kwa kusaidiwa na makuhani tofauti wa umri na umakini tofauti, kwa mujibu wa uwezo maalum wa kila mmoja wao, ili kila wakati ujao wa kichungaji, uweze kung’amua na kudumisha, sio tu urahisi wa wito wa kikuhani, lakini  pia hata kwa namna binafsi na isiyorudiwa ambayo Bwana ameweka kwa sasa na iwe hai na kufanyiwa mazoezi. Wanachangia kwa kusindikizwa na wafundaji wa watu wengine ambao wanasadia waseminari katika makuzi yao ya kibinadamu na kiroho. Hapo lazima kuwakumbuka wadau wawajibikaji wa uzoefu wa kichungaji waliojikita katika kozi ya mafunzo ya mwanzo kwa namna ya pekee maparoko, kama ilivyo hata wataalam ambao wameitwa kushirikiana ikiwa ni lazima. Baba Mtakatifu kwa maana hiyo kwa amependa kuelezea kwa upya shukurani kwa Kanisa kwa sababu yao wanaojikita katika maisha yao na katika utume wa wachungaji wajao ambao watakuwa kaka zao katika ukuhani na ambao kwa kuungana chini ya uongozi wa Askofu watatupa nyavu za Injili kama wavuvi wa kweli wa watu. Na Maria Mtakatifu, Mama wa Makuhani awatie nguvu na kuwalinda katika utume wao.

Papa akutana na walezi wa Seminari za Bara la Amerika Kusini
Hotuba ya Papa Francisko kwa wakurugenzi na walezi wa waseminari II
10 November 2022, 16:37