Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amesikitishwa na taarifa za shambulio jipya na kali zaidi la kombora dhidi ya Ukraine. Baba Mtakatifu Francisko amesikitishwa na taarifa za shambulio jipya na kali zaidi la kombora dhidi ya Ukraine. 

Papa Francisko Asikitishwa na Shambulio la Kombora Nchini Ukraine, Ataka Majadiliano

Hili ni shambulio ambalo limesababisha maafa makubwa. Papa anawaalika waamini kuungana pamoja naye ili kumlilia Mwenyezi Mungu, aweze kuwaongoa viongozi ambao wanaendelea kuchochea vita, ili waweze kujikita katika majadiliano yanayosimikwa katika ukweli na uwazi, ili haki na amani viweze kutawala tena na hatimaye, kukomesha vita kati ya Ukraine na Urusi!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Jumuiya ya Kimataifa imelaani vikali shambulizi la kombora lililofanywa na Jeshi la Urusi nchini Ukraine Jumanne tarehe 15 Novemba 2022 na hivyo kupelekea watu kadhaa kupoteza maisha pamoja na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundo mbinu kati kati ya mji mkuu wa Kyiv. Wachunguzi wa mambo ya kivita wanasema kwamba, zaidi ya makombora 70 tayari yamekwisha kushambulia Ukraine na kusababisha hasara kubwa kwa maisha ya watu na mali zao. Maeneo mengi nchini Ukraine hayana nishati ya umeme kutokana na mashambulizi haya yanayotishia amani, usalama na mafungamano ya Jumuiya ya Kimataifa.

Papa Francisko asikitishwa na shambukio ka kombora dhisi ya Ukraine.
Papa Francisko asikitishwa na shambukio ka kombora dhisi ya Ukraine.

Ni katika muktadha huu, Baba Mtakatifu Francisko Jumatano tarehe 16 Novemba 2022 wakati wa Katekesi yake, amesikitishwa na taarifa za shambulio jipya na kali zaidi la kombora dhidi ya Ukraine. Hili ni shambulio ambalo limesababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao. Baba Mtakatifu anawaalika waamini kuungana pamoja naye ili kumlilia Mwenyezi Mungu, aweze kuwaongoa viongozi ambao wanaendelea kuchochea vita, ili waweze kujikita katika majadiliano yanayosimikwa katika ukweli na uwazi, ili haki na amani viweze kutawala tena na hatimaye, vita kati ya Ukraine na Urusi viweze kukoma kabisa.

Kombora Ukraine
16 November 2022, 16:30