Papa amewandikia barua waukraine baada ya miezi tisa tangu kuibuka kwa vita
Na Angella Rwezaula; – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Ijumaa tarehe 24 Novemba 2022, ameandika Barua kwa watu wa Ukraine katika siku ambayo inakumbusha uvamizi wa Urussi nchini Ukraine miezi tisa iliyopita. Katika barua hiyo Papa amebainisha kwamba katika ardhi yao kwa muda wa miezi tisa, uwazimu wa kipuuzi wa vita umetolewa. Katika anga lao sauti mbaya ya milipuko na sauti ya kutatanisha ya ving'ora vinasikika bila kukoma. Miji yao inapigwa na mabomu huku mvua ya makombora ikisababisha vifo, uharibifu na maumivu, njaa, kiu na baridi. Katika mitaa yao, wengi wamelazimika kukimbia, wakiacha nyumba zao na wapendwa wao. Kando ya mito yao mikubwa inatiririka mito ya damu na machozi kila siku. Kwa maana hiyo baba Mtakatifu anapenda kuunganisha machozi yake na yao na kuwaambia kuwa hakuna siku ambayo hayupo karibu na wao na wala bila kuwabeba moyoni mwake na katika maombi yake. Maumivu yao ni maumivu yake. Katika msalaba wa Yesu leo hii anawaona, wanavyoteseka kwa hofu inayotokana na uchokozi huo. Ndiyo, msalaba ambao ulimtesa Bwana unaishi katika mateso yanayopatikana katika maiti, katika makaburi ya alaiki yaliyogunduliwa katika miji mbalimbali, katika wale na katika picha nyingine nyingi za umwagaji damu ambazo zimeingia ndani ya nafsi zetu, ambazo huinua kilio cha kujiuliza ni kwa nini? Je watu wanawezaje kuwatendea watu wengine hivyo?
Historia nyingi za kuhuzunisha
Historia nyingi za kuhuzunisha ambazo tumejifunza kuzihusu Baba Mtakatifu amesema ssinamjia akilini. Kwanza kabisa wale wadogo: ni watoto wangapi waliouawa, kujeruhiwa au yatima, walioraruliwa kutoka kwa mama zao! “Ninalia na ninyi kwa kila mdogo ambaye, kwa sababu ya vita hivi, amepoteza maisha yake, kama Kira huko Odessa, kama Lisa huko Vinnytsia, na kama mamia ya watoto wengine: katika kila mmoja wao ubinadamu wote umeshindwa. Sasa wako tumboni mwa Mungu, wanaona shida zao na wanaomba yaishe”. Papa ameongeza kusema je inawezekanaje tusihisi uchungu kwa ajili yao na kwa wale wote, vijana kwa wazee, ambao wamefukuzwa? Maumivu ya akina mama wa Kiukreni hayawezi kuhesabiwa. Papa amefikiria juu yao, vijana, ambao ili kutetea kwa ujasiri nchi yao ilibidi kuchukua silaha badala ya ndoto walizoziota kwa siku zijazo; Anawafikiria wanawake waliofiwa na waume zao, lakini kwa kuuma midomo yao waendelee kwa ukimya, kwa heshima na azma, kutoa kila sadaka kwa ajili ya watoto wao; kwao, watu wazima, ambao hujaribu kwa kila njia kulinda wapendwa wao; kwao, wazee, ambao badala ya kuwa na machweo ya amani walitupwa katika usiku wa giza wa vita; kwa hao wanawake waliodhulumiwa na wenye mizigo mizito mioyoni mwao; kwao wote waliojeruhiwa mwilini na rohoni. Anawafikiria na yuko karibu nao kwa upendo na mshangao kwa jinsi wanavyokabili majaribu magumu kama hayo.
Watu wa kujitolea, wachungaji na watawa
Na amewafikiria watu wa kujitolea, ambao hutoa huduma kila siku kwa ajili ya watu; kwa, Wachungaji wa watu watakatifu wa Mungu, ambao mara nyingi kwa hatari kubwa kwa usalama wao wamekaa karibu na watu, wakileta faraja ya Mungu na mshikamano wa ndugu, kwa ubunifu kubadilisha maeneo ya jumuiya na makao ya watawa kuwa makao ambapo wanaweza kutoa ukarimu, misaada na chakula kwa wale walio katika hali ngumu. Tena, Baba Mtakatifu amewafikiria wakimbizi na wakimbizi wa ndani, ambao wanajikuta wako mbali na makazi yao, ambao wengi wao wameharibiwa; na kwa Mamlaka wanazoziombea: zina wajibu wa kutawala nchi katika nyakati za majonzi na kufanya maamuzi ya kuona mbali kwa ajili ya amani na kuendeleza uchumi wakati wa uharibifu wa miundombinu mingi muhimu, mjini na mashambani. Baba Mtakatifu Francisko ameandika kwamba katika bahari hii yote ya uovu na maumivu, miaka tisini baada ya mauaji ya halaiki ya Holodomor ameshangazwa na bidii yao nzuri. Licha ya janga kubwa linaloendelea, watu wa Ukraine hawajawahi kukata tamaa au kuachwa kwa huruma. Ulimwengu umetambua watu shupavu na wenye nguvu, watu wanaoteseka na kusali, kulia na kupigana, kupinga na kutumaini: watu waungwana na waliouawa kishahidi. Papa amebainisha kwamba anaendelea kuwa karibu nao, kwa moyo wake na kwa maombi, na wasiwasi wa kibinadamu, ili wahisi kuwa wanasindikizwa, ili wasizoe vita, ili wasiachwe peke yao leo na zaidi ya yote kesho, wakati labda kutakuwa na jaribu la kusahau mateso yao.
Hali halisi ya baridi na siku kuu ya kuzaliwa kwa Bwana
Katika miezi hii, ambayo ugumu wa hali ya hewa hunafanya kile wanachokiona kuwa mbaya zaidi, amependa kusema kwamba upendo wa Kanisa, nguvu ya sala, nzuri ambayo kaka na dada wengi katika maeneo yote wawakupenda kuwapatia busu. Katika wiki chache zijazo itakuwa Siku kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana na mateso makubwa yatazidi kuonekana zaidi. Lakini Papa amependa kurudi pamoja nao huko Bethlehemu, kwa kesi ambayo Familia Takatifu ilipaswa kukabiliana nayo usiku huo, ambapo ilionekana baridi na giza tu. Badala yake, nuru haikutoka kwa wanadamu, bali kwa Mungu; si kutoka duniani, bali kutoka Mbinguni. Mama yake na Mama yetu, ambainisha awalindie. Kwa Moyo wake Safi, kwa umoja na Maaskofu wa ulimwengu, aliyoweka wakfu Kanisa na ubinadamu, hasa nchi yao na Urussi. Kwa Moyo wake wa Kimama anawasilisha mateso yao na machozi yao. Kwa yule ambaye, kama mwana mkubwa wa nchi yao aliandika, kuwa “aliyemleta Mungu katika ulimwengu wetu", tusichoke kamwe kuomba zawadi ya amani inayotamaniwa sana, tukiwa na uhakika kwamba "hakuna lisilowezekana kwa Mungu” (Lk 1) :37). Na atimize matazamio ya haki ya mioyo yao, awaponye majeraha yao na awape faraja yake. Papa yupo pamoja nao na anawaombea na wao wamwombee.