Papa amteua Kamishna maalum ili kuipa ari Caritas Internationalis!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Shirika la Caritas Internationalis linamsaidia Baba Mtakatifu na Maaskofu katika kutekeleza huduma yao kwa maskini na wahitaji zaidi, wakishiriki katika usimamizi wa dharura za kibinadamu na kushirikiana katika uenezaji wa upendo na haki ulimwenguni kwa mwanga wa Injili na mafundisho ya Kanisa Katoliki. Ili kuboresha utendakazi wa dhamira hiyo, inaonekana ni muhimu kupitia kwa upya mfumo wa sasa wa udhibiti ili kuufanya uweze kufanya vizuri zaidi kwa kazi za kisheria za Shirika, na pia kuandaa uchaguzi utakaofanyika kwa Mkutano Mkuu ujao . Kwa nia kubwa ya kupendelea upyaishaji wa taasisi Baba Mtakatifu Francisko wamemteua Dk. Pier Francesco Pinelli kuwa Kamishna Maalum wa Caritas Internationalis, ili aweze kuongoza kuanzia tarehe 22 Novemba 2022 kwa muda kwa amri ya Kiti cha Kitume Vatican, akiwa na madaraka yote ya uongozi, kwa mujibu wa sheria ya kawaida na Sheria na Kanoni za Shirika na kitivo kamili cha kongoza ikiwa itaona inafaa au ni muhimu.
Kwa kuingia pamoja na kuanza kutumika kifungu hicho, Wajumbe wa Baraza la Uwakilishi na Halmashauri Kuu, Rais na Makamu wa Rais, Katibu Mkuu, Mweka Hazina na Msaidizi wa kikanisa wanasitisha shughuli katika ofisi hiyo. Kamishna maalum atasaidiwa katika majukumu yake na Dk. Maria Amparo Alonso Escobar akiasaidiwa na Mheshimiwa Padre Manuel Morujão, S.I., kwa ajili ya kuwasindikiza wafanyakazi na kiroho, katika kutazamia masasisho ya Sheria na Kanuni za Caritas Internationalis, kwa utendaji wao na ufanisi zaidi, kuliongoza Shirika katika maandalizi ya Mkutano Mkuu ujao. Katika kazi ya mwisho ya kamishna maalum atakuwa karibu na Kardinali Luis Antonio G. Tagle, ambaye hasa ajajikita kutunza mahusiano na Makanisa mahalia na Mashirika Wanachama wa Caritas Internationalis. Kamishna Maalum atafanya hivyo kwa hatua ya makubaliano na Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu.
Katika miaka ya hivi karibuni tumeona ongezeko kubwa la mahitaji ya watu wengi wanaosaidiwa na Caritas, na ni muhimu kwamba Caritas Internationalis imejiandaa vyema kukabiliana na changamoto hizi,” alisema Kadinali Michael Czerny SJ, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu (DSSUI). Na kwamna “Papa Francisko anatualika kuzingatia ‘utume ambao Caritas inaitwa kutekeleza katika Kanisa... Hisani si utendaji tasa au sadaka rahisi kutolewa ili kunyamazisha dhamiri zetu. Jambo ambalo hatupaswi kusahau kamwe ni kwamba upendo una asili na asili yake katika Mungu mwenyewe (rej. Yn 4:8); upendo ni kumbatio la Mungu Baba yetu kwa kila mtu, kwa namna fulani kwa walio wadogo na wanaoteseka, ambao huchukua nafasi ya upendeleo katika moyo wake (Mei 27, 2019). Maneno yake yanawatia moyo wote wanaohusika kuhakikisha Carits Internationalisi (CI) inatimiza dhamira yake.” Baada ya kuzingatia matokeo ya uthibitishaji na kuhamasishwa kusaidia kuleta (CI) katika kiwango kinachostahili dhamira yake, DSSUI itaendelea kutumia "utaalamu" wake kwa ajili ya Caritas Internationalis, kuhimiza utatuzi wa masuala yaliyoangaziwa katika uthibitishaji uliofanywa nje na tume. Kwa kuzingatia umuhimu wa dhamira ya (CI) na uharaka wa kuboresha usimamizi wake, tunatazamia sala na tunatumaini msaada wa kila mtu.
Na katika taarifa iliyotolewa na Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani kuhusiana na muktadha wa uteuzi wa Papa, wamebainisha kwamba kwa mujibu wa katiba mpya ya kitume ya, 'Praedicate Evangelium', yaani 'Hubirini Unjili' Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu (DSSUI) "inatumia uwezo uliowekwa na sheria kwa Kiti Kitakatifu katika kuanzisha na kusimamia vyama vya misaada ya kimataifa na Mfuko ulioanzishwa sawa na madhumuni, kulingana na yale yaliyowekwa katika Sheria husika na kwa kufuata sheria ya sasa(Art 174 § 3) ya uwezo wake wa Caritas Internationalis (...), kwa mujibu wa kanuni yake (Art 174 § 2). Katika mchakato wa mwaka huu, Baraza la Kipapa la Huduma ya maendeleo Fungamani ya Binadamu (DSSUI) iliagiza ukaguzi wa shirika na ustawi wa kazi wa Sekretarieti Kuu ya CI na upatanisho na maadili ya Kikatoliki ya hadhi na heshima ya kila mtu. Uhakiki huo ulifanywa na tume ya wataalam huru; pamoja na Bwana Pinelli, Padre Enrico Parolari na Dk. Francesca Busnelli, wote wanasaikolojia, walikuwa sehemu ya tume. Wafanyakazi wa Caritas Internationalis (CI), pamoja na wafanyakazi wa zamani na washirika, walialikwa kushiriki katika ukaguzi. Kazi iliyofanywa haikufichua ushahidi wowote wa usimamizi mbaya wa kifedha au tabia isiyofaa ya asili ya unyanyasaji, lakini wakati huo huo masuala na maeneo ambayo yanahitaji uangalizi wa haraka yaliwekwa katia nuru. Kwa maana hiyo yalibainishwa mapungufu yanayohusiana na taratibu za usimamizi na matoke hasi pia kwa moyo wa timu na ari ya wafanyakazi.
Caritas Internationalis ni shirikisho la mashirika 162 ya Kikatoliki ya misaada, maendeleo na huduma za kijamii yanayofanya kazi katika nchi na maeneo zaidi ya 200 duniani kote. Dhamira ya mashirika wanachama ni kufanya kazi ili kujenga ulimwengu uwe bora, hasa kwa maskini na wanaokandamizwa. Caritas Internationalis ni muungano kwa maana hiyo wa mashirika ya kitaifa ya Caritas na ina ofisi yake iliyosajiliwa Vatican chini ya Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu (DSSUI) ina mamlaka juu ya Caritas Internationalis.